Nimeipenda Tamthilia ya Kombolela iko vizuri

Mario Kempes

Member
Jun 29, 2021
63
120
Kupitia AzamTv kuna tamthilia inaitwa kombolela, iko vizuri sana, mimi sio mpenzi wa tamthilia za Bongo, ila hii ni kali.

Inaakisi maisha halisi ya uswahilini, maisha halisi ya Mtanzania wa hali ya chini(Mnyonge).

Maisha ya Familia zetu za kiswahili, Baba na Mama wanaishi pamoja na Watoto wao pamoja na wajukuu wao nyumba moja! Yaani zile familia unakuta wadada wamezalishwa wakiwa nyumbani halafu wajukuu wanalelewa na babu na bibi.

Huku upande wa pili kuna kaka mkubwa wa familia, haeleweki maisha yake na yeye yupo nyumbani tu kula anamtegemea baba. Familia ambayo ukichelewa wakati wa msosi ndio nitolee.

Ukipata muda icheki iko poa sana, inafundisho kubwa sana, ina gwiji mzee nkwabi

1713F41D-CB30-401D-85DC-F91123A6D72A.jpeg
 
Kati ya vitu vimenipitia kushoto ni hizi tamthiliya zetu za Kiswahili, nadhani nimeathirika na ubovu wa kazi za hapo kati walizokuwa wakiziita Bongo movie...

Kuna wakati nilipenda sana production ya mini-series moja nadhani jinale ni Siri ya Mtungi ndani yake alikuwepo yule marehemu Sharo nini sijui, ilikuwa na videography moja nzuri...
 
Kupitia AzamTv kuna tamthilia inaitwa kombolela, iko vizuri sana, mimi sio mpenzi wa tamthilia za Bongo, ila hii ni kali.

Inaakisi maisha halisi ya uswahilini, maisha halisi ya Mtanzania wa hali ya chini(Mnyonge).

Maisha ya Familia zetu za kiswahili, Baba na Mama wanaishi pamoja na Watoto wao pamoja na wajukuu wao nyumba moja! Yaani zile familia unakuta wadada wamezalishwa wakiwa nyumbani halafu wajukuu wanalelewa na babu na bibi.

Huku upande wa pili kuna kaka mkubwa wa familia, haeleweki maisha yake na yeye yupo nyumbani tu kula anamtegemea baba. Familia ambayo ukichelewa wakati wa msosi ndio nitolee.

Ukipata muda icheki iko poa sana, inafundisho kubwa sana, ina gwiji mzee nkwabi

View attachment 2084230
Iko poa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom