Nimeharibu siku yangu!!!!!!!

Nimeharibu siku yangu!!!!!!!

Nchi hii sijui nisemeje???enyway maana sijui nianzie wapi mimi yangu macho namshukuru hicho nitakachopata ewala!
 
IMF nao ni wajinga? Wahisani nao ni wajinga? unatumia kuliko uchachopata, Je hapo unahitaji kusoma uchumi mpaka darasa la ngapi? je huo ni ujanja au ulimbukeni as if ndege na hotel za nyota tano umeziona ukubwani.
 
Hapa jamvini na hata mitaani kuna watu wameonyesha kukerwa na hatua ya Kikwete kuandaa semina elekezi hivi karibuni pale Dodoma ilihali ni juzi tuu ametoka kutembelea kila wizara kwa masuala haya haya ya kiutendaji.

Binafsi sikuelewa ni kwanini wanakerwa sana na hicho kitendo. Mda mfupi uliopita nilikuwa maeneo maarufu kwa kuuza chakula kwa bei ambazo mtu wa kiwango changu anaweza kumudu, almaarufu kwa jina la “Holiday out”.

Nilikuwa nimewahi kidogo kupata msosi kabla mchuzi haujaongezwa maji, nilikuwa nimekaa napiga story na jamaa mmoja ambaye alijitambulisha kwamba ni muhasibu serikalini.

Pembeni yake kuna watu walikuwa wanajadili ishu za semina elekezi ya Dodoma, mimi nikawa nimeonyesha kutopenda watu wanavyo ponda, basi jamaa alianza kunifafanulia vizuri baadhi ya mambo kuhusiana na gharama za kuendesha semina kama ile.

Maneno yake yalikuwa kama ifuatavyo


“Unajua ndugu yangu malalamiko mengi unayoyasikia mitaani usiwe unayapuuzia tuu yanakuwa yamewakwaza baadhi ya wataalamu humu humu ndani ya serikali na wakati mwingine wanakuwa wamemshauri kitaalamu muheshimiwa lakini kawapuuzia hivyo huishia kutekeleza maagizo japo wanafahamu fika kwamba jamaa anachemka.

Kwa mfano hebu fikiria wewe kama kiongozi wataalamu wanakushauri kwamba nchi ipo katika hali tete haiwezi kabisa kuongeza mishahara katika miaka ya hivi karibuni lakini unawapuuzia unaenda majukwaani na kutangaza kwamba utaongeza mishahara.

Hivi hii ni akili kweli? Kwa ufupi ndugu yangu semina elekezi ya Dodom ilikuwa na mambo yafuatayo hasa ukichukulia hali ya pesa kwa kila wizara ni hoi kwa sasa….


Msafara wa rais inakadiriwa walisafiri wafanyakazi zaidi ya 125 kwa ajiri ya kuandaa mazingira kwa zaidi ya siku 12 na kulipwa posho zote za msingi na ghalama za usafiri ambayo ni magari ya serikali na mabasi.

Walialikwa Mawaziri na manaibu waziri woote jumla wapo hamsini(50) na madereva wao hamsini wakisafiri hulipwa posho zote za msingi, bila kusahau Magari yao 50 ya kifahari yanasafiri kwenda Dodoma, mizunguko ya Dodoma kwa siku zote na yatarudi Dar na kufanyiwa service

Walialikwa Makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu woote jumla wanakaribia 45 na madereva wao 45 wakisafiri hulipwa posho zote za msingi, bila kusahau Magari yao zaidi ya 45 ya kifahari yanasafiri kwenda Dodoma, mizunguko ya dodoma kwa siku zote na yatarudi Dar na kufanyiwa service.

Viongozi wakuu wa ulinzi na usalama walialikwa pia waweza kuwa zaidi ya 20, hawa wanalipwa na serikali posho zao zoote na bila shaka walikuwa na magari yanayotumia mafuta na yenye atleast madereva 20 wanaolipwa posho zote zinazohusiana na kusafiri.

Inakadiriwa mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu walisafiri na wasaidizi wao kama vile personal secretaries(PS) ambao wanaweza kufanana na idadi ya hao viongozi, hawa pia wanastahili posho zao zote wanaposafiri kikazi.

