Mkuu Pole sana kwa tukio hulo.Na mumshukuru saana mungu kwamba mpo wazima.
Hembu tuambie Weekend yako uliianza vipi na kuimalizia jana kwa style ipi?
Maana kuna Mshkaji wangu yeye alilala nyumba yoote milango wazi,cha ajabu gari aliiacha Bar na yeye akakodi Taxi.
Cha kushangaza kuamka asubuhi akaanza kuitafuta gari na kusema imeibiwa,akaenda vituo vyoote vya Polisi kusema kwamba Gari yake Imeibiwa na nyumba imefunguliwa kwa Master Key.
Sasa alitokea jamaa mmoja mwenzie akamuambia mkuu haujavunjiwa nyumba wala haijafunguliwa,utakuwa ulilala milango wazo,jamaa alimtukana balaa,na kumuambia oyaaa mie ninaakili zangi timamu,siwezi kulala mlango wazi.
Basi jamaa akawa mstaarabu,na kumuambia unajua kwamba gari yajo uliicha Bar?na uzuri Bar yenyewe kwa mlio Zanzibar ni Gymkhana Bar ambapo ulinzi upo mzuri sana.Ikabidi jamaa aliganda akavuta kumbukumbu kwa aibu akasepa wiki nzima mtaani hayupo.
Sasa nakuuliza kujua je weekend yako iliishaje mkuu na mlikuwa nanani siku hiyo