Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Hapa jamvini na hata mitaani kuna watu wameonyesha kukerwa na hatua ya Kikwete kuandaa semina elekezi hivi karibuni pale Dodoma ilihali ni juzi tuu ametoka kutembelea kila wizara kwa masuala haya haya ya kiutendaji.
Binafsi sikuelewa ni kwanini wanakerwa sana na hicho kitendo. Mda mfupi uliopita nilikuwa maeneo maarufu kwa kuuza chakula kwa bei ambazo mtu wa kiwango changu anaweza kumudu, almaarufu kwa jina la Holiday out.
Nilikuwa nimewahi kidogo kupata msosi kabla mchuzi haujaongezwa maji, nilikuwa nimekaa napiga story na jamaa mmoja ambaye alijitambulisha kwamba ni muhasibu serikalini.
Pembeni yake kuna watu walikuwa wanajadili ishu za semina elekezi ya Dodoma, mimi nikawa nimeonyesha kutopenda watu wanavyo ponda, basi jamaa alianza kunifafanulia vizuri baadhi ya mambo kuhusiana na gharama za kuendesha semina kama ile.
Maneno yake yalikuwa kama ifuatavyo
Unajua ndugu yangu malalamiko mengi unayoyasikia mitaani usiwe unayapuuzia tuu yanakuwa yamewakwaza baadhi ya wataalamu humu humu ndani ya serikali na wakati mwingine wanakuwa wamemshauri kitaalamu muheshimiwa lakini kawapuuzia hivyo huishia kutekeleza maagizo japo wanafahamu fika kwamba jamaa anachemka.
Kwa mfano hebu fikiria wewe kama kiongozi wataalamu wanakushauri kwamba nchi ipo katika hali tete haiwezi kabisa kuongeza mishahara katika miaka ya hivi karibuni lakini unawapuuzia unaenda majukwaani na kutangaza kwamba utaongeza mishahara.
Hivi hii ni akili kweli? Kwa ufupi ndugu yangu semina elekezi ya Dodom ilikuwa na mambo yafuatayo hasa ukichukulia hali ya pesa kwa kila wizara ni hoi kwa sasa .
Msafara wa rais inakadiriwa walisafiri wafanyakazi zaidi ya 125 kwa ajiri ya kuandaa mazingira kwa zaidi ya siku 12 na kulipwa posho zote za msingi na ghalama za usafiri ambayo ni magari ya serikali na mabasi.
Walialikwa Mawaziri na manaibu waziri woote jumla wapo hamsini(50) na madereva wao hamsini wakisafiri hulipwa posho zote za msingi, bila kusahau Magari yao 50 ya kifahari yanasafiri kwenda Dodoma, mizunguko ya Dodoma kwa siku zote na yatarudi Dar na kufanyiwa service
Walialikwa Makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu woote jumla wanakaribia 45 na madereva wao 45 wakisafiri hulipwa posho zote za msingi, bila kusahau Magari yao zaidi ya 45 ya kifahari yanasafiri kwenda Dodoma, mizunguko ya dodoma kwa siku zote na yatarudi Dar na kufanyiwa service.
Viongozi wakuu wa ulinzi na usalama walialikwa pia waweza kuwa zaidi ya 20, hawa wanalipwa na serikali posho zao zoote na bila shaka walikuwa na magari yanayotumia mafuta na yenye atleast madereva 20 wanaolipwa posho zote zinazohusiana na kusafiri.
Inakadiriwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu walisafiri na wasaidizi wao kama vile personal secretaries(PS) ambao wanaweza kufanana na idadi ya hao viongozi, hawa pia wanastahili posho zao zote wanaposafiri kikazi.
Kuna ghalama za ukumbi na refreshments ndani ya ukumbi ambayo ghalama zake lazima ziendane na hadhi ya wahusika kama waweza nenda pale Ngurdoto katafute ghalama zilizotumika katika semina elekezi ya mwaka 2006 ndipo utajua serikali inatumia pesa kiasi gani kwa vitu kama hivi.
Usiombe ufanye kazi serikalini alafu uwe na roho ya uzarendo utapata taabu sana kisaikolojia. Hiyo yooote tisa sijakugusia kabisa pesa zitakazopotea kwa ajili ya mafuta ya magari yanayochukuliwa kwa ajiri ya msafara wa Rais hasa ukichukulia kiprotokali msafara wa rais unahitaji magari mazito zaidi ya kumi na hapa na-asume Rais na bodi gadi wake hawalipwi hata senti moja kwa siku husika na mbaya zaidi ni ..
Kabla hajamalizia nikajinywea mchuzi wangu na kujiondokea maana kisha niingiza hasara ya kupoteza siku yangu mapema kabisa.