Nimeibiwa simu aina ya iPhone, naomba kusaidiwa namna ya kuipata

Dodo86

Member
Oct 23, 2018
91
64
Nimeibiwa simu yangu kwenye begi aina ya iPhone 7 tangia juzi na kila nikiipiga haipatikani na nimejaribu kwenda polisi naona siwalewi.. Nimeweka iCloud yangu kwenye simu ya Dada yangu kutumia Find My IPhone Naona inaonesha iko offline.

Kwa wenye uzoefu wa hizi simu ni njia gani nitumie nyingine kupata simu yangu? Nimeibiwa Morogoro.. Naomba msaada wenu wana Jamii wenzangu.
 
Pole mkuu, msaada hapo ni polisi kuitafuta kwa kutumia IMEI, ila kumbuka ni mpaka iwekwe laini ili network provider aweze kuona details.
ingawa iphones hazibadilishiki imei ila siku hizi wengi wakiiba wanauza kama spea, inatolewa kioo mashine inatupwa.

kama una una uwezo kidogo nunua simu nyingine maana unaweza ukapoteza gharama ya simu kutafuta simu maana hawa ndugu zetu hawana huruma.

pole sana.
 
Polisi watakwambia gharama kubwa kuliko amankulingana na bei ya simu mwishowe wakwambie mara ipo mwanza ongeza pesa ya mafuta utajuta.

Kama uchumi unaruhusu nunua nyinginr tu ila kama unataka kuifatilia andaa mpunga wakutosha maana polisinjaa watakula pesa yako hadi basi.
 
Kanunue simu nyingine tu mkuu pole sana, siku hizi hata ikiwa na icloud kuna wazee wa kufanya bypass
 
Pole mkuu, msaada hapo ni polisi kuitafuta kwa kutumia IMEI, ila kumbuka ni mpaka iwekwe laini ili network provider aweze kuona details.
ingawa iphones hazibadilishiki imei ila siku hizi wengi wakiiba wanauza kama spea, inatolewa kioo mashine inatupwa.

kama una una uwezo kidogo nunua simu nyingine maana unaweza ukapoteza gharama ya simu kutafuta simu maana hawa ndugu zetu hawana huruma.

pole sana.
Si lazima lakini aiwashe ili ahakiki kana ni nzima maana sidhani utautoa kioo bila kuiwasha au?
 
Nimeibiwa simu yangu kwenye begi aina ya iPhone 7 tangia juzi na kila nikiipiga haipatikani na nimejaribu kwenda polisi naona siwalewi.. Nimeweka iCloud yangu kwenye simu ya Dada yangu kutumia Find My IPhone Naona inaonesha iko offline.

Kwa wenye uzoefu wa hizi simu ni njia gani nitumie nyingine kupata simu yangu? Nimeibiwa Morogoro.. Naomba msaada wenu wana Jamii wenzangu.

Huna namna akiizima; mpaka awashe; akiiwasha Police wanaweza kukusaidia!

Ni Rahisi Sana kwao maana inaonyesha iPhone Fulani inatumika Na namba Fulani
 
find my iphone itafanya kazi kama simu ikiwa connected na internet na location ipo on.
 
Back
Top Bottom