Bunge la Senegal limemchagua Waziri Mkuu wa zamani, Ousmane Sonko, kuwa Spika mpya. Hatua hii inaweza kumpa jukwaa lenye nguvu kubwa la kutoa upinzani kwa Rais Bassirou Diomaye Faye.
Spika wa zamani wa bunge hilo, El Malick Ndiaye, alijiuzulu Mei 24, 2026 hatua ambayo wachambuzi wa mambo wanasema ililenga kumpisha Ousmane Sonko ili agombee nafasi hiyo ya mkuu wa bunge, ambako chama chake cha Pastef kina idadi kubwa ya wabunge.
Wabunge waliitwa kwenye kikao kamili cha bunge leo Mei 26, 2026, ambapo Sonko alirudishwa kwanza kuwa mbunge na kisha akachaguliwa kuwa Spika wa bunge hilo.
Hata hivyo, wabunge wa upinzani nchini Senegal walisusia kikao hicho cha bunge.
Mapema leo Mei 26, 2026 Rais Faye amemteua Ahmadou Al Aminou Lo, kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
Soma pia
Source: TRT AFRIKA

- Rais wa Senegal amteua Waziri Mkuu mpya Ahmadou Al Aminou Lo
- Spika wa Bunge Senegal ajiuzulu, aeleza ni kwa Maslahi mapana ya Taifa
Source: TRT AFRIKA