Nimekataliwa kuoa kisa mimi mwislam

Nimekataliwa kuoa kisa mimi mwislam

msumeno

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2009
Posts
2,826
Reaction score
1,738
Waungwana nisaidieni, nimekataliwa kuoa kisa mimi mwislam, wakwe wanasema sifa zooote ninazo ila dini yangu eti sisi wengi wetu ni magaidi, bibie yeye yuko radhi tufunge ndoa bila ridhaa ya wazazi ila mimi naona haiwezekani hususan kwa tuhuma hii ya kidini, sasa wanajamii mnanishauri nini na upande wa dini je inaswihi ndoa ya ilofungwa bila ridhaa ya wazazi,, habari hii si ya kubuni hivyo naomba muelewe hivyo
 
kwa mujibu wa misingi ya kiislam inaswihi ikiwa wazazi hawana sababu za msingi.ila kijamii ni hatari.mtapigwa na dhoruba ambayo hamtaiweza.chakufanya tumieni uwezo wenu wa kidiplomasia kuwashawishi wazazi.kuhusu waislam kuhusishwa na fujo;tuwalaumu watu jamii ya kina ponda ndo waaotufikisha hapa.
 
Can you do without her?
Can you change dini?
Can you do without the consent of ur inlaws?

Majibu ya haya maswali yatakusaidia kufanya decision l think.
 
mkuu usifanye kosa kuoa bila ridhaa ya wazazi, maana maisha ni zaidi ya watu wawili.. jadilianeni vizuri na mkeo... usitumie jazba swala la muda tu litaamua "time will tell'
 
Badili dini wewe au yeye ama songa mbele ...:confused2:
 
We oa bila ridhaa kisha siku ya siku hatuombei ila imetokea bibie yupo hoi bin taaban au ameenda ahera sijui utafanyeje??
Na familia zetu hizi za kitanzania.
Diplomasia ichukue mkondo ukiona haiwezekani jua huyo si mke wako bado hujakutana na wakwako.
Siku ukimpata hakutakuwa na vikwazo mambo mteremko tu.
 
hivi waislamu bado hamjajua mlivyo na jina baya nchini? yaani hata wewe vitendo vya wenzio mliohadaika nao na hii imani ya waarabu huvioni tu?
 
Hili shauri linaweza kutatuliwa na wewe, yeye wazazi wake, wazazi wako na ndugu zenu.., ushauri mwingine is immaterial sababu reaction za watu tofauti zipo tofauti na ukioa bila wazazi kukubali unaweza ukafanikiwa au usifanikiwe na wazazi wakakusamehe au wasikusamehe (ila all in all sio mwanzo mzuri wa kuanza hii safari ngumu ya ndoa)
 
badili dini ww uoe unachelewa wenzio wakimuwahi utakuja kulala mika tena au
 
matatizo ya akiana Ponda zanaanza taratibu kama maumivu ya kichwa maana inawezekana wazazi wanachukia wao kuitwa MAKAFIRI na wanaangalia mbelle ya safari yenu itakuaje ktk kuwasaidia kama wazazi wakishirikiana na wazazi wenu

tafakari sana kabla ya kufanya maamuzi magumu kama anayosema EL kwa mwaka huu
 
Oneni sasa jinsi upuuzi ufanywao na waislam wengine unavyowaaribia Goodwill.Kuna haja ya kukemea ujinga ufanywao na wenzenu ili muwe na good publicity.
MMESHAKUWA JANGA LA TAIFA SASA NA DUNIA KWA UJUMLA.
 
Seepa Mbona Nasi Tunao Madem Wazuri Tena Wanaojiheshimu Kuzidi Huyo Wa Wazazi Mambwiga?
Sepa Kamanda Langu!
 
Can you do without her?
Can you change dini?
Can you do without the consent of ur inlaws?

Majibu ya haya maswali yatakusaidia kufanya decision l think.
akibadili dini, je anaweza kuishi na tension kwa nduguze mwenyewe?
Seriously, kama unajijua kwenu ni watu wa kujali sana kuhusu dini why dont you date within your religion? Aaagh!
 
Back
Top Bottom