Nimegundua makosa madogo ya kiuandishi katika Press Release ya leo iliyotolewa na Madam Zuhura Yunus

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,022
144,380
Japo mimi sio mtaalama wa maswla ya uandishi na wala si mwandishi wa habari, ila nimegundua makosa madogo ya kiuandishi katika Press Realease ya leo iliyotolewa na Madam Zuhura Yunus aliefanya kazi kwenye chombo kikubwa cha habari kama BBC.

Kwa uelewa wangu mdogo, Dada yangu Zuhura anakosea katika matumizi ya comma, ila kutokana na unyeti wa nafasi yake, makosa haya yasipuuzwe unless mimi ndio niko wrong.

Kwa mfano, neno TPA liloko katika mabano, lilipaswa kufuatiwa na comma kabla ya kutaja jina la Ndugu Eric Hamisi ambae uteuzi wake umetenguliewa.

Kasoro nyingine naiona katika hii sentesi: "kabla ya uteuzi huo".

Kwa uelewa wangu mdogo, mwisho wa sentesi hiyo fupi, kulistahili kuwa na comma kabla ya kuendelea na sentesi iliyofiuayta inayoanza na "Ndugu".

Ukiacha kasoro hizo mbili, hata hii sentesi: "Ndugu Plascude Mkeli Mbossa" , iliostahili kufuatiwa na comma kabla ya kuendelea na maneno yanayofuayta (yaani ingeandikwa hivi: "Ndugu Plascude Mkeli Mbossa, ......").

Hata katika aya ya kwanza, sentesi: "...... leo 04, July 2022 ......" comma ilipaswa kufuata baada ya 2022 na kisha ndio angeendelee na maneno yaliyofuata(yaanii ingekuwa hivi: "..... leo 04, July 2022, ametengua ......).

Kama nimekosea mnisahihishe, ila kama niko sahihi kama navyoamini, wataalamu wa uandishi watakuwa wanaona makosa mangapi na ukizingatia hii ni document kutoka ofisi kubwa kabisa kwa nchi yetu?

Kwakweli kama ni kupitiwa au alisahau kufanya editing, basi walau kasoro hiyo ingejitokeza mara moja au mbili, ila hapa imejitokeza mara tatu na si ajabu kuna makosa mengine yanayoweza kuainishwa na wataalamu wa uandishi.

Ukosoaji huu ni kwa nia njema kwani document kama hii inasomwa na watu wengi wa ndani na nje ya nchi.

Sisi wengine hata tukichapia sawa tu, ila sio Zuhura kwa nafasi aliyonayo, na pia kwa fani aliyonayo ya uandishi wa habari.

NB: Tatizo kubwa hapa si typing error, kosa ambalo wengi hulifanya/tunalifanya, bali tatizo linaoonekana ni Mhusika kuwa na udhaifu kwenye matumizi ya "comma" kwenye uandidshi na ndio maana kasoro husika imejirudia zaidi ya mara tatu kitu ambacho sio kizuri kwa mtu kama yeye ukizingatia wadhifa alionao.

1656958222189.png
 
Makosa ni mengi tu kiukweli.

Hata uandishi wa tarahe haujakaa sawa,pia neno Ikulu mwisho wa habari lilipaswa liwekewe nukta lakini hajafanya hivyo!!


Alama za uandishi hazijazingatiwa kabisa. Kuna haja kubwa sana kufanyiwa kazi haya makosa madogo. Kuandika tarehe "4Julai,2022"aise HAPANA!!
 
Makosa ni mengi tu kiukwelo.

Hata uandishi wa tarahe haujakaa sawa,pia neno Ikulu mwisho wa habari lilipaswa liwekewe nukta lakini hajafanya hivyo!!


Alama za uandishi hazijazingatiwa kabisa. Kuna haja kubwa sana kufanyiwa kazi haya makosa madogo. Kuandika tarehe "4Julai,2022"aise HAPANA!!
Ukosoaji huu akiuchukulia positive, utamsaidia, vinginevyo anajiharibia.
 
Mkuu wala usiwaze, unapaswa kukosoa pale unapoona hapako sawa.

Lakini makosa haya yapo kabla ya zuhura, nadhani ni kama hakuna anayejali. Wakati wa Jaffari haniu ndio makosa yalikua mengi hadi basi, majina ya wateuliwa yanarudiwa rudiwa mara mbili, baadhi ya sehemu zinasahaulika n.k
 
Tatizo la kuandika maneno kwa usahihi, matamshi, kuweka alama sahihi kwenye sehemu sahihi ni kubwa zaidi ya hapa kwa Zuhura Yunus.

Wanaoandika au kutangaza huajiriwa bila kuzingatia umuhimu wa hayo, kwa kuwa hata waajiri ni walewale.

Tukirudi kwa Zuhura na wakubwa wengine, wao huandikiwa na kama wanaoandika hawajui, na kwa kuwa wao huamini wanacholetewa kipo sawa, basi sisi tunayapata kama hivi na hivyo ukosoaji kama huu.
 
Nijuavyo kwa ufupi kuhusu matumizi ya comma na nukta.

Comma inatumika pale ambapo unaendelea kuelezea jambo husika, kama habari inamuhusu Salary Slip basi mtu hutakiwa kuweka comma kwa kila jambo linalomuhusu Salary Slip.

Nukta hutumika pale tunapoanza kuzungumzia jambo jipya, mfano, baada ya kumzungumzia mtu wa kwanza, anayefuatia nae huanza kumzungumzia kwa baada ya kuweka nukta kwa yule aliyemtangulia.
 
Kwa uelewa wangu mdogo, Dada yangu zuena anakosea katika matumizi ya comma, ila kutokana na unyeti wa nafasi yake, makosa haya yasipuuzwe unless mimi ndio niko wrong.

Hata katika aya ya kwanza, sentesi: "...... leo 04, July 2022 ......" comma ilipaswa kufuata baada y 2022 na kisha ndio angeendelee na maneno yaliyofuayta(yaanii ingekuwa hivi: 2022, ametengua ......).
Simtetei, ila hata mimi nimeona makosa kwenye uandishi wako.
Kwenye quote ya kwanza, dada yetu anaitwa Zuhura, siyo Zuena; na jina lilipaswa kuanza na herufi kubwa.
Kwenye quote ya pili, neno 'yaliyofuayta' lilipaswa kuwa 'yaliyofuata'.
Ni hayo tu.
 
Mleta hoja hapa hata wewe bandiko lako la masahihisho kwa Zuhura Yunus lina makosa mengi sana. Ulitakiwa "kuliediti" kabla hujaruhusu au hujaliachia liende hewani.
 
Back
Top Bottom