Nimefiwa...

Pole mkuu mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu !
 
Poleni sana Mkuu!
Tunamwomba Mungu amlaze Marehemu Pahala Pema na nyinyi wafiwa Mungu awape nguvu na subira.
R.I.P. Nelasi
 
Pole sana bwana Mphavu kwa yaliyokukuta. najua ni jinsi gani unaumia kwa hayo yalitokea lakini yote ni mipango ya Mola na kazi ya Mungu haina makosa, cha kufanya tumuombee kwa Mola ili apate kupumzika kwa Amani. Pole sana bwana Mphavu.
 
Pole sana ndugu yetu!
Huo ni mtihani so unapaswa kuushinda kwa kumshukuru mungu!
 
@Wote.
Nashukuru kwa pole zenu, nimefika hapa msibani kama masaa mawili yaliyopita, mwili bado uko hospitali, leo ndo tutaaga na kusafirisha kuelekea Mbeya kwa maziko.
 
poleni sana! Yote hayo ni mapenzi ya Mungu inabidi 2mshukuru Mungu kwa kila jambo
 
Pole Mphamvu,
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Tunawatakia mazishi na maziko mema, na Mungu akusimamie kwa kila kitu,
Ameeen.
R.I.P NELASI,Tuko nyuma yako.
 

hii ni CHIT Chat?

Pole kwa msiba. nafikiri iende kwenye jukwaa jingine kama sio chit chat
 
Pole sana ndugu yetu jikaze kipindi hiki kigumu zidisha ibada saaana Mungu atakusaidia
 
Kama