Nimeingia choo cha kike ...........! (4) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeingia choo cha kike ...........! (4)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Mar 2, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Niliendelea kusikia maneno na mawazo yakikizunguka kichwa changu. Moyo wangu na akili zangu zilikuwa katika vita vikali, moyo ukipenda na kutamani wakati sheria ya akili yangu ikijawa na tahadhari ,huruma na uzalendo juu ya uhusiano ninaotaka kuulazimisha. Wakati wote huo, Angel alikuwa mbele yangu, kajiinamia akijaribu kucheza cheza na simu yake ya mkononi. Ni dhahiri pia alikuwa ametawaliwa na aina fulani ya hofu kuhusiana na jibu alilonipa. "Asante angel kwa jibu ulilonipa …" Nilizungumza kwa utulivu "ni wadada wachache sana wenye uwezo wa kuzungumza ukweli kulinda mahusiano yao na wenzi wao, na wewe umekuwa mmoja wao ….. Nimefurahi kwa uaminifu wako …." Niliongeza. Ni kweli HP, ni kweli kabisa, sasa mi naomba nikuache tutaonana jtatu kazini" alizungumza haraka haraka huku akiinuka na kuanza kuondoka. Sikutaka kumkatiza, nilimsindikiza, akaingia kwenye gari, akaniaga na kuondoka.

  Kwa dakika 20 zaidi nilisalia Brajec Pub nikitafakari mchakato mzima ulivyokuwa. Maswali mengi yalinizunguka na kujikuta nikijijibu mwenyewe na kunifanya nijichanganye zaidi. Niliamua kulipia vinywaji, nikaingia kwenye gari yangu tayari kuelekea kwangu.

  "Karibu Mkoa wa Pwani" kilikuwa ni kibao pembeni ya barabara ya kuelekea bagamoyo kilichonifanya nigunduwe kuwa nilikuwa nimepitiliza nyumbani kwangu. Ktk hali ya kawaida ilipaswa nipige breki maeneo ya boko CCM na kukunja kuelekea kwenye nyumba yangu. Nilijilaumu sana kwa kutokuwa mwangalifu wa kufikia hatua hata ya kupitiliza kwangu. Niligeuza na kurudi nyumbani kwa mwendo wa taratibu sana. Wazo lililonijiwa haraka haraka ilikuwa na kufuta hali hiyo iliyojijenga kwa siku mbili tu kichwani kwangu kwa kasi ya ajabu mno. Niliamua kujiliwaza kwa kuingia jamii forums na kupitia mada mbali mbali ambazo zimepostiwa na JF members mbali mbali. Nilipitia mada na comments za Mtambuzi, Bishanga, Masikini_jeuri, Judgment, The Boss, AshaDii, Smile,Obsesd, Badili Tabia, PakaJimmy, SweetyLady, Husninyo, Kongosho, Mwanakijiji, FirstLady1 na wengineo wengi. Kwa ujumla JF ilinifariji sana ktk hali niliyokuwa nayo. Lakini, haikusaidia kuniondoa ktk dimbwi la mawazo. Nilitafuta "Boring books" na kuanza kusoma ambazo zilinifanya nipitiwe na usingizi kwa haraka.

