Nimekamatwa na kupigwa na mgambo baada ya kuwapiga picha wakifukuza machinga

ProBook

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
552
250
Leo asubuhi nimetokea mabatini ninapoishi na kuja igogo..nilipokaribia maeneo ya uwanja wa mchafukoga nikaona gari na watu wengi wapo hapo uwanjani...nikahisi ni ile ishu ya MACHINGA.

Nikaamua kusogea ili nijiridhishe.kumbe kweli vitu vingi vya machinga vinatupwa hapo chini ya ulinzi wa Polisi na mgambo.kwa hiyo nikaona ngoja kwanza nichukuwe picha ndipo nije hapa niandike nikiwa na ushahidi wa picha.
Nilipochukuwa picha ya tatu ghafla askari akaniona na kunikimbiza...nikaona isiwe shida bora anikamate kwani naweza itwa mwizi.

Aliponikamata mgambo wakaja na kunipiga mikanda huku simu wamechukuwa.. Baadaye nikapandishwa kwenye gari na kupigwa mikanda...kama sikosei jina la polisi liliandikwa.Alexidilia ila sina uhakika kama nimelipatia.

Baada ya gari kuanza kuondoka nikaanza kuwambembeleza sana waniachie. Askari akaniomba rushwa ya sh.50000. Nikawaambia Nina shi.8000.wakadharau sana na safari ya kuelekea Polisi ikaanza huku nikielezwa kuwa mimi ni chadema na nimetumwa.. Dreva akaniambia hiyo kazi wao wametumwa na Maghufuli kwa hiyo watanionesha kazi

Kufanya story fupi nilipofika Pepsi wakawa wameniachia ila tayari mikanda nimekula.
Ndio ujifunze..siku ingine ufwate yanayokuhusu..
 
  • Thanks
Reactions: lup

Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,302
2,000
Yaah..!! Kipigo kilikuwa ni haki kwako....hujui kuwa kumpiga (kuchukua) picha mtu bila ridhaa ni KOSA...!? Usichukulie poa....
 

ngalelefijo

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
3,046
2,000
neve
Acheni kumsingizia Rais kwa vitu vinavyofanywa chini.
Acheni kutunga habari ili mradi tu iwe na bad image kwa Rais basi ndiyo furaha yako.

Hapo Mwanza kuna Serikali kamili na taratibu zake ktk kutekeleza majukumu yake.

Mwacheni Rais afanye mambo ya msingi ya nchi.

Naona sasa kila maana JF akijisikia tu kumsema Rais bila sababu yoyote Anafanya na hata credibility ya JF inazidi kufa kila siku

Mwisho JF utakuwa mtandao wa wambaye tu maana hakuna Facts
never jf kufa never
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom