Nimejiandikisha kupiga kura sasa nauza kadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimejiandikisha kupiga kura sasa nauza kadi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Companero, Mar 27, 2010.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hatimaye leo nimejiandikisha kupiga kura. Sasa nauza kadi yangu. Kama unaihitaji unapaswa kuwa na sifa hizi:

  1. Uwe mgombea wa Urais, Ubunge au Udiwani
  2. Uwe huombi, hupokei wala hupokelewi rushwa
  3. Uwe tayari kuleta mapinduzi ya kiujamaa 2010

  Aluta Continua!The Struggle continues! Mapambano yanaendelea!
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  sidhani kama utapata mteja kwa vigezo vyako hivyo
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo nitumie vigezo gani ili nipate wateja?
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kama uko serious basi nakudelete kati ya wanajamii niliowaconsider kuwa na busara. Unauza kadi ya kupigia kura? Na usipopiga huu ujinga tulio nao madarakani tutaumalizaje!
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  unataka nimpigie kura nani na nani ili huo "ujinga ulio madarakani" tuumalize?
   
 6. senator

  senator JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Basi hukuwa na ulazima wakujiandikisha kama unauza kadi!!!
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Bado tuko mwanzo wa thread na tumeshaona wavivu wa kufikiria. Mtu amesema anauza kadi as terminology na ametoa vigezo. lakini majuha wanathink literary dammit.

  Mkuu Kompanyero. kwa hivyo vigezo vyako hakuna mteja utakayempata. Na sana sana wameshakusoma na wataenda china kutengeneza kadi mbadala kama ya kwako na utashangaa umewapa kura bila hata ya kuwapigia
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,657
  Likes Received: 1,485
  Trophy Points: 280
  wakulu nawshauri mumsome comredi Companero kati kati ya mstari, tukijifikirisha kidogo, tutaelewa ana maana gani hapa,

  komredi, at first kigezo cha kwanza utawapata wengi, kigezo cha pili wote watakimbia kama wakitaka kuwa honest,which means kigezo cha tatu cha mapinduzi kitakuwa kimekufa kabisa

  hivi, huamini kuwa Azimio la Arusha...dira yetu ya Ujamaa, lilizaliwa Arusha na kuzikwa Zanzibar...nimesikia kaburi lake limefunikwa kwa zege, sasa kulifufua hapo ipo kazi kweli...labda tukamwombe comredi Hugo copy hata kama siye ndo tulimpatia!
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,657
  Likes Received: 1,485
  Trophy Points: 280
  mkulu Msanii yani kumbe tulikuwa tunafikiria sawa kabisa....inauma sana we dont take even 2 minutes to think .....
   
 10. senator

  senator JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Sidhani kama kuna hitajika mwalimu wa fasihi kuelezea alichoandika labda Compa nafanana na Masiha mana ndo wachache waliokuwa wanasema vitu kwa mifano then wanapatika wahubiri kutafsiri kilichoandikwa -...Statement ipo clear kuwa
  Cha kwanza hapo ni huyo bwana kajiandikisha kupiga kura
  then akaamua kuuza kadi(mana hapo ni biashara anaifanya na nikwa makusudio ndo mana amejiandikisha akitegemea kwa njaa zake italipa kama ilivyo kawaida ya walahoi wengi)
  Mwisho anatoa sifa za mnunuzi..hivi muomba/mpokea/mtoa rushwa wanatambulika machoni pa watu??
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nikiwa kwenye foleni leo nilifanya kautafiti (survey) kujua kwa nini watu wanachukua kadi. Japo kautafiti haka hakakuwa na sampuli ya uwakilishi (representative sample) nilipata matokeo haya ya awali (preliminary results):

  1. Watu wengi wamechukua kadi iwe utambulisho kwa sababu hawana paspoti wala kitambulisho
  2. Hivyo ni wenye kadi wachache sana watapiga kura na inawezekana wengi kama mimi wataiuza

  Je, kuna hitaji la kuu-synovate/redet utafiti huu?
   
 12. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mkuu ukipata mteja ni-PM, nami yangu naitafutia soko.
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Niuzie mimi, nataka kugombea ubunge. Siombi, sipokei wala sipokelewi rushwa. Ila ukiniuzia kadi nitakukatia kifuta jasho. Na nipo tayari kuleta mapinduzi makubwa. Nafikiri nikifika bungeni tu nitashawishi bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa kuwa ameshindwa kutatua matatizo yetu mengi. Tafadhari niPM.
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Du, u-nafikiri!
   
Loading...