Kuna ghalama za ukumbi na refreshments ndani ya ukumbi ambayo ghalama zake lazima ziendane na hadhi ya wahusika kama waweza nenda pale Ngurdoto katafute ghalama zilizotumika katika semina elekezi ya mwaka 2006 ndipo utajua serikali inatumia pesa kiasi gani kwa vitu kama hivi.

Usiombe ufanye kazi serikalini alafu uwe na roho ya uzarendo utapata taabu sana kisaikolojia. Hiyo yooote tisa sijakugusia kabisa pesa zitakazopotea kwa ajili ya mafuta ya magari yanayochukuliwa kwa ajiri ya msafara wa Rais hasa ukichukulia kiprotokali msafara wa rais unahitaji magari mazito zaidi ya kumi na hapa na-asume Rais na bodi gadi wake hawalipwi hata senti moja kwa siku husika na mbaya zaidi ni………..”

Kabla hajamalizia nikajinywea mchuzi wangu na kujiondokea maana kisha niingiza hasara ya kupoteza siku yangu mapema kabisa.

Pole sana Mkuu,

Kuna viswali vichache vya kujiuliza kabla ya kuweka mikono kichwani na kuendelea kumshangaa mkulu
*Hayo matumizi yalikasimiwa kwenye bajeti?
*Nini matarajio yake kwa Senema, sorry! semina hiyo elekezi?
*Kama taifa tutegememee nini? Usanii plus plus?
*Ziara zake Wizarani zimekuwa na mafanikio yepi kwake na kwa utendaji wa hao wasaidizi wake?
*Kwanini hakufanyia semina hii dar kupunguza matumizi yasiyo lazima ya vipesa vyetu vya mkopo?
* Anaongeaga nini na hao wasaidizi wake kwenye cabinet meetings?

Samahani, hivi katiba ijayo itaruhusu mwananchi kumkana rais wake kama haridhishwi na utendaji wake? wala msijibu!
 
Griiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii nimeshawahi kufanyia mkutano ule ukumbi gharama zake ni

Ukumbi wa executive 30,000,0000+ per day
Chai 10,000
Chakula cha mchana 20,000+
Chakula cha usiku 20,000+
Refleshment 10,000
Vyumba vya kulala vinaanzia 100,000+

Kwa mahesabu ya haraka utajua ni kiasi gani kitatumika kwenye accomodation

Kuhusu perdiems, fuel na service ya magari hapo ndio sijui

Hadi tumbo la kuhara limenishika sijui kama nitapata kidonge cha magnizium hapa dispensary yetu, hamjaniambia huko amana wagonjwa wanaendeleaje kuhusu kulala mzungu wa 4 kitanda kimoja wagonjwa 2, kuhusu madawa kama wamepata hilo ndo usiseme.Yani mpaka kununua mashuka tunaomba wahisani watununulie, hivi hizao hela si zingetosha kabisa kunua vifaa kama hivo

Napita tu
 
Afadhali mm nimeisoma jioni hi kwani thread hi ingeniharibia siku
 
Hapo kwenye red ni shilingi ngapi hizo! Nyie si mlikuwa mnacheka zile cheki zilizokosewa tarakimu?
Halafu mbona hamuonyeshi kukerwa na pesa zetu zinazotumika kwenye MAANDAMANO POTOSHI?!!!!
Au zile milioni saba na nusu anazoziponda JOSEPHINE kila mwezi!
Acheni ujinga! grow up!


Jesuit acha utani na ushabiki kwenye thread za masikitiko sijakuelewa unaposema maandamano potoshi na hii thread vinauhusiano gani? kwani dodoma yamefanyika na maandamano potoshi? rudi kwenye topiki plz
 
hapo kwenye RED maana yake ni kwamba hapo hapo kuna hotel Holiday inn ndio mafisadi wanakwenda kula lunch ya shilling 30,000/= na hapo opposite ndio wadanganyika tunakwenda kupata lunch yetu ya uhakika vile vile, ila muhimu kujaza tumbo bei ni kuanza 1500 na bei ya juu kabisa ni shilling 3000/=

Naomba nikusahihishe penye nyekundu hapo unataka kuupotosha umma, mimi leo nimekula wali nyama na mboga za majani pembeni kwa bei ya Ths1200 tu
 
kweli ni matumizi mabaya ya hela zetu wakati serikali haina hela, wizara na tasisi mbali mbali za serikali zilisha pewa waraka wa kupunguza bajet kwa zaidi ya 40% tangu januari, na sasa serikali inakopa ili kulipa mishahara.
Naona wanaohusika na hili huko serikalini ni vichwa maji na hawajui 'priority' kwa mambo ya wananchi na kuendesha serikali ni nini?
 
