Nimeibiwa 245,000/= MPESA VODACOM

Itakua umejiibia kama isemavyo serikali ya hawamu ya 5 kuwa watu wanajiteka sasa na wewe hyo utakua umejiibia!
 
Mimi nimewahi kuibiwa shs. 4,450,000/= kutoka benki ya DTB . Na bado fedha yangu haikurejeshwa, japo mwanzo walinipa matumaini ya kurejeshewa.

Kipindi hicho huduma ya mobile ktk mabenki ilikuwa haijawa kama leo. Wiki mbili zote, jamaa alikuwa anatoa pesa kupitia ATM visa card fake, bila mimi kujua kupitia mabenki mengine.

Mambo haya ni changamoto.
 
Uliza swali sehemu ambayo hujaelewa maana naamini hayo maelezo yamekamilika. Wanalijua ndio maana siku zote tunasisitizwa kutunza namba zetu za siri, watakuwa labda wanalitafutia mwarobaini
Nilitaka jua hill kwamba MTU akiweka namba yako kwenye simu yake akadownload mpesa apple na akawa anajua namba yako ya siri anakupiga?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu simu ilijibonyeza menu, ikachagua toa pesa, ikajiingiza namba ya wakala na ya siri na ikathibitisha? Itakuwa simu ya maajabu
[emoji1787]
 
Aiseee!![emoji134][emoji134]
 
Huwa namba zinaingiliana.
kama uliwahi kabla wakala hajampa huyo mtu pesa...utazipata.ila kama ulichelewa...kuna mawili.
1 wakala kulipa
2 kupoteza.


Ni kwa mara ya kwanza kutokea? Endelea na mamba yako ila badili nenosiri.
Mambo ya kupigia huduma kwa wateja ndo yanafanya mtu ashindwe kupata hela yake sometimes.... Njia ni moja tu... kwenda kwenye ofisi zao.....
 
Kuna mtu anaejua namba yako ya siri aliweka line yako kwa simu yake akadownload Mpesa app
Hili nalo linawezekana.... but pia huyo mtu lazima aliijua namba ya siri ya jamaa... nje ya hapo asingeweza....
 
Yeah, anachukua line yako anaweka kwenye simu yake anadownload mpesa app then anaendelea kufanya transactions kwa kutumia app aliyodownload kwa kutumia line yako
Nilitaka jua hill kwamba MTU akiweka namba yako kwenye simu yake akadownload mpesa apple na akawa anajua namba yako ya siri anakupiga?
 
watu watakua wanalizwa sana kwa hii mpesa app, sio salama kama mtu mwingine anaweza kuitumia kutoa pesa kwa namba ya mtu. Waifanyie marekebisho kwa usalama wa fedha za watu
Usalama wa M-pesa ni namba yako ya siri bila hivyo utapigwa mpaka ukome
 
Duuh aisee
 
Mfano wangekua wanatuma sms ya conrfimation code kwenye namba yako ambayo ungeiweka ili kuconfirm muamala nafikiri hapa ingeweza kutatua tatizo
Matter ni namba ya siri mkuu.... hii app me naipenda sana sababu nakumbuka kuna kipindi nilikuwa natoa hela kwa wakala hata kama line yangu ipo mbali....

Kama mtu anashindwa kutunza namba yake ya siri there is no way anaweza kusaidika....
 
Mi ilishawahi kunikuta NBC kwa kuibiwa 2.1M hadi kuna uzi niliweka humu. Nilienda hadi BOT, pesa nilirudishiwa ila ilichukua takribani miezi 3.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…