Nimeibiwa sim usiku huu Namba za IMEI tenco w3lite naipataje?

Nimeibiwa sim usiku huu Namba za IMEI tenco w3lite naipataje?

kuipata kupitia tcra utaipata ila hizo ulizoziandika sio namba za IMEI
 
Hio sahau tu mkuu, we kafunge line yako tu mapema, kuna mchezo hao vibaka wanatuma sms kwa contacts zako zote wakitaka ndugu na jamaa watume kiasi fulani cha fedha kwenda namba ingine wakijinasibu ni wewe una dharura.
Nashukuru mkuu
 
Mkuu ndo nauliza jinsi ya kuzipata maana siku save ndo maana nimetoa model ya simu Kuna wataalam wanajua jinsi ya kuzipata humu

Brother, kila simu ina imei namba zake.
Hakuna namna ambavyo mtu anaweza kukisia IMEI namba za simu.
Kutaja aina ya simu na model yake bado hakuna msaada kabisa, maana hizo namba ni tofauti kwa kila simu.
Ni rahisi kukisia rangi ya chupi zilizovaliwa na wadada kituo cha basi kuliko hizo IMEI namba .
Baadhi ya wauzaji huandika hizo namba kwa risiti.
Note : Jambo la msingi ni kufungia line zako na kuwajulisha ndugu Jamaa na marafiki maswahibu yaliokukuta.

Pole sana.
Next time andika pembeni IMEI yako.
 
IMEI number unaweza ipata kupitia mtandao unaotumia, kama una mtu unamjua ongea nae atakusaidia au la nenda polisi karipoti watakusaidia kupata IMEI number sema ujiandae kutoa hela japo ni huduma ya bure ila huwa wanapenda sana hela
 
Hio sahau tu mkuu, we kafunge line yako tu mapema, kuna mchezo hao vibaka wanatuma sms kwa contacts zako zote wakitaka ndugu na jamaa watume kiasi fulani cha fedha kwenda namba ingine wakijinasibu ni wewe una dharura.
Mkuu hii imenikuta na mimi
 
Back
Top Bottom