Nimefunga kwa ajili ya Taifa stars

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,685
29,007
Mzuka wanajamvi!

Kwaanzia usiku huu hadi kesho jioni nimefunga kwa ajili ya timu yetu pendwa ya taifa stars ishinde mechi zake zote zilizo salia na ifuzu kombe la dunia. Sitakula, kunywa wala kuvuta hadi kesho jioni.
 
Mzuka wanajamvi!

Kwaanzia usiku huu hadi kesho jioni nimefunga kwa ajili ya timu yetu pendwa ya taifa stars ishinde mechi zake zote zilizo salia na ifuzu kombe la dunia
Hahaaa!!kudra hazishindi uwezo!!japo ni vizuri kutiana moyo lakini ukweli "HATUTOBOIIII!!!
 
unaacha kuombea mambo muhimu,,,,,,,unaombea mpira,,,,,,
Unajuaje siombeagi mambo mengine? Maombea sana lakini hii ni siku maalum ya kuiombea taifa stars na tutashinda mechi zote zilizo salia. Tukutane kesho baada ya mechi.
 
Hapo kwenye kuvuta sikushauri mkuu vuta tu kila kitu and wait, time will tell kwa Stars yetu hii ni matumaini tu.
 
Kwa tozo hizi na vifurushi kupanda unapata wapi mzuka wa kuacha kula kwasababu ya taifa stars?
Kibaya zaidi wahamasishaji ndiyo wenye tozo.
 
Mara paap! Taifa stars ikashinda mechi zake na kuinigia top ten halafu huko nako ikashinda na kutika qatar kukutana na miamba ya soka duniani, timu kama uingereza, brazil, ujerumani, argentina na italia ikachezea kichapo cha aibu kwa tanzania wenye imani haba wasioamini haya wataficha wapi nyuso zao? Mpira unadunda na una maajabu yake, congo drc inafungika kirahisi tu na tanzania licha kusheheni wachezaji wanaocheza ulaya na kwingineko kwenye ligi maarufu.
 
Nimefunga arobaini, pamoja na maombi mengine naomba Mungu amwondolee Freeman Aikaeli Mbowe teso hilo.

Kipimo walichompimia watesi wake wapimiwe wao na kusukwasukwa.
 
Back
Top Bottom