Kuna dhambi ukizitenda hata ukizitubu na kusamehewa ni lazima ziendelee kukutafuna tu. Japo Mfalme Daudi alisamehewa ile dhambi ya kuzini na hatimaye kumuoa Bethsheba baada ya kumuua mumewe, familia yake haikuwa na amani kuanzia wakati huo (incest, kuuana, uzinzi...). Na matatizo yaliendelea hata kwa mwanawe Sulemani (baharia mpaka akavunja rekodi ya wake na michepuko).
Inavyoonekana mkeo alikusamehe lakini aliumia sana na bado yumo katika maumivu na hakuamini tena. Na anavyokuona pengine mwendo wako haujabadilika sana na bado unawasiliana na huyo mwanamke wa nje; na au una michepuko mingine. Wanawake ni wavumilivu sana lakini pia nao ni binadamu na wanaumia sana hasa kama alikuwa anakupenda na kukuamini kabisa kabisa.
Japo hapo juu unapewa ushauri wa kuwa mbabe na mabaharia ningekuwa wewe ningeenda naye waifu pole pole hasa kama bado nampenda. Ningemwonyesha kwa vitendo kuwa bado nampenda na kwamba kosa lililofanyika sitalifanya tena; na kweli lilikuwa kosa. Huu ndiyo muda wa kuwa naye karibu sana na kumwonyesha mapenzi ya kweli. Spend a lot of time with her. Mtoe nje huko hata kama ni kwenda kula mihogo. Jenga imani yake polepole ili akuamini tena. Na kila unapopata nafasi mkiwa faragha mkumbushe kuwa bado unampenda na mhakikishie kuwa hutaki mwanamke mwingine na mtakuwa pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha. Kama bado anakupenda utaona ameanza kubadilika. Msongo wa mawazo alionao kutokana na majeraha ya usaliti utaanza kupungua. Hata ngozi yake usoni itaanza kung'ara na ataanza kutabasamu tena. Hata hasira alizonazo zitapungua. Wanasema time is the best healer na muda si muda majeraha yake yatapona na amani itaanza kurudi nyumbani mwako. Lakini mruhusu apone taratibu na usilazimishe mambo. Hata kama ikitokea majeraha aliyonayo hayaponyeki basi mpe uhuru wa kufanya anachotaka hata kama ni talaka. Ila kama kweli alikuwa anakupenda, akiona juhudi zako za kweli kabisa (siyo maigizo), ataanza kukuelewa tu.
Hata wewe yawezekana tukio hilo limekuathiri pia kisaikolojia japo hujui. Unajilaumu. Una hasira. Unajuta sana nafsini. Basi jisamehe (kama kweli umeamua kuacha hiyo tabia). Kama ni mkristo sali sana. Tubu dhambi hiyo kwa dhati kabisa na amini kuwa Mungu Ameshakusamehe halafu uanze upya. No regrets please. Hapo ndipo hata wewe utaanza kuiona nuru na maisha mapya katika mahusiano yenu hayo.
Wakumbuke hao watoto wenu. Ni muhimu sana muwalee pamoja. Say no to divorce mkuu hasa kama bado unampenda waifu wako. Please fight for your family. Blessings

