Nimekata tamaa na CHADEMA!

Nimekata tamaa na CHADEMA!

Marire , mimi nakufahamu vyema juu ya mrengo wako wa kisiasa humu jukwaani.Lakini unaona wenzako wanavyoanza kukutukana na kukukejeli! hivyo ndivyo hata wale waliojaribu kushauri walitukanwa na kukejeliwa, wengine wakakata tamaa wakaacha na wengine wanavumilia wanaendelea. Nakushauri ili usipate shock sana, wekeza zaidi katika kujadili mijadala ya jumla ya kitaifa zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wala sikushangai kwa wewe kukata tamaa, SIASA za TZ ni kama kamari vile............kila unayemsogelea ni mjanja kwa staili yake, hata wale unaodhani labda uwawaamini pia ukichunguza sana unagundua kuwa walikuwa ukoo mmoja na wenzao ila waliparanganyika tu kutokana na sababu kadha wa kadha......pole sana.
 
Mkuu Marire ni wewe? mkuu usipanic! come down! jipe muda wa kujipumzisha kama wiki moja hivi akili itulie na utajikuta ukipata nguvu tena! usipanic! ushauri wako bado ni muhimu kwa jamii wote tukiamua kukata tamaa, mwisho wake ni nini? mkuu Marire nakusihi sana usikukimbie tafadhali!

Muache kamanda apumzike kutumika,usishangae kesho Mwita Maranya,Mikael P Aweda wakafuata.Mzito Kabwela akitoka kitandani kwa heka heka za ........... alizozipata Kalenga nae ataungananao.Ni hatari vijana wanajitoa kuandamana,kupambana na polisi,kuteka watu,kukesha mitandaoni,kufungwa na kulawitiwa halafu viongozi wanaponda raha na kujitengenezea mazingira ya kuendelea kuwatumilia kisiasa.
 
mbowe, slaa, lema na mtei wanaiua chadema,,.anguko la chadema halizuiliki.
 
Aya nenda lumumba ukachukue buku saba yako!

yaani wewe ingekuwa ni mtihani ungepata division_0
umeelewa nilichoandika lakini?
hawa ma GT wa hili jukwaa wameenda wapi? uwiii
kuna watu wapo CCM na chadema ila hawajui kwanini wapo huko...
 
Ajashindwa zt wala ajashindwa mbowe na slaa alieshindwa cdm ? Ndugu
 
Marire , mimi nakufahamu vyema juu ya mrengo wako wa kisiasa humu jukwaani.Lakini unaona wenzako wanavyoanza kukutukana na kukukejeli! hivyo ndivyo hata wale waliojaribu kushauri walitukanwa na kukejeliwa, wengine wakakata tamaa wakaacha na wengine wanavumilia wanaendelea. Nakushauri ili usipate shock sana, wekeza zaidi katika kujadili mijadala ya jumla ya kitaifa zaidi.

mkuu wangu asante sana,ila kwa sasa kwa kusema ule ukweli wa moyoni nimehamia jukwaa la picha,ujasiriamali na hoja mchanganyiko,miaka mitano imeisha tuliowapa majimbo hatuna tunachoweza kijisifia kwao hasa kwenye kampeni zijazo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Marire umeona wenzako mliokuwa mnashirikiana kututukana Leo wamekugeuka na kukuita buku Saba?
 
Last edited by a moderator:
Heshima kwenu wakuu.
kwa nitakaowaudhi waniwie radhi.
_Mimi ni mwanachama wa chadema na nina kadi hai kabisa ninafurahiswa na viongozi wa chadema wakiwemo wabunge na madiwani majukwaani tu na si kwenye maendeleo...
kwa muktadha huo hata hili jukwaa la siasa nilikuwa mchagiaji mzuri sana kwa kuitetea chadema ndio sasa nikaamua leo niwaage rasimi hapa kwa kuwa ccm siwapendi na chadema siipendi ila nitabaki na kadi yangu hadi hapo watakapokuja viongozi watakaoleta maendeleo.
kama alivyokwishatuahidi. Dr.W.Slaa wakati anamnadi diwani wa kirumba Danny kaungu kuwa atahakikisha kata na majimbo yanayoongozwa na chadema yatakuwa mfano wa kuigwa kauli nayoifananisha na ya maisha bora.
_leo nawaaga rasim wakuu wa jukwaa hili la siasa !
__NB jimbo la Nassari na Mnyika tu ndio walau utasema kuna uongozi wa mbunge!
Khaa!! Mnyika huyu aliyewatapeli wanaubungo? Tunamuomba mungu amuweke hai hadi 2015 imkute :A S embarassed:
 
Khaa!! Mnyika huyu aliyewatapeli wanaubungo? Tunamuomba mungu amuweke hai hadi 2015 imkute :A S embarassed:

Lema kiwanja cha hospitali amebadilidha matumizi na kuwa binafsi ya familia yake,trekta nalo ameuza.
 
Mkuu Marire umeona wenzako mliokuwa mnashirikiana kututukana Leo wamekugeuka na kukuita buku Saba?

hahaha,mkuu Yote maisha ila wewe kwa comments za unasitahili matusi kwa kweli!
 
Last edited by a moderator:
mkuu wangu asante sana,ila kwa sasa kwa kusema ule ukweli wa moyoni nimehamia jukwaa la picha,ujasiriamali na hoja mchanganyiko,miaka mitano imeisha tuliowapa majimbo hatuna tunachoweza kijisifia kwao hasa kwenye kampeni zijazo

Mkuu, sasa na sisi tulioingia siku za karibuni tufanye nini ? yaani ni confusion! na ndio maana tunajaribu tu kutoa vijiushauri vya hapa na pale ila majibu tunayoyapata! dah!

