Nimeibiwa simu, je hawa Wetrack wanaweza kunisaidia?

IsaacMG

Member
Dec 6, 2019
76
91
Habari waungwana nimeibiwa simu kampuni ya Google pixel 8 pro, ila kuna kampuni huwa naona matangazo yao ikijinasibu kuwa wanatrack simu zilizoibiwa na ofisi yao iko Ilala boma wanajiita wetrack. Nimewasiliana nao wananiambia kuwa niwape asilimia 10 ya gharama ya simu.

Shida sio gharama, je kuna yeyote ambaye amewahi kupata simu yake kupitia Hawa jamaa au na wao ni kama polisi wetu wa njoo kesho rudi kesho kutwa.

Naombeni ushuhuda kabla sijapata maumivu kwa mara ya pili.

Asanteni
 
Habari waungwana nimeibiwa simu kampuni ya Google pixel 8 pro, ila kuna kampuni huwa naona matangazo yao ikijinasibu kuwa wanatrack simu zilizoibiwa na ofisi yao iko ilala boma wanajiita wetrack, nimewasiliana nao wananiambia kuwa niwape asilimia 10 ya gharama ya simu, shida sio gharama je kuna yeyote ambaye amewahi kupata simu yake kupitia Hawa jamaa au na wao ni kama polisi wetu wa njoo kesho rudi kesho kutwa.
Naombeni ushuhuda kabla sijapata maumivu kwa mara
Pia kama utaenda unatakiwa uwe na imei ya simu yako
 
Habari waungwana nimeibiwa simu kampuni ya Google pixel 8 pro, ila kuna kampuni huwa naona matangazo yao ikijinasibu kuwa wanatrack simu zilizoibiwa na ofisi yao iko ilala boma wanajiita wetrack, nimewasiliana nao wananiambia kuwa niwape asilimia 10 ya gharama ya simu, shida sio gharama je kuna yeyote ambaye amewahi kupata simu yake kupitia Hawa jamaa au na wao ni kama polisi wetu wa njoo kesho rudi kesho kutwa.
Naombeni ushuhuda kabla sijapata maumivu kwa mara ya pili.
Asanteni
Wana track hawana longolongo
 
Hakuna njia yoyote ya kutrack simu kwa kutumia imei namba ikiwa simu imezimwa na location imezimwa.
Imei namba si kitu ni namba tu kama namba ya Nida hivi yaani ni utambulisho wa simu kwenye kampuni iliyoizalisha na wala haijaunganishwa na mifumo yoyote ya satellite.

Ndio maana unaanza kwa kuwalipa hela kwanza lakini ukienda wata track na watakupa location ya simu yako kabla haijazimwa yaani mara ya mwisho kuwa online. Na hapo kazi yao itakuwa imeisha na hela yako itakuwa imeliwa.

Watu wanapoteza simu kila siku ila suala la kuipata hio huwa ni story tu za vijiweni. Kama bado unataka kuwapa hela yako basi wape baada ya kazi ama back up taarifa zako za muhimu baada ya kuongezea hiyo hela ununue simu nyingine maisha yaendelee.
 
M
Hakuna njia yoyote ya kutrack simu kwa kutumia imei namba ikiwa simu imezimwa na location imezimwa.
Imei namba si kitu ni namba tu kama namba ya Nida hivi yaani ni utambulisho wa simu kwenye kampuni iliyoizalisha na wala haijaunganishwa na mifumo yoyote ya satellite.
Ndio maana unaanza kwa kuwalipa hela kwanza lakini ukienda wata track na watakupa location ya simu yako kabla haijazimwa yaani mara ya mwisho kuwa online. Na hapo kazi yao itakuwa imeisha na hela yako itakuwa imeliwa.
Watu wanapoteza simu kila siku ila suala la kuipata hio huwa ni story tu za vijiweni.
Kama bado unataka kuwapa hela yako basi wape baada ta kazi ama back up taarifa zako za muhimu baada ya kuongezea hio hela ununue simu nyingine maisha yaendelee
aifunge tu hiyo simu hatoipata?
 
Ni wachache sana siku hizi atumie simu ya wizi/kuikota n.k bila kubadilisha imei..

Hiyo kwakweli ni kubeti, tangu nilipoibiwaga simu miaka hiyo na kuvuruga mishe zangu zote, Mpaka leo sina huruma na mwizi, naona maumivu yako, tofauti tuu na simu vitu vyako.

Ifike mahali kampuni za simu zije na technolojia ya kueleweka ya security ya simu kama simu, sio kutudanganya na viji privacy vinavyozibuliwa na mawinga Kariakoo, wabongo wengi security tunayotaka ni ya hii mijizi, kuhusu sijui security ya ma faili ni wachache, wengi ni wazee wa pilau, msg za madeni na michepuko...

Yaani inatakiwa mtu anaiba simu anaambulia kioo tuu kama spear, motherboard inakuwa locked full.

Pole sana.
 
Back
Top Bottom