  Jmosi nilishinda kwa rafiki zangu kadhaa tukibadilishana mawazo juu ya biashara mbali mbali tunazofanya nje ya kazi na kuangalia ligi za mpira wa miguu za nchi za nje, na kunipa ubize, uliofanya siku iishe mapema. Jpili jioni nilikuwa na laptop yangu nikiandaa report na kazi za kupambana nazo jtatu kazini. Nilisikia mlio wa sms nikaamua kuchukua simu na kuchungulia inbox "Mambo HP, kimya?" "Poa, tight na maandalizi ya kazi za kesho" Nilimjibu na kuendelea na kazi yangu. "Nakusumbua ?" Aliuliza. Kwa kipindi kile nilikuwa nimedhamiria kukaa mbali na huyu binti. Nilijua wazi si vyema sana kumng'ang'ania mtu asiye wako. "Busy!" Nilimjibu. "Huwezi kuchat hata kwa dk moja?" Aliuliza. "Busy!" Nilijibu. "Umewahi kuwa na huruma?" aliuliza. Nilishtuka kwa hili swali na nilihisi kengele ikigonga kichwani pangu. "Huruma, una maanisha nini?" "Muenekano wako ulivyo na matendo yako kama tofauti vile …" Alijibu. Nilielewa wazi ni wapi anaelekea ni nilifahamu wazi hatari inayoanza kunikabili. "Hapana, nipo kama nilivyo" Nilijibu. "Unashindwa nini kupoteza five minutes or less kuongea na mimi? Mtu unayempenda?" Aliuliza. "Sipenda kujibizana na wake za watu usiku, si vyema na ni hatari kwa mahusiano yako". Nilimjibu. "Wewe unajua niko wapi na niko na nani?" "Sidhani kama kuna umuhimu wa mimi kujua hayo, huo si wajibu wangu; yupo anyepaswa kufanya hivyo!" Nilijibu "Nilijuwa wewe ni katili sana, yaani hauhitaji kujua niko wapi? Je kama nadhurika?" Aliuliza "Mimi si katili, ila napenda kuheshimu mahusiano ya watu na isitoshe aliye ktk hali ya kudhurika hana muda wa kuandika meseji." "una maanisha napretend?" aliuliza. "Naomba muda Angel, kuna kazi namalizia" Nilimjibu "Mbona leo umekuwa tofauti na juzi? Majibu yako kama siyaelewi hivi"? aliuliza. "Busy" Nilijibu. Ghafla nilisikia simu ilikianza kuita. Sikuweza kujua nini hasa kimenfanya anipigie simu. Nilishusha pumzi na kuinyanyua simu yangu ….

  ****** Naingia kwenye kikao nikitoka nitawapa mwendelezo wa yaliyonikuta ….******
   
 2. BAOSITA

  BAOSITA JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakusubiri mkuu...
   
 3. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,202
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  mhhhhhhhhhhhhhh umetuacha T junction
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Vuta subra, nikitoka kwenye kikao namalizia uzi ...
   
 5. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Aaaah ndo nini sasa ? Achana na kikao , jf ni ya muhimu kuliko kazi za ofisini eti.
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Weweeee, acha mambo yako, kwani JF wananilipa mshahara?
   
 7. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wee kweli mwandishi au ndo shigongo mwenyewe
   
 8. Mhilu

  Mhilu Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  duuuh umetuacha njiani kama ni movie ingefanya mtu aende dukani mbio kutafuta season five
   
 9. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Naona ana undugu na shigongo!
   
 10. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  JF ni zaidi ya mshahara .
   
 11. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hahaaa, meseji yako ina ukweli kiasi, JF inakupa burudani na ushauri wa maana sana. Idumu JF!
   
 12. kikwakwa

  kikwakwa Senior Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HP kwenye miutamu tena unakatiza,bt upo juu.
   
 13. YNNAH

  YNNAH JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mh!! Yani najiweka vizuri niendelee kusoma,nakutana na ***. Kwani kikao kinaisha saa ngapi?
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hizi story mwakani unaweza zikuta kwa Shigongo
   
 15. G

  GALIMA JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kikao hakijaisha tu??
   
 16. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mbona tena mapicha picha hp ?
   
 17. i

  interlacs Senior Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  kwani, ukiingia choo cha kike hutopiga kubwa au ndogo? shida lako sinikujisaidia tu. piga kubwa popote akija mtu we guna tu au piga makofi tu.
   
 18. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  HP usikawie bwana sema na wewe utakuta unakuja kutuwekea season 3 kesho kutwa...
   
 19. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Oyaaaa, malizia bhana..
   
 20. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kikao hakiishi? eh
   
Loading...