Nimefurahishwa na maamuzi ya CAF kumvua ubingwa Senegal

Nimefurahishwa na maamuzi ya CAF kumvua ubingwa Senegal

Umejitahidi kusite mifano but mifano uliyotoa badala ya kuongeza uzito wa hoja yako ndo kwanza inaififisha hoja. Hivi unajua kuwa match fixing ni kosa kubwa sana kwenye any sport field si kwenye football tu. Kupanga matokeo unakula na kifungo kabisa, kupigwa life ban au timu kushushwa madaraja ya chini kama ilivyotokea kwa Juventus.
Lakini ishu ya Senegal ni tofauti kabisa waligomea mchezo kwa dkk kadhaa then gemu ikaendelea kwa refa kuendeleza mchezo na mshindi kupatikana kihalali kwa matokeo ya uwanjani(ambayo kimsingi hayabadilishwi na maamuzi mengine). Kama senegal wangegoma kabisa na refa akamaliza mpira sheria hii ingetumika.
Kifupi bodi ya rufaa ya Caf imepuyanga kama ilivyopuyanga Cuf ya Lipumba. Caf na Cuf sasa hivi zote ni Cuf
bahati nzuri caf walikabidhi ubingwa kwa senegal na adhabu walitoa kuashiria mwisho wa mashindano,ilikuwaje tena wakakaa kamati na kuja na hii mpya ya kuvua ubingwa? Hawa CAF ni wa kuchunguzwa na wao pia.
 
20260318_152545.jpg
 
Mkuu ni kosa kubwa kuhatarisha amani ya uwanjani, sasa uliza kwanini walirudi uwanjani?
Vita ni vita kumamake unafikiri km wakipewa ushindi wa Mezani unachezea unaenda kusema kwa Mama naenda kusema kwa Mama ukitegemea Mama atakupa ushindi wa Mezani, CAF wamezingua wanaongozwa na vilaza pumbafu ni wameharibu historia ya mpira Afrika na dunia kwa ujumla
 
Senegal walifanya uhuni. Kisheria refa alitakiwa amalize mechi pale pale uwanjani na Morocco atangazwe bingwa. Lakini zikatumika busaraa. Baadae senegal alipewa adhabu kwaiyo hapakua na haja ya kumpokonya ubingwa. Senegal walizingua, CAF wamekuja kuzingua zaidi
 
Senegali walifanya tukio la aibu mbele ya wageni na dunia nzima. Wakati mpira wa Afrika ukianza kuimarika na kutazamwa na watu wote dunia wao Senegal hawakuona hilo na wala hawakuweza kufikiri nini kinafuata.
Mpira ni biashara na hatima za maelfu ya watu unawezaje kufanya blander kama ile kwenye uwanja wenye watazamaji zaidi ya elfu 50? Ulitaka wauane? Ulitaka wadhamini wa mashindano walifikirie vipi soka la Afrika?



1. Juventus – Serie A (2005 & 2006)

Walitwaa ubingwa wa Serie A
Baadaye walinyang’anywa makombe yote mawili kutokana na kashfa ya kupanga waamuzi (Calciopoli)
2005 haikupewa mtu, 2006 walipewa Inter Milan

2. Olympique de Marseille – Ligue 1 (1992–93)
Walitangazwa mabingwa wa Ligue 1
Baadaye walinyang’anywa ubingwa huo baada ya kuthibitika kupanga matokeo (match-fixing)
Huo ubingwa haukupewa timu nyingine

3. Steaua Bucharest vs Dinamo Bucharest – Kombe la Romania (1988)
Mechi ya fainali ilisimamishwa kwa utata
Kwanza kombe walipewa Steaua, kisha likaondolewa/kuhamishwa kwa maamuzi ya kamati
Tukio hili linajulikana kwa mzozo mkubwa wa kisiasa wakati huo

4. FC Sion – Kombe la Uswisi
Walishinda Swiss Cup
Baadaye wakanyang’anywa haki ya kushiriki mashindano ya Ulaya kwa kutumia mchezaji asiye halali
Ingawa kombe lenyewe halikuondolewa moja kwa moja kila wakati, ushindi wao uliathiriwa rasmi

5. Legia Warsaw – Ligi ya Poland (1992–93)
Walimaliza juu kwenye Ekstraklasa
Lakini walinyang’anywa ubingwa kwa tuhuma za kupanga matokeo mechi ya mwisho
Ubingwa ulipewa timu nyingine
Dogo unahusisha kupanga matokeo na tukio la Senegal? Mbona unachekesha?
FIFA inainyang'anya timu iliyosusia mchezo. Kumbuka "kususia*. Senegal walimaliza dakika zote tisini uwanjani. Je, unaweza kusema walisusia?
 
Senegal walifanya uhuni. Kisheria refa alitakiwa amalize mechi pale pale uwanjani na Morocco atangazwe bingwa. Lakini zikatumika busaraa. Baadae senegal alipewa adhabu kwaiyo hapakua na haja ya kumpokonya ubingwa. Senegal walizingua, CAF wamekuja kuzingua zaidi
Referees wote waliochezesha mechi za Morocco walizingua sana(viashiria vya rushwa).
Kwa kuwa referee alisubiri mpaka timu ikarudi mpira ukaendelea, uamuzi wa refa ndiyo ulikuwa uamuzi halali wa mwisho.
Kilichowauma plan zao hazikufanikiwa, penati ya mchongo wakashindwa kufunga na mshindi halali akapatikana uwanjani.
 
Referees wote waliochezesha mechi za Morocco walizingua sana(viashiria vya rushwa).
Kwa kuwa referee alisubiri mpaka timu ikarudi mpira ukaendelea, uamuzi wa refa ndiyo ulikuwa uamuzi halali wa mwisho.
Kilichowauma plan zao hazikufanikiwa, penati ya mchongo wakashindwa kufunga na mshindi halali akapatikana uwanjani.
Yap, kama refa akiendelea na mchezo maana yake matokeo ya mwisho ndio yatahesabika. Mechi imalizike halafu umpe ubingwa alieshindwa hiki ni kituko
 
Back
Top Bottom