Mfano kuna siku niliandika;

[h=2]Ushindani wa Kisiasa Tanzania na Siasa Tunayoitaka! (Sehemu ya II- 'AJIRA')[/h]
Wadau,

Katika sehemu ya kwanza na mada hii ya "Ushindani wa Kisiasa Tanzania na Siasa Tunayoitaka" Nilizungumzia kwa uchache suala la gesi.Sasa leo nizungumzie kidogo katika suala la ajira.

Ni wazi kwamba kwa sasa licha ya kuwa na tatizo kubwa la ajira nchini, kuna jitihada za hapa na pale ambazo zimefanywa kupunguza tatizo hilo japo tatizo bado ni kubwa.Jitihada hizo zinaweza kuwa bora au kuwa dhaifu.Katika hali ya kawaida tu, inategemewa ushindani wa kisiasa utupelekee katika kupata njia bora zaidi katika eneo hili na kama ushindani huo ukitupeleka kinyume chake, sidhani kama utakuwa na maana yeyote.

Katika serikali inayoongozwa na CCM, Tanzania kuna viwanda vidogo vidogo (Light Industries) kadhaa na hili ni jambo la wazi tu kwa sababu vinaonekana na vinatoa ajira japo kwa uchache sana.Sasa tunategemea katika ushindani wa kisiasa, tuone wanasiasa wanaopingana na jitihada mipango au mbinu zilizopo kwa sasa kwa kusema sisi tunaweza kutengeneza mazingira kwa watu binafsi/au sisi tukipewa serikali kama serikali tutajenga viwanda vizito (Heavy Industries) kama vya magari na Ndege,n.k au wataongeza kasi ya kuendeleza viwanda vidogo vidogo kama vya juice ambavyo hata sasa vipo.Hata hivyo ni lazima waoneshe dalili na nia yao kwa matendo maana kwa kusema tu, haiwezi kusaidia kitu.Kwa mfano, kama chama kitaahidi kujenga viwanda vizito ili kuwapatia watanzania ajira ,wakati huo huo kinashindwa hata kujenga ofisi yake,wala hakioneshi jitihada ya kufanya hivyo, hakiwezi kuaminika.

Kwa sasa kuna wanasiasa wamebuni mbinu mbali mbali za kuwapatia watanzania ajira.Mbinu nyingine zimebuniwa katika level ya kitaifa, na nyingine katika level za majimbo.Kwa mfano, Mtemvu wa temeke, yeye ameona kuwatafutia watanzania kazi huko uarabuni ndio njia ya kuwanusuru!, kuna wengine huko dodoma wameona kuwasaidia watanzania waweze kufuga nyuki katika maeneo yao ndio njia ya kuwanusuru, wengine wameona kuwasaidi watanzania waweze kufuga kuku ndio njia ya kuwanusuru, wengine wanadhani boda boda ndio mpango!.Ni suala la mawazo tu, mawazo haya yanaweza kuwa imara au dhaifu na ndio maana kukawa na ushindani wa siasa ili tuweze kupata mawazo bora zaidi.

Hivyo basi, katika hali ya kawaida, haitarajiwi kusikia wanasiasa wanaodhani wao ni mbadala wakilalamika na kulaumu tu bali kuja na mbinu mbadala bora zaidi na zinazotekelezeka, na nilazima wawe washaanza kuzifanyia rehearsal mbinu hizo katika majimbo wanayoshikilia.Kwa mfano, Haina maana ya CHADEMA kwa mfano,kumlaumu Mtemvu tu kwamba anawapeleka watanzania uarabuni, wakati wabunge wa CHADEMA hawajaonesha mbinu zao za kuwapatia vijana ajira katika maeneo yao ili tuweze kulinganisha. Inafaa katika majimbo ambayo yanashikiliwa na upinzani yawe mashamba darasa ili hata ahadi zikitolewa katika level ya taifa iwe ni rahisi kueleweka kwa kuangalia katika level ya majimbo.Mfano, Lema Anatakiwa kuweka wazi kwamba anawasaidia je vijana wa Arusha kwa sasa kupata ajira,Msigwa, Halima Mdee, na kadhalika wafanye hivyo hivyo ili tuweze kulinganisha na hawa wa CCM, wanaoleta mawazo mara ya kufuga, nyuki, kuku, au kuwatafutia watu kazi huko uarabuni.n.k kwa kufanya hivyo watanzania wataweza kulinganisha na kujua nani ni nani na kwa mwendo huo tutakuwa tunafanya siasa zenye manufaa.

Hizi ndizo siasa za ushindani wanazozitaka watanzania!
Lakini reaction yake ilikuwa ni very negative, na mifano mingine mingi ila kwa kuwa mimi naamini nchi hii hujengwa na wananchi na wananchi ni mimi na wewe ndio maana nakushauri usikate tamaa sana.endelea kufikiria alternative inayoweza kusaidia kusukuma maendeleo yanchi mbele.
 
Marire
Pole na misukosuko ya maisha, Uchaguzi wa Kalenga umeacha makovu mengi.
Huna haja ya kuichukia siasa, maana siasa ndio maisha. Jiunge na wapambanaji CCM, ili tuendeleze harakati za kuwapigania wanyonge na kudumisha Amani, Umoja na Mshikamano. Hawa CHADEMA ni wahuni tu.

na ccm ni mijizi tu,hakuna cha kumtetea mnyonge kwa ccm wanaangalia matumbo yao,waalimu na madaktari wanaandamana karibu kila mwaka halafu unakuja na hoja za ukasuku huku jf
 
Last edited by a moderator:
Kila mtu mwenye akili timamu anayeogopa dhambi lazima aichukie chadema.
 
Back
Top Bottom