Dah na mie jioni yangu imeharibika kabsa, hivi hawa watu wanatuona watanzania ni madunya eeh?? Siku inakuja.
 
Ubadhirifu wa mali ya umma tu. Kama kweli kulikuwa na haja wangeweza kuweka kila kitu online, mtu anasoma, akimaliza anapigwa quiz, kwishney.

Hivi tunatumia teknolojia kubana matumizi kweli? E-Government iko wapi?

Kiranga kazi iliyoponi kubwa lakini may be mkubwa hajui haya. Kwa vitu kama hivi tuwalaumu wataalamu wengine.

Sasa hata director wa ICT akitaka kuwasiliana na mtu wake aliye ofisini mkoa fulani badala ya kutyumia skype au yahoo amabyo ni free kakariri lazima atumie simu ya TTCL hapo kuna tatizo.

Yaani kama vitengo vya teknolojia havutumii teknolojia ya kisasa na nafuu wanasiasa wataaanzia wapi??? Inawezekana Wataalmu wa IT wanasurbiri JK ambaye mwanasiasa. aje na wazo la kiteknolojia aseme nataka nifanye video conference ya Skype na wakuu wa mikoa wote .......

Sasa tujiulize director wa IT wa ikulu na director wa Communication wanataumiaje ujuzi wao na taaluma zao na available technlogies kumuwezesha rais kufanya baadhi ya kazi bila kuhitaji kuzunguka zunguka na kwa gharama nafuu ???

. Je wamependekeza mkuu akagoma? I dont belive so.


BTN

Mimi sioni ubaya wa hizi semina zinazoitwa elekezi kama zingekuwa zinachocchea outupu yeyote. Sijui amakuna mtu atasema before semina elekezi hali ilikuwa hivi baada ya semina elekezi imekuwa hivi.

Hivi kiongozi mlevi mapka kumuundia semina. si anaitwa ofisini tu. Semina elekezi laba ingekuwa ni kuwafundisha kufanya Decision Making. wangatfuta wataalam wa kuwapiga msasassa hawa viongozi wetu KJ angekaa magogoni tu
 
lm proud of my president, lm proud of his zuzuness mind.
 
I wish tungeingia ndani ya roho ya willy (slaa) tukaona uchungu anaopata. Tunaamshwa hatuamki!
 
Ningemuona ana maarifa sana kama angetangaza, kuanzia sasa sote tuliopo hapa dodoma ofisi zetu zipo hapa hakuna tena ofisi dar!kwani makao makuu ya nchi ni dodoma!

Na TRAFFIC JAM ingeisha
 
Halafu mbona hamuonyeshi kukerwa na pesa zetu zinazotumika kwenye MAANDAMANO POTOSHI?!!!![/COLOR]
Au zile milioni saba na nusu anazoziponda JOSEPHINE kila mwezi!
Acheni ujinga! grow up!


wewe kuna kitu kigumu utakuwa umekalia na kitakuwa kimekuingia! Na utakuwa unafurahia sana. Enjoy....!!!
 
Kwa binadamu wa kawaida vitu vinavyokuweka mahali pa heshima ni Busara, Aibu na Huruma na hivi havifundishwi darasani. Kwa kufanya "FUNGATE" ile pale Dodoma kipindi hiki ambacho "vice" ya hali ya maisha inazidi kumbana kila Mtanzania kunaonyesha UONGOZI tulionao umekosa vitu vyote vitatu vinavyoweza kuuheshimu. Naamini kama Chadema wasingekua na maandamano ambayo wananchi wanaonyesha hadharani kutoridhishwa na mwenendo wa Uongozi wa nchi na Chama kinachotawala hapa "PANGELIPUKA"
 
Back
Top Bottom