Nimeharibu siku yangu!!!!!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Hapa jamvini na hata mitaani kuna watu wameonyesha kukerwa na hatua ya Kikwete kuandaa semina elekezi hivi karibuni pale Dodoma ilihali ni juzi tuu ametoka kutembelea kila wizara kwa masuala haya haya ya kiutendaji.

Binafsi sikuelewa ni kwanini wanakerwa sana na hicho kitendo. Mda mfupi uliopita nilikuwa maeneo maarufu kwa kuuza chakula kwa bei ambazo mtu wa kiwango changu anaweza kumudu, almaarufu kwa jina la “Holiday out”.

Nilikuwa nimewahi kidogo kupata msosi kabla mchuzi haujaongezwa maji, nilikuwa nimekaa napiga story na jamaa mmoja ambaye alijitambulisha kwamba ni muhasibu serikalini.

Pembeni yake kuna watu walikuwa wanajadili ishu za semina elekezi ya Dodoma, mimi nikawa nimeonyesha kutopenda watu wanavyo ponda, basi jamaa alianza kunifafanulia vizuri baadhi ya mambo kuhusiana na gharama za kuendesha semina kama ile.

Maneno yake yalikuwa kama ifuatavyo


“Unajua ndugu yangu malalamiko mengi unayoyasikia mitaani usiwe unayapuuzia tuu yanakuwa yamewakwaza baadhi ya wataalamu humu humu ndani ya serikali na wakati mwingine wanakuwa wamemshauri kitaalamu muheshimiwa lakini kawapuuzia hivyo huishia kutekeleza maagizo japo wanafahamu fika kwamba jamaa anachemka.

Kwa mfano hebu fikiria wewe kama kiongozi wataalamu wanakushauri kwamba nchi ipo katika hali tete haiwezi kabisa kuongeza mishahara katika miaka ya hivi karibuni lakini unawapuuzia unaenda majukwaani na kutangaza kwamba utaongeza mishahara.

Hivi hii ni akili kweli? Kwa ufupi ndugu yangu semina elekezi ya Dodom ilikuwa na mambo yafuatayo hasa ukichukulia hali ya pesa kwa kila wizara ni hoi kwa sasa….


Msafara wa rais inakadiriwa walisafiri wafanyakazi zaidi ya 125 kwa ajiri ya kuandaa mazingira kwa zaidi ya siku 12 na kulipwa posho zote za msingi na ghalama za usafiri ambayo ni magari ya serikali na mabasi.

Walialikwa Mawaziri na manaibu waziri woote jumla wapo hamsini(50) na madereva wao hamsini wakisafiri hulipwa posho zote za msingi, bila kusahau Magari yao 50 ya kifahari yanasafiri kwenda Dodoma, mizunguko ya Dodoma kwa siku zote na yatarudi Dar na kufanyiwa service

Walialikwa Makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu woote jumla wanakaribia 45 na madereva wao 45 wakisafiri hulipwa posho zote za msingi, bila kusahau Magari yao zaidi ya 45 ya kifahari yanasafiri kwenda Dodoma, mizunguko ya dodoma kwa siku zote na yatarudi Dar na kufanyiwa service.

Viongozi wakuu wa ulinzi na usalama walialikwa pia waweza kuwa zaidi ya 20, hawa wanalipwa na serikali posho zao zoote na bila shaka walikuwa na magari yanayotumia mafuta na yenye atleast madereva 20 wanaolipwa posho zote zinazohusiana na kusafiri.

Inakadiriwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu walisafiri na wasaidizi wao kama vile personal secretaries(PS) ambao wanaweza kufanana na idadi ya hao viongozi, hawa pia wanastahili posho zao zote wanaposafiri kikazi.

Kuna ghalama za ukumbi na refreshments ndani ya ukumbi ambayo ghalama zake lazima ziendane na hadhi ya wahusika kama waweza nenda pale Ngurdoto katafute ghalama zilizotumika katika semina elekezi ya mwaka 2006 ndipo utajua serikali inatumia pesa kiasi gani kwa vitu kama hivi.

Usiombe ufanye kazi serikalini alafu uwe na roho ya uzarendo utapata taabu sana kisaikolojia. Hiyo yooote tisa sijakugusia kabisa pesa zitakazopotea kwa ajili ya mafuta ya magari yanayochukuliwa kwa ajiri ya msafara wa Rais hasa ukichukulia kiprotokali msafara wa rais unahitaji magari mazito zaidi ya kumi na hapa na-asume Rais na bodi gadi wake hawalipwi hata senti moja kwa siku husika na mbaya zaidi ni………..”

