Nimeibiwa ATRIUMS hotel Sinza.

Mkuu pole sana,mimi nilshaibiwa hotelini dar na haki ya mungu siku hizi najiadhari kinoma,yaani niliibiwa nilipoenda kuoga asubuhi,na milango ilikuwa imefungwa kama kawaida ina maana ni wafanyakazi wa hoteli hiyo

Wewe hukulala self ulilala zile za choo nje hatua 20 hapo lazima wakombe wanakulia timing tu
 
Pole,shigongo ni nomaa,street university hyo,elimu ya kitaa,wanacheza na nafasi hao,wajasiliamali hao!! Hapo ni Guest ya mademu wa kona bar!!
 
one sided story

siku ukiibiwa wewe hapo ATRIUMS ndio utajuwa story ya upande wa pili, kwa sasa itakuwa ngumu kwako kuamini kuwa haya yamenitokea kama navyoeleza hapa, ilikuwa usiku wa march 04 2012, saa 3 usiku.
 
duh pole,hivi hotelini sio kama guesthouse kuwa unatakiwa uache vitu reception kama unatoka??????kama ndio hivyo usiwalaumu....kama sivyo,then kata rufaa mkuu they should be made accountable for the loss.......

Usijaribu hata siku moja kuacha vitu reception siku ya kuondoka wanachora mpango na wezi wanakupora njiani. yaani sijui ufanyaje.
 


Pole sana. Nilishawahi patwa na msala pale. Jamaa yangu alikuwa anataka sehemu ya honey moon na akapendekeza Atriums. Nilienda kufanya booking na kulipa. Ajabu niliweka kikasha chenye kadi za benk, driving license na ID cads kwenye dashboard ya gari, na niliiona wakati naiacha. Nilipotoka sikuangalia, I just drove and go. Baada ya muda jamaa alipiga simu na kunambia kuna mtu kapeleka vitambulisho kaviokota. Nikambana jamaa anambie kaviokota wapi hakusema, ila kasema nipeleke shs 50,000 ili nirudishiwe vitu vyangu.
Nilirudi hotelini baada ya kubanana nao nikatoa sh 15,000. ajabu aliyeokota ni mfanyakazi wa pale. Ofcourse nilikuwa discouraged sana na hoteli ile. Inaonekana ndiyo kawaida yao maana hata mwangalizi hakuplay part yoyote kuwa huyu ni mteja arudishiwe.
 
Pole sana mkubwa.Nikupongeze kwa kuwa mungwana,coz kama ivi we are jst warned.Jipe mwoyo,kila jaribu lina lango la kutokea.Utapata vingne mku
 
duh! Shigongo nilidhani ni mtu mwema sana! Kumbe nae jambazi tu!! Naanza kuziamini tetesi zinazomhusisha na madawa ya kulevya!
 
Hii dunia...kuna watu kama tax bubu,mara plate namba za njano mara nyeupe! Shigongo huyu huyu aliyesoma Nsumba? Hizi pesa hizi..pole Mwita Mungu atakupa vingine!
 
Naona picha ya tanzania kuwa na makundi ya mafia yatakayokuwa yakisaidia watu kulipiza kisasi, makundi haya yatakuwa tajiri sana kama mafionso wa italoa na mafia mobs wa rashia.
 
watu tunapishana humu duniani,yani mimi niwe na vidolali vyangu 2300 au hata hela ya madafu eti niache chumbani?ni ngumu kueleweka!wiki moja kubwa kaka,au ulipata' mwenyeji' wa muda kakuliza!??
 
Nchi imejaa majizi kila kona ni aibu na inafedhehesha sana!! ukienda hotel unaibiwa,restaurant wanaongeza bei chakula, dukani hivo hivo,sokoni madalali yaani huu mfumo wa kuiba sasa ni fashion hata home napo unapigwa tu yaani shida shida shidaaa...na haya yote ni ccm imeyaleta na kuyalea,,,,
 
duh pole,hivi hotelini sio kama guesthouse kuwa unatakiwa uache vitu reception kama unatoka??????kama ndio hivyo usiwalaumu....kama sivyo,then kata rufaa mkuu they should be made accountable for the loss.......
Kama chumba ni changu na nimelipia kwanini nipeleke vitu vyangu reception? Nadhani kuna umuhimu kwa kutolala nyumba za aina hiyo zinazotaka upeleke vitu vya thamani reception maana mantiki yake ni kwamba hapo kuna wezi, lafau hata utakapoweka reception kama mali za thamani sana ukirudishiwa unaweza kufanyiziwa usiku na kuibiwa ama hata kuuwawa, la maana mie nadhani kabla ya kufanya malipo ya chumba ni kuuliza kama nyumba hiyo wanahitaji vitu kuwekwa reception, ukisikia hivyo ni kuondoka tu maana hilo ni genge la wezi.
 
Yule dingi mwenye Namnani hotel ndo nilimuona mtu mwenye utu, kuna siku niliibiwa pale hotelini kwake alichofanya ni kuniambia niende urafiki kufungua jalada then nirudi, niliporudi akanikabidhi hela yangu akaniambia atadeal na huyo kijana aloingia kufanya usafi wakati niko restaurant. ukweli nilimuona wa pekee na anayemjali mteja sio kama huyu shigongo mtunga hadithi
 
Hivi kila mtu akiibuka hotelini na kusema nimeibiwa dollar 50000,htc 5,blackberry 6,tsh 7M atalipwa?Hotel si zitafilisika? Kuna utaratibu weka katika safe kama hamna kabidhi reception,kama huwaamini reception then hio hotel sio hadhi yako usilale hapo. Je huyu mwenzetu alifanya hivyo? Its funny unaibiwa dollar 10,000(mfano) kwenye hotel ya 40dollar/night!why dont u spend 100d and be safe?
 
ATRIUMS HOTEL hamnaa kitu pale kwanza haina hadhi ya kuitwa HOTEL ile ni GUEST HOUSE tu kama zilivyo Guest nyingine za uchocholoni, hivyo usalama pale ni sifuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…