Nimegundua ZANTEL ndio baba lao Tanzania. Kasi ya internet, bando la uhakika MB na dakika

zantel ipo vizuri hata nikiendaga huku kijijini kwetu bado internet yake inakuwa inasoma H+

kuhusu vocha sihangaiki napata kwa tigopesa au tigo rusha kwa wakala wa tigo pesa
 
Zantel hawapo vizuri Kama mnavyowasifia humu
Ukweli wanaridhisha kulikohalotel kwa Sasa.
Gharama nafuu Sana internet kasi ya kawaida.
Nina halotel na zantel Ila to be honest go for zantel
Tigo, voda wako fasta Ila too expensive
 
Zantel hawapo vizuri Kama mnavyowasifia humu

Screenshot_20210503-201424.png
 
Habarini waungwana.

Nadhani mnakumbuka sekeseke la vifurushi kupanda lilivyoitikisa Tanzania na viunga vyake maana hadi sasa inakadiriwa Tanzania ina watumiaji wa internet million 32.

Pamoja na kwamba TCRA na Rais wa awamu ya sita mama, kuongelea kuhusu hili lakini dizaini kama vile makampuni ya simu yameweka mgomo baridi kwenye kushusha vifurushi vyao, mitandao mingine wameamua kabisa tena kwa makusudi kuondoa hata zile ofa ambazo wengine walikuwa wanaponea, mfano bando za usiku, bando za chuo n.k.

Nyinyi mtakuwa mashahidi 1GB inauzwa ghali kabisa na mitandao ya Vodacom, Tigo na hata Airtel, ni halotel pekee na TTCL wanauza 1 GB kwa 1000 ila hata hao haloteli mtandao wao kama Airtel, nunua bundle network tafuta mwenyewe. Na wakikupa hiyo 1GB dakika za kuongea hawakupi. Wakikupa ni haloteli kwenda haloteli.

Zantel wamekuja na mapinduzi ya kufa mtu. Kwa 1500 unapata 1.5GB, dakika 160 mitandao yote na sms 500. Hamna mtandao wenye ofa kama hiyo na hapo hapo internet yao ina kasi ya kufa mtu. Mie niko maporini huku lakini kama niko jijini dar es salaam. Tumieni zantel wakuu hamtajuta.

Nina line 6 za simu mtu hanidanganyi kitu chochote kuhusu mtandao wowote. Nimeandika baada ya kufanya research yangu ndogo tu.

Uzi tayari.
Hakuna wa kukudanganya meku

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom