Nimekata tamaa na CHADEMA!

Nimekata tamaa na CHADEMA!

Joined
Jun 30, 2013
Posts
21
Reaction score
14
Mbinu pekee tuliyobaki nayo sasa hivi ni kurusha Chopa na kusingizia daftari la wapiga kura.Hatuna mbinu mpya! Imefika mahala sioni jipya mbele yangu,mimi na wanangu sasa tumepoteza matumaini juu ya Chama chetu.Ushindi sasa kwetu mwiko!

Inakera sana!
 
Subira subira unakuta mwana si wako
 
Vijana wengi wa kitanzania walio ahidiwa ahadi kemu kemu na chama cha kiraghai cha upinzani (CDM) Wamekata tamaa.

Hii ni baada ya vichapo mfurulizo kukiandama chama hicho. Na chama hicho kutumia gharama kubwa za uchaguzi huku wapiga kura wakila ugali na kachumbali.

Vilevile imeelezwa na vijana wa kuaminika kutoka chama hicho kuwa waliahidiwa madonge manono kiasi cha vijana hao kutumia nguvu nyingi ikiwamo kuhatarisha maisha yao na watu wemgine.

vijana hao wamekuwa kama wamenyeshewa mvua ya mawe kiasi cha kupotea kwenye mitandao ya kijamii hususani JF. Machachari yao na tambo zao zote kuishia kwenye keyboard za kopyuta huku masanduku ya kura yakitoa somo.

Ombi langu kwa vijana hao warudi kundini (CCM) kusema kweli hatuta watupa.
KARIBUNI SANA CCM TUJENGE NCHI ACHANANENI NA SIASA ZA KIRAGHAI.
 
Kweli CDM ni kiboko..hamuwezi lala bila yenyewe..hapa tuu chama tawala hakilali, mkiwa wpainzani itakuweje?
 
Kweli CDM ni kiboko..hamuwezi lala bila yenyewe..hapa tuu chama tawala hakilali, mkiwa wpainzani itakuweje?

.....Mkuu wanajifariji kukinga mafuriko kwa kutumia magodoro....magamba ni magamba tu !!!
 
Chadema kina miaka 22 sasa toka kianzishwe ni aibu kupata kura 2 kwenye kituo, hawa vijana wa Chadema ndio watakaoiuwa Chadema.
 
Kweli CDM ni kiboko..hamuwezi lala bila yenyewe..hapa tuu chama tawala hakilali, mkiwa wpainzani itakuweje?

Naona meku umeamka saa hivi na mwendo wa viroba... upo kiroba cha ngapi saivi
 
Ni kweli vijana wa tanzania wanataka mabadoliko..ila cdm inayachelewesha hasa kwa kutoshinikiza kuhusu taratibu za uchaguzi kuboreshwa vijana wengi wamejiandikisha uanachama cdm lkn hawajajiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi...na tunasema kila siku hata katiba ingebaki hiyo alafu..cdm wasimamie taratibu za uchaguzi ziboreshwe cdm wangeshinda...sijui kwa nn viongozi hawaoni hii weakness...obama na democratic walishonda kwa kuweza kushawishi vijana kwenda kupiga kura baada ya kuhamasisha... Kura kura kura ndo msingi wa chama cha siasa as chama cha siasa lengo kuu ni kishika madaraka...huwezi kushika madaraka bila kua na wapiga kura...
 
Wanajidanganya na chopa,wat wanakuja kuanglia kahelkopta 2
 
Sasa nikihamia ccm itabidi nibadilishe jina na kumkana baba yangu mkulima ili nipate fursa?nijiite EDMUND J KIKWETE AU EDMUND NGOYAI AU EDMUND CHE NKAPA?
 
Jamani mimi nauliza tu, hivi zile ahadi za mheshimiwa 'ametelekeza' na 'ametekeleza' ngapi???Zile alizojinadi nazo mwaka 2010??
 
Vijana wengi wa kitanzania walio ahidiwa ahadi kemu kemu na chama cha kiraghai cha upinzani (CDM) Wamekata tamaa.

Hii ni baada ya vichapo mfurulizo kukiandama chama hicho. Na chama hicho kutumia gharama kubwa za uchaguzi huku wapiga kura wakila ugali na kachumbali.

Vilevile imeelezwa na vijana wa kuaminika kutoka chama hicho kuwa waliahidiwa madonge manono kiasi cha vijana hao kutumia nguvu nyingi ikiwamo kuhatarisha maisha yao na watu wemgine.

vijana hao wamekuwa kama wamenyeshewa mvua ya mawe kiasi cha kupotea kwenye mitandao ya kijamii hususani JF. Machachari yao na tambo zao zote kuishia kwenye keyboard za kopyuta huku masanduku ya kura yakitoa somo.

Ombi langu kwa vijana hao warudi kundini (CCM) kusema kweli hatuta watupa.
KARIBUNI SANA CCM TUJENGE NCHI ACHANANENI NA SIASA ZA KIRAGHAI.

Upuuzi mwengine huu. Chadema ni chama cha upinzani tu; serikali ndiyo iliyoahdidi maisha bora kwa kila mtu na kubadilisha miji kama kigoma kuwa Dubai au Singapore. Iwapo serikali imeshindwa kuleta maisha bora kwa kila mtu iweje lawama hizo zielekezwe chadema?
 
duuu yaliyopita yamepita. aliyechezewa faulo kaumizwa. ngoja tuelekeze nguvu zetu chalinze.
 
Back
Top Bottom