Hawa ndio wanawake wa kizazi chetu. Mimi siwaelewi, sijui ninyi

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,961
Hiki ndicho kizazi cha sasa kizazi cha hovyo cha wanawake wasioweza kukaa sehemu moja ya mahusiano kwa muda mrefu bila kutafuta au kujipa sababu ya kwenda sehemu nyingine ya mahusiano sababu ya hofu ya kujicommit na mahusiano ya kudumu. Kizazi cha kuanza na kuachana kama mchezo. Yaani "Hook up n Break up culture".

Wanawake maneno / kauli zao haziendani na matendo. Midomoni wanasema wanaume serious wapo wapi, natafuta mume mwema, napenda maisha ya kifamilia ya baba mama na watoto ila akilini, moyoni na nafsini mwao wanajua wazi kuwa hicho wanachosema wenyewe hawakiamini hata kidogo na ndio maana hawapo tayari kuishi sehemu moja kinyumba ingawa wakifikiria maisha ya baadae wanapatwa na hofu ya kutisha je maisha baada ya ujana nitamringia nani na nitakuwa mtu wa aina gani nje ya mfumo wa maisha ya kifamilia.

Hawawezi hata kuimagine namna gani wataweza ishi na mtu m'moja milele hadi uzeeni na kujiwekeza kwake tu bila kujihusisha na mtu mwingine nje ya huyu wa sasa ndio maana lazima wakimbie tu baada ya usiku moja wa ngono au siku kadhaa za ngono.

Hawa wa sasa wanachukia wazo la kudumu na mtu m'moja kama baba na mama au babu na bibi vile waliishi na ndio maana hawapo tayari kufanyia kazi hilo wazo litimie katika maisha yao wanaona ni kama aina ya uovu dhidi ya uanamke kuishi na Mwanaume m'moja maisha yote.

Wanawake wa sasa wanataka kuamini kuwa wao ni breed ya tofauti ya binadamu na hivyo wanatakiwa kuishi kwa misingi tofauti na vizazi na vizazi vya karne na karne huko nyuma ambavyo vimepokea , kurithishwa na kudumu na mfumo huu wa kuishi ndani ya familia na mwanaume m'moja. Wanataka kuamini kuwa wao huu utamaduni hauwahusu na ni utamaduni wa kutoka ulimwengu wasioufahamu wala hakuna mtu kwenye asili yao alishawahi kuuishi na ndio maana ukikuta anabishia au kubishana na mifumo ya ndoa na kutetea mifumo kinyume na Ndoa mtazame usoni namna anavyoongea kwa kujiamini na kustaajabu wewe unaemshangaa kwann anakengeuka na kulazimishwa kufuata mfumo wa maisha ambao kila binadamu kaumbiwa kuishi ndani yake.

Ni kizazi cha wanawake wanaojitambua kuwa wamezaliwa katika ulimwengu huru na hivyo wanatakiwa kuishi uhuru huo. Wanaamini wao ni kizazi huru katika kila eneo bila mipaka sio kiuchumi, kisiasa , kijamii, kijinkijinsia, popote wanaweza fanya lolote bila kuwajibishwa na hata wakikosea jamii ndio itabeba kuwajibika kwa niaba yao. Wapo huru kulala na yeyote wakati wowote wanapojisikia na popote pale. Watakataa kufanya mazuri na kukubali kushiriki mabaya sababu wao ni viumbe huru.

Kwa kiburi au utomvu wa nidhamu wameridhia kutenganisha tendo la ngono na upendo ili walitumie tendo hili raha yake kama dhamana ya kuishi katika jamii na silaha ya maamuzi ndio mwanamke silaha yake kubwa kwa sasa ni kumnyima mwanaume ruhusa ya kulala nae labda abakwe.

Kizazi cha wanawake wanaoamini katika kuvutiwa kwa kupewa vitu vya kusisimua akili kisha bila kutafakari mara mbili kinachofuata ni kulala kwanza na mwanaume ndipo aamue kama kumpenda au kutompenda itafaa. Kizazi ambacho kipo haraka sana kuoffer ngono na sio loyalty.

Kizazi cha wanawake wanaoamini katika "Open relationship" status kwa makusudi na kujifanya hawajui ina maana gani ila wanajua kuifanya sawa na mlevi anayekunywa ulevi fulani na anaujua ladha yake hata akiwa usingizini halafu akwambie hajui unaitwaje,haimake sense.

Kizazi cha wanawake kinachoamini katika "Open relationship" yaani kuwa na mahusiano na mtu ambaye kila mtu anamfahamu kisha kuwa na wengine kumi pembeni ambao si kila mtu anawafahamu ila wanamahusiano ya kingono.

Kizazi cha wanawake wanaoamini katika urafiki wa faida yaani "Friends with benefits" . Hapa utakuta yule rafiki wa kiume ambaye anajua kuwa huyu binti ni girlfriend wa fulani ila mimi ninahitaji tu kupewa nafasi ya kufanya mapenzi na kuinjoy penzi la wizi huku tukimuinjoy jamaa kila anapotukuta sehemu kwa kujifanya marafiki kumbe sisi ni undercover F*ck mates.

Kizazi cha wanawake wasiotaka au kujenga mashiko katika mahusiano wanayopitia yaani "No strings attached", atakutana na mwanaume Club, au kwenye harusi, au kwenye mgahawa, au popote pale ili mradi alisimamishwa kwa utulivu na akavutiwa na sauti yake, perfume yake nzuri, mavazi, gari etc na kupewa mualiko sehemu nzuri ya kufurahia saa kadhaa. Atakwenda na kujikuta ameshavua nguo na kupigwa ududu hadi kuridhisha nafsi kisha baada ya hapo ni tusiwasiliane wala kutafutana sababu boyfriend au mume wake atagundua hiyo dirty secret. Ila atamtafuta tena kama atataka show tamu kama ile tena wakati mwingine.

