Nimegundua mimi si binadamu wa kawaida. Tena si Mtanzania Halisi.

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,515
Yaani sina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Ukifanya vizuri hata kama juzi tumetukanana nitakusifia kuwa hapo umefanya vizuri.

Ukikosea hata kama asubuhi nimeamka na wewe na ni mrembo sana nitakuambia ukikasirika shauri yako mi nimeshakuambia. Hata kama ni jamaa,mshkaji,ndugu au rafiki wa karibu nakwambia tu ukichukia sawa ukielewa sawa maisha yanaendelea.

Na kama nlikosea sehemu ukanyamaza na ukijua nimekosea au nakosea ntakuja kukwambia tu kuwa hiyo ni roho mbaya. Ya kichawi na kinafiki. Mkosoe mwenzio na mrekebishe.

Humu JF nmejikuta ninaendelea na tabia hiyo hiyo...nikiona mtu anataka attention za kipuuzi au kuwalisha watu matango pori au uyoga wenye sumu namchana tu. Haijalishi dk kadhaa zilizopita alisifia au kukandia uzi wangu.

Style hii ya maisha inanifanya niwe na amani muda wote. Sijali wala nini. Na sina stress na sibebi kinyongo au chuki. Mi nakutapikia nyongo.nabaki mwepesi nasonga zangu mbele.

Hii si tabia ya kawaida TENA KWA WATANZANIA. NI WANAFIQ SANA. NDO MAANA NIKAWA NAAMBIWA NA WATU MI SI WA KAWAIDA.

Nimekaa pale. 👉
 
Dah bora wewe umegundua ni binadamu ila sio wa kawaida...Mimi niligundua kuwa sio binadamu kabisa...Yaani nilipopima Xray & MRI inaonekana sina maini, nyongo, mapafu, moyo na bandama....Vyote vimekuwa replaced na viungo vingine ambavyo hata madaktari walikuwa wanavishangaa.

Nilipowauliza wazazi kwa makini wakaniambia ukweli kuwa hawakunizaa ila waliniokota kama kichanga shambani porini...ila sehemu nilipookotewa kulikuwa na shimo kubwa yani kama nilianguka kutoka juu kama jiwe...Wanahisi nimetokea sayari nyingine.
Nina uwezo wa kuread minds, au kujua past/ future ya mtu nikimtazama kwa muda mrefu
 
ulivyo ww basi haupo peke yako ... wapo watu elfu 1000 sample yako kwhy usijishangae sana wala nn.... nenda uwanja wa ndeg wa egypt kuna bango pale la kukukribisha utajfunz kitu
 
Back
Top Bottom