Kabla hajamalizia nikajinywea mchuzi wangu na kujiondokea maana kisha niingiza hasara ya kupoteza siku yangu mapema kabisa.
 
Taratibu mtaamka wote na kuona mnavyoibiwa! Dr Slaa amejaribu kuwaamsha, mkadhani ni mchezo anafanya! Sasa endeleeni na huyu mjinga wenu miaka mingine mi-nne muone atawafikisha wapi...
 
Dah inahuzunisha sana...namie nishaharibu siku yangu kwa kusoma hii sredi...nahisi huyu Rais wetu hashauriki!!Mkapa nae alikuwa hashauriki lakini etlist alikuwa ma maono/fikra pevu lakini huyu gamba dah!!
Hili swala Dk Slaa aligusia kwenye mikutano yake(hapa nazidi kuthibisha kwamba Dk habahatishi na wala hakurupuki), yaani nchi iko tete na bado wanaponda mali..

Hivi inaingia akilini??maandalizi ya siku 12...semina ya dakika 45...mabilioni yote haya ni kodi hizi za wananchi au???

Ezan...asante kwa kuniharibia siku yangu,nina hasira :frusty::frusty::frusty:....napita tu hapa!!
 
Sasa hapa jf inabidi niwe naingia usiku maana sasa tafukuzwa kazi. Jana nimeshindwa kufanya kazi baada ya kusoma thread ya ufisadi wa madiwani Geita na K'ndoni. Leo tena!?
 
Tuna Kiongozi msanii na mjinga...hawezi kuthubutu! Agggggggggggggggggggggrrrr Garbage Presidaaaaaaaaaaa


attachment.php
 

Attachments

  • Mkwere.jpg
    Mkwere.jpg
    39.3 KB · Views: 378
Wakati wa kampeni kuna dada mmoja mmarekani alicomment kwa wall ya Kikwete ya Facebook akishauri watu wasimchague, Namnukuu alisema hivi, "I have talked with Jakaya Kikwete face to face when he came in Los Angels, he is a GARBAGE for the head of state."
I was angry and felt so bad for th way this Mzungu alivyomuita Rais wetu hivi, but as days goes nazidi kuona kuwa she was never wrong, but I was wrong to think that she was Wrong..!
12 days for the preparations of 1-2 hours meeting? Bad enough few days alizungukia wizara almost zote alishindwa nini kutoa hizo seminar elekezi huko? Hivi tukisema hawa viongozi wanafikiria kwa kutmia nyayo zao na sio ubongo watasema nimewatukana??
I don't wana believe we have such kind of presdent. The system has rotten, the presidency is stinking, Presdent mwenyewe ndo kashazoea harufu hiyo, Ee Mola tunusuru na hili janga.
Naomba Mungu hii iwe ndoto may be nitaamka na kukuta mambo hayako hivi..!:A S cry::A S cry::A S cry::A S cry:
Honestly sometimes nafikiria hata nisirudi Nchini kabisa, yaani niwe nakuja kusalimia tu.
 
Serikali yote imeoza kuanzia rais mpaka mawaziri wake. Hata miezi miwili haijapita toka awatembelee kwenye wizara zao inakuwaje leo tena kuwaita Dodoma jamani. Hivi huyu rais atatufanyua sisi ndondocha mpaka lini.

Huwezi amini hospitali ya taifa muhimbili inakosa dawa rahisi kama lasix halafu wao wanafuja pesa Dodoma, ni wengi wamepoteza maisha na wanazidi kupoteza maisha kwa kukosa matibabu rahisi kabisa. Naamini roho za hawa wanaowaua huku wao wakila raha Dodoma zitawahukumu.

Watu gani wasio na huruma hawa, hivi ni binadamu kweli, ewe JK kama nchi imekushinda si uache, kwani lazima uendelee kuwa rais wakati ubongo wako hauna uwezo huo?

Da jamani nami siku yangu imeharibika, hebu ngoja niji"sedate" nilale.
 
Ningemuona ana maarifa sana kama angetangaza, kuanzia sasa sote tuliopo hapa dodoma ofisi zetu zipo hapa hakuna tena ofisi dar!kwani makao makuu ya nchi ni dodoma!
 
Ezan

Kuna mambo serikalini ukiyajua unaweza usiamini....niliisha sema tuna raisi Mbu mbu!

Jamani hivi huyu jamaa kwenye kampeni alipokuwa anasema miaka mitano alikuwa anajifunza urais, tumpe miaka mitano mingine kufanya kazi mnafikiri alikuwa anamaanisha nini? Binafsi sikumchagua lakini kwasababu lilikuwa ndiyo chaguo la akina lewis makame na siruhusiwi kuhoji kisheria basi. Nimekwisha poteza vitu vingi sana katika maisha yangu ila ninaumia sana kupoteza hata haki ya kuongozwa na kiongozi niliyemchagua
 
me naamini sio kwamba watanzania bado idad kuubwa tumelala,
tunafaham ujinga mwingi tu uliopo ndani ya serikali lakini tataizo ni
nani amfunge paka kengele.

Tusubiri kidogo labda dr slaa amejitosa.
lakini pa1 na hayo jamnii anposema na si tumsapot basiii!
 
Nimeharibu siku yangu. Na kila atakayeingia humu ataharibu siku yake. Tanzania inawaka moto inateketea. Nina wasiwasi miaka minne ijayo nchi hii tutakuwa tunazungumzia nini. Uchumi wa nchi unazidi kudidimia. Kile kidogo kilichopo wakubwa wanakikomba. Bado sasa huo mgao wa umeme unaokuja. Kwanza nina mashaka kama hapa kwenye shirika lenyewe pako sawasawa kwa sababu siamini kwamba kwa watu na akili zao timamu (kama wanazo) wanaweza kuiweka nchi katika giza kwa siku zote hizo na masaa yote hayo eti kwa sababu ya kusafisha mitambo??!!! Bila kutafuta njia mbadala. Sikatai umuhimu wa kusafisha mitambo lakini kweli wameshindwa kutafuta njia mbadala wakati wanasafisha mitambo yao ili viwanda visifungwe???!!! Kubwa zima linatangaza kwenye luninga ujinga huo na linaona kama fahari vile. Naona hata huyo Masoud wake safari hii kajionea ujinga kutangaza pumba kila siku akamwambia bosi wake atangaze mwenyewe aonyeshe ujinga wake. Nina wasiwasi mafisadi wanawatumia hawa. Akili pumba pumba pumba pumba kabisa
 
Taratibu mtaamka wote na kuona mnavyoibiwa! Dr Slaa amejaribu kuwaamsha, mkadhani ni mchezo anafanya! Sasa endeleeni na huyu mjinga wenu miaka mingine mi-nne muone atawafikisha wapi...

Hebu tueleze mkuu mnaibiwaje vile?
 
jamani...........wakati mwingine waTZ tuache ubinafsi na kujifanya hatujali...namaanisha nini...haya yanayofanywa na serikali yenu (maana sikuichagua) yanaonekana wazi ila tunakasumba ya kumuona mtoa taarifa as if ana shida na dhiki...mimi nimefuatilia hotuba zote za kina slaa na wenzake,nina watu serikalini hasa wizara ya fedha wananipa data halisi..WAMECHOKAAAA....najiuliza jamani what is the WAY FOWARD..nani ajitoe mhanga?kwa nn tusihimize watu wakaingia BARABARANI jamaniiii......tuache ubinafsi kisa eti uana kikaz chako na laki zako 4 unajiona hufi tena ilhali una mafuta lita 2500,na umeme wik ijayo huna!!jamani JK angeonyesha japo anajali au ana uchungu na nchi hii tukajumuika pamoja kulia umaskini...ningemwelewa...watu tunafanya kazi mshahara wote unaishia matumizi ya kawaida...kila kitu kipo juu...ebu nambie..basi tena tuingie barabarani jamani:israel::israel::israel:
 
jamani...........wakati mwingine waTZ tuache ubinafsi na kujifanya hatujali...namaanisha nini...haya yanayofanywa na serikali yenu (maana sikuichagua) yanaonekana wazi ila tunakasumba ya kumuona mtoa taarifa as if ana shida na dhiki...mimi nimefuatilia hotuba zote za kina slaa na wenzake,nina watu serikalini hasa wizara ya fedha wananipa data halisi..WAMECHOKAAAA....najiuliza jamani what is the WAY FOWARD..nani ajitoe mhanga?kwa nn tusihimize watu wakaingia BARABARANI jamaniiii......tuache ubinafsi kisa eti uana kikaz chako na laki zako 4 unajiona hufi tena ilhali una mafuta lita 2500,na umeme wik ijayo huna!!jamani JK angeonyesha japo anajali au ana uchungu na nchi hii tukajumuika pamoja kulia umaskini...ningemwelewa...watu tunafanya kazi mshahara wote unaishia matumizi ya kawaida...kila kitu kipo juu...ebu nambie..basi tena tuingie barabarani jamani:israel::israel::israel:

Kuingia barabarani ili kuiangusha serikali halari sidhani kama kuna nchi itakuunga mkono kikubwa kama utawala huu hujaupenda tujipange kuushina katika uchaguzi ujao
 
Back
Top Bottom