Nimekata tamaa ya maisha nahitaji msaada

Mtu physical nilipata mmoja tu ila mambo yake anadai hayako vizuri, hii ndio option pekee niliyobaki nayo sasa nikikosa ndio basi sijui nitakuwa na hali gani, bado namuomba Mungu
 
Usimpumbaze awe kama wewe, Wewe una Gari yeye ana njaa gawa hiyo gari yako usiwe na pesa ya kula tuone kama utendelea kuwa kama wewe.

Sio kila nyakati Ego itumike ukiendekeza Ego utakufa unajiona.
Kama unatengeneza connections na watu alafu unawapigia simu hawapokei, SMS hawajibu na ukituma message whatsapp ile bluetick inakaa siku saba, utasema huyo mtu anataka kujenga connection na wewe?

Yamenikuta sana hayo ndio maana nimemshauri asilazimishe connections na watu. Atafute pesa lakini asidhalilishe utu wake.
 
Ukiona hvo ujue hao unaowaita connection hauwafai. Connection inatakiwa iwe both ways, iwafae both parties, tofauti na hapo utakuwa unataka msaada tu, na dunia ya sasa watu wanasaidia maskini wale wasiojiweza kabisa.

Sent from my BLA-L29 using JamiiForums mobile app
 
Naomba hizo njia za kutafuta pesa nikaweza kulipa bills zangu na mimi, kumbuka sina mtaji
 
Kuna mmoja alikuwa hapokei simu zangu nilipomaliza chuo mwaka 2009 alikuwa anafanya kazi kampuni ya mawasiliano, ila mwaka 2018 nikiwa ninafanya kazi Dodoma akawa ananitafuta kunipa CV ya mtoto wa kaka yake. Na mimi niliichukua ile CV nikaiweka kabatini kwangu mpaka leo sijampa connection yoyote ile.
 
Hahhaaaa, ndiyo maana ya connection.

Sent from my BLA-L29 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…