Wanawake walioacha nafasi ndogo sana ya kumjua mtu kwa haiba yake ya makuzi na malezi ya asili sio hizi haiba za mitandaoni au kwenye movie. Kila mwanamke anataka mwanaume anayeonekana na kubehave kama wale top movies stars and actors wa famous Hollywood movies au mastars wa muziki ila sio kwa namna ya uhalisia wa namna mtu kazaliwa. Leo si haba utasikia binti anasema mimi napenda mwanaume kama Idris Elba maneno hayo anamtamkia kijana mwenye mwili wa kawaida mwenye kimo cha kawaida cha futi tano kamili au futi 4.9 ambaye akiyasikia hayo maneno atajikuta anajiuliza ina maana yeye sio binadamu kama Idris Elba na afanyaje ili kuongeza urefu na kutanuka mbavu awe kama Idris Elba.

Wanawake wasiothamini mahusiano kama sehemu ya kujengea maisha na kuandaa future zao kwa maisha ya baadae ila wanaothamini hali za kimahusiano kama sehemu ya kujibanza wakisubiria kuhamia sehemu nyingine ambayo itamletea new excitement. Kwa kifupi hawaoni thamani ya kuwa ndani ya relationship kwao ni kazi sana kubeba majukumu yake ila wapo comfortable kuwa katika situationships ambazo zinawapa comfortzone ya kusurvive na kuescape relationship responsibilities.

Wanawake ambao watamuacha the most suitable and compatible and deserving partner kwajiri ya kumtafuta "that perfect handsome Prince charming au Black Knight" atakae kuja na kumfanya asikie raha kama amefunguliwa milango ya mbingu na kukaribishwa chumba chenye kila anachotaka kwenye akili yake. Mwanaume ambaye kiuhalisia the more anafit 100% profile wanataka the more anakuwa si wa ukweli kiuhalisia na possibility ya kukutana nae in life ni slim zero to none.

Hawa ndio wanawake waliokuzwa na jamii na kuandaliwa tukutane nao katika enzi hizi. Salamu kwa watoto na wajukuu,vitukuu,vining'ina na Vilembwe zetu na vizazi vijavyo mtatusamehe sana babu zenu kwa kuwaangusha kujenga misingi bora ya jamii na familia bora kutokana na aina za mabibi zenu ambao tulikuta nao kizazi chetu hiki. Walijitoa ufahamu ili wao wafurahie maisha ya huu ulimwengu bila kujali hatima yenu sisi na wao tukishaondoka.

Babu na bibi zetu sisi wa miaka mingi iliyopita, walipambana kutuimarisha na walitujengea misingi ambayo sisi babu zenu tulipokea ila bibi zenu wakagoma na kusema ni misingi ya kipumbavu na kuipa majina mengi ya ajabu kama Mfumo Dume, unyanyasaji na ukandamizaji wa wanawake, na kujiamulia mifumo yao ya kuishi ambayo mingi walikopi kutoka mataifa ya magharibi kupitia mitandao ya kijamii na television (sijui kama bado mtakuwa mnatumia hizo mifumo au kutakuwa na maboresho zaidi).

Tunaweka kumbukumbu sawa kuwa bibi zenu wamechukia sana Ndoa kwenye matendo yao ila midomoni wanaongea tofauti.

Mjihadhari sana na vitu watakuja kuongea wanawake wa kizazi chenu kuwa sisi wanaume ndio wakorofi na msije mkaamini. Tulikuta kanuni kuwa wanawake hawatakiwi kuongea kwenye kikao cha wanaume na hawatakiwi kuwa na nafasi ya maamuzi tukatengua hizo mila tukijua ni kuwaonea wanawake na kuwanyima haki zao za kimsingi ila enyi wajukuu zetu wa kizazi kipya kama mtaweza kuandika katiba naomba muonane na Taleban (kama bado watakuwapo) wawasaidie kutengeneza katiba na sheria juu ya wanawake maana wale jamaa ndio wanajua namna ya kuishi na kuwamudu wanawake sisi tumeponzwa na ujuaji wetu wakuona wanawake ni viumbe dhaifu na wanahitaji sana sauti na kupewa kipaumbele ila sasa tunajuta. Msije mkakosea kama sisi wala kurudia upuuzi tuliofanya.

Nyoka aliyejeruhiwa na kuokotwa na msamaria mwema sasa kaanza kupona na ameanza kupanga njama za kumuuma msamaria mwema kama shukurani yake. R
 
1
FB_IMG_1654021136637.jpg
 
Hiki ndicho kizazi cha sasa kizazi cha hovyo cha wanawake wasioweza kukaa sehemu moja ya mahusiano kwa muda mrefu bila kutafuta au kujipa sababu ya kwenda sehemu nyingine ya mahusiano sababu ya hofu ya kujicommit na mahusiano ya kudumu. Kizazi cha kuanza na kuachana kama mchezo. Yaani "Hook up n Break up culture".
😂😂😂😂😂😂. Invest in yourself bro acha kulilia mapenzi ya kweli mapenzi hayo utayapata kwa muumba wako pekee hawa wengine ni kanyaga twende ,,,,,,,,, hujiulizi kwann domo anawatafuna ka big G alafu anawatupa huko kaa chonjo mkuuu 💩💩💩💩💩
 
Back
Top Bottom