lup
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 2,514
- 2,732
Leo asubuhi nimetokea mabatini ninapoishi na kuja igogo..nilipokaribia maeneo ya uwanja wa mchafukoga nikaona gari na watu wengi wapo hapo uwanjani...nikahisi ni ile ishu ya MACHINGA.
Nikaamua kusogea ili nijiridhishe.kumbe kweli vitu vingi vya machinga vinatupwa hapo chini ya ulinzi wa Polisi na mgambo.kwa hiyo nikaona ngoja kwanza nichukuwe picha ndipo nije hapa niandike nikiwa na ushahidi wa picha.
Nilipochukuwa picha ya tatu ghafla askari akaniona na kunikimbiza...nikaona isiwe shida bora anikamate kwani naweza itwa mwizi.
Aliponikamata mgambo wakaja na kunipiga mikanda huku simu wamechukuwa.. Baadaye nikapandishwa kwenye gari na kupigwa mikanda...kama sikosei jina la polisi liliandikwa.Alexidilia ila sina uhakika kama nimelipatia.
Baada ya gari kuanza kuondoka nikaanza kuwambembeleza sana waniachie. Askari akaniomba rushwa ya sh.50000. Nikawaambia Nina shi.8000.wakadharau sana na safari ya kuelekea Polisi ikaanza huku nikielezwa kuwa mimi ni chadema na nimetumwa.. Dreva akaniambia hiyo kazi wao wametumwa na Maghufuli kwa hiyo watanionesha kazi
Kufanya story fupi nilipofika Pepsi wakawa wameniachia ila tayari mikanda nimekula.