Nimeingia choo cha kike ... Part 6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeingia choo cha kike ... Part 6

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Mar 26, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Inaendelea toka sehemu ya 5 ...


  “Naitwa Angel, Naweza kuongea na HorsePower?” Iliuliza sauti toka upande wa pili. “Mimi ndiye!” Nilijibu kifupi. “Jamaniii, Unaumwa?” “Kwanini?” “Si sauti ya HP yule ninayemfahamu!” “Mi mzima, labda malaria ndo nahisi inaninyemelea!” Niliropoka kwa sauti ya chini, kupotezea. “Pole, sana. Sauti yako ni kweli haiko sawasawa, lakini usijali, nafikiri nawajibika kukurudishia furaha kama hutajali ….” Sikutegemea na wala kupendelea kauli hii kwa wakati huu. Nilitupa jicho langu liligongana na la rafiki yangu Katunzi na nikajikuta nakosa cha kumjibu Angel. “Asante kwa concern yako, ila …..” Kabla sijamalizia Angel alinikatiza kwa swali “Naweza kukuona ofcn kwako sasa?” Kwa kipindi chote hiki cha majibishano, akili yangu kwa kweli haikuwa sawa na hata majibu niliyotoa sikujua yalikuwa yanatoka wapi maana sikupendelea Katunzi aelewa uhusiano nilioanzisha na binti huyu, na wala kujua kuwa ninaongea naye kwa simu muda huo. Nguvu yangu kubwa niliitumia kufupisha mazungumzo kujinasua na mgandamizo wa mawazo ulionikumba ghafla. Kitendo cha Angel kuulizia kama anaweza kuja ocfn ndicho kilinistua zaidi na kunitoa ktk dimbwi la mawazo na kunikuta nikiropoka kwa sauti nzito “Ohhh No, nipe dk chache nakuja ofcn kwako” na kurudisha receiver mahali pake bila hata kuagana!. Muda wote huo Katunzi alikuwa amekaa kimya akinitazama usoni. Ni wazi aligundua kuwa kuna dada amezama moyoni mwangu na kuharibu utaratibu wote wa akili na ubongo wangu kwenye kufikiri na kupanga mambo. Alionekana dhahiri anatamani kuninasua ktk hali niliyokuwa nayo.

  “Vipi ndo huyo nini?” “Hapana, ni hawa madereva wetu Bwn, saa nyingine wanaongea sana mpaka wanakera” Nilijibu kwa kujihami. “Mhhh, sina uhakika na jibu lako!” Alijibu Katunzi. Wakati naongea na Katunzi sauti ya Angel iliendelea kusumbua akili yangu na nilibaini wazi kuwa nisingeweza kupata unafuu wowote pasipo kwenda kumuona hapo ofcn kwake. “Chief, nashukuru kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi. Naomba nikuache mara moja nionane na Executive Director, nina appointment naye muda huu, nikitoka nitakuja ofcn kwako!” Nilimwambia Katunzi. Hakujibu lolote, alinyanyuka na kufungua mlango na kutoka kwa hasira. Nilijua wazi amehisi nimemdharau, lakini sikuwa na njia mbadala ya kusolve matatizo ya moyo wangu kwa kipindi hiko.

  Nilifungua mlango taratibu sana kama mgonjwa anavyoingia kwa daktari na kuingia ofcn kwa Angel. Kwa mbali nilimuona Angel akiwa amesimama dirishani akiangalia bustani na mandhari nzuri za Majengo yaliyojengwa kwenye nyumba nzuri za Masaki. Ni wazi alikuwa na mawazo sana! Ghafla, mawazo yangu yalibadilika, baada ya macho yangu kutua juu ya umbile lake dada huyu aliyekuwa akiangalia dirishani bila kutambua uwepo wangu. Macho yangu yalijipitisha tena kwenye umbo la dada huyu kwa kasi. Miguu yake ya bia, rangi yake ya asili yenye mng’ao usio wa cream, kiuno chembamba na mduara wa wastani uliotulia vzr kiunoni kwa nyuma, ulinifanya niamini kuwa huyu ni malaika na si binadamu wa kawaida! Nikiwa kwenye tafakari, nilishangazwa kwa mwenendo wa tabia njema alionao na kuishi muda mrefu kwa maisha ya kifahari bila boy friend au mume. Hili lilinipa utata mkubwa!

