Nimegundua mpenzi wangu kanichoka

Nimegundua mpenzi wangu kanichoka

Bata batani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
3,257
Reaction score
3,905
Ndugu zangu wana JF naombeni ushauri, nahisi kuchanganyikiwa vituko na visa ninavyofanyiwa na mpenzi wangu. Imefika hatua nimegundua huyu Bi. Dada kanichoka ila yupo na mimi basi tu kwa heshima tu ya mzazi wangu tu na ndugu zangu kwa sababu tu wanamkubali.

Lakini ninachokiona nimechokwa kwani hatuna maelewano nimejaribu mbinu zote kujishusha kukubali yaishe lakini wapii

Naombeni ushauli wana JF uamuzi mzuli wa kuchukua
 
Wewe ndio mwenye matatizo. Siku zote mwanaume unatakiwa kuwa kiongozi wa maisha yako na kufanya maamuzi unayoona yana manufaa kwako. Sasa kama wewe umeshaona kabisa mtu amekuchoka, unachoendelea kung'ang'ania hapo ni kitu gani?

Hivi kuna raha gani ya kuwa na mwanamke ambae amekuchoka na umeshajua kabisa kwamba amekuchoka? Unafikiri kujishusha na kulia lia ndio kutamfanya aache kukuchoka au ndio anazidi kukuchoka zaidi? Tembea mbele mkuu wanawake wamejaa
 
Pole mkuu naomba unipatie namba yake na kapicha kake nione namna ninavyoweza kusaidia
 
We tulia fanya mambo yako kama ni wako atajirudi tu ila kama sio wako tena/ hakupendi ndio basi tena. Acha tabia ya kumlilia lilia hiyo ndo inampa kiburi cha kukuonesha kuwa amekuchoka


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wewe ndio mwenye matatizo. Siku zote mwanaume unatakiwa kuwa kiongozi wa maisha yako na kufanya maamuzi unayoona yana manufaa kwako. Sasa kama wewe umeshaona kabisa mtu amekuchoka, unachoendelea kung'ang'ania hapo ni kitu gani? Hivi kuna raha gani ya kuwa na mwanamke ambae amekuchoka na umeshajua kabisa kwamba amekuchoka? Unafikiri kujishusha na kulia lia ndio kutamfanya aache kukuchoka au ndio anazidi kukuchoka zaidi? Tembea mbele mkuu wanawake wamejaa
Ushafunga uzi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom