Nimekata tamaa ya maisha nahitaji msaada

Nimekata tamaa ya maisha nahitaji msaada

Mwenzako changamoto yake sio kuchafuka kwa tope wala kushindwa kusimamia au kuingia shambani, mtaji au pesa ya kuendeshea shughuli za shamba ndio tatizo.

Sasa wewe unaelezea usimamizi wa vibarua na mambo ya boot wapi na wapi? Lakini hongera kwa kuwa na shamba.
Changamoto yake siyo kukosa mtaji, changamoto yake nikutaka kuanza na kikubwa ilhali mtaji alionao ni mdogo, hapo utajikuta unapoteza hata kidogo ulokuwa nacho.
 
Changamoto yake siyo kukosa mtaji, changamoto yake nikutaka kuanza nakikubwa ilhali mtaji alionao ni mdogo, hapo utajikuta unapoteza hata kidogo ulokuwa nacho.
Hapana ni mtaji mkuu, yaani nimeyumba, wala sio sehemu ya kuanzia labda ukunielewa
 
Hapana ni mtaji mkuu, yaani nimeyumba, wala sio sehemu ya kuanzia labda ukunielewa
Mkuu kama nimekuelewa umesema shambani ulienda na laki 7, nampaka sasa umepanda eka 5 bado tena kadhaa, ni sahihi? Kama ulikuwanayo laki7 wakati unakwenda shamba inamaana huo ndiyo ulikuwa mtaji wako wa shambani (700,000), ulitakiwa upange mipango yako ya shambani kwa mtaji ulionao, siyo kwa matarajio mengine. Kazi ya shamba ina tatizo moja, unatakiwa uwe umeset aside cash kwa ajili ya kazi husika, pesa ya kazi yote iwepo.

Sijajua unalima nini, lakink sisi tunakolimia mfano mahindi kila eka moja unatakiwa kuweka pembeni laki tano, kwa maana hiyo laki7 inatosha eka moja tu. Ungeanza na hiyo moja ungefaulu, japo mwingine huenda akaona kama mchezo, lakini ukiwa makini msimu unaofuata unaweza kudouble uzalishaji. Kidogokidogo unapanda huku unajifunza. Ndiyo nlivowaza ndugu yangu.
 
Pole kwa yanayokusibu! Maelezo uliyotoa yanakinzana na CV yako. Ujasiriamali umeyumba, ushawishi kwa wateja/ madalali pia hukuumudu, ila kwenye karatasi umeweka.
Ikitokea unapata mtaji, usipoteze muda wako kwenda kulima, kama hutanunua mazao, basi nunua vitu mjini wapelekee vijijini hasa baada ya kuuza mazao yao wanapokuwa na pesa.
 
Shukrani kaka, muda mwingine tunafanya vitu kwa msukumo wa tamaa ya kufanikiwa haraka au kwa kuwa tumedondoka tunalazimika kujaribu kunyanyuka na kukimbia, hakika hili ni somo kubwa sana kwangu, tuombe Mungu tuendelee kuwasiliana tusaidiane mawazo mbele ya safari, shukrani kaka mkubwa
 
Pole kwa yanayokusibu! Maelezo uliyotoa yanakinzana na CV yako. Ujasiriamali umeyumba, ushawishi kwa wateja/ madalali pia hukuumudu, ila kwenye karatasi umeweka.
Ikitokea unapata mtaji, usipoteze muda wako kwenda kulima, kama hutanunua mazao, basi nunua vitu mjini wapelekee vijijini hasa baada ya kuuza mazao yao wanapokuwa na pesa.
Asante kwa ushauri kaka
 
Back
Top Bottom