  “HorsePower, nimefurahi kukuona, na pole kwa kukuita asbh hii” “Haina shida” Nilijibu. Moyo wangu ulienda mbio na niligundua kuwa I was deeply in love with her. Nilishangazwa pia na hali ya kusita iliyokuwa imeshikilia fahamu zangu. “Nilifikiria tukutane nje ya ofc lakini nimeona hapa ofcn patatufaa zaidi. ” Alizungumza huku akinivutia kiti na kunikaribisha kwa adabu. Wakati wote huu, sikuweza kusikia lolote maana macho yangu yalikuwa bize na ziara zisizo rasmi kwenye mwili wa dada huyu. “Asante” Nilijikuta nimejibu bila hata kukumbuka niliambiwa nini.

  “HorseP, wewe ni miongoni mwa watu ninaowaamini mno hapa ofcn.” Alianza “Nilitamani sana kupata nafasi ya kukuzoea pengine hata kuongea na wewe kama tulivyokutana leo lakini nikashindwa …” Nilistuka baada ya kuona mzungumzo sasa yanageuka. Yale niliyotarajia mimi kuongea ndiyo yeye ameanza kuyazungumza. Hofu iliniingia. Nikahisi huyu dada ana jambo kubwa. “Yeah inawezeka kila mtu alikuwa anaitafuta hii nafasi, nasijui kwa nini wote hatukuipata mpaka imetokea leo hiii …” Nilimjibu bila kujiamini. Alitabasamu kidogo, moyo ukastuka tena na kuendelea “Sidhani kama ingepita mwezi huu bila kukutafuta, naamini wewe unaweza kuwa msaada kwangu!” “Yeah, kabisa inawezekana”. “Unatatizo gani, mbona unanitisha?” “Maisha!” Alijibu. “Maisha? Kivipi?” “Yamekuwa magumu na machungu kwangu!” Nyumba nzuri, magari kadhaa, mshahara mzuri-Niliwaza, maisha yamekuwaje magumu tena kwa huyu dada?. Nikapigwa na butwaa. “Kabla sijakwambia, HP,naomba nihakikishie jambo ….” “Kuna nini tena Mungu wangu!” moyo ulijiuliza. “Uliza tu mamaa, niko kwa ajili yako”. Nilijikakakamua. “Unanipenda? I mean kwa moyo wako wote?” Nilibaki kinywa wazi, na ni dhahiri nilijua kuwa nimeingia mtegoni. Nilifumba macho, nikavuta pumzi,na kutaka kuongea jambo ……


  ********** Mniwie radhi, huyu dada (Angel) kaniita tena, ofcn kwake, nikitoka nawamalizia hiki kisa, mwenzenu nimeingia matatani *********
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ahhh ndefu jaman...
   
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  looh, nawasifu kwa kuandika magazeti.
   
 4. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ww mbona kila mara dharura haziishi kamanda wangu? unatupotezea utam
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Dharura ni sehemu ya maisha, kila kilichopo dunia kipo kwa dharura mkuu ....
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umenena mkuu!
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Na hapo bado hatujasomea uandishi wa habari!!!
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mimi nipo kimya tu nafuatilia hii maneno mpaka nijue mwisho wake....................
  Sijui uliingia choo cha shimo au cha kuflash..........................LOL
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Yaani huu muda uliotumia kuwajibu hawa ungerusha mistari hata miwili huku tukikusubiri urejee..

  Probably cha kuflash, lol
   
 10. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mmmh!
  Ndefu !
  Nini ubaya wa ndefu ?
  Au wewe unapenda fupifupi? Jamani !
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Judgement.... Mkweo nipo kukusoma hapa.....
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  HP Tuna omba uwe unaziunganisha.... Waweza paste zote zilizofuata kwenye ile namba moja ili kufuatilia vizuri zaidi na kuweza eleweka....
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Iko mwishoni, zimebaki season mbili tu ....
  Poleni kwa usumbufu.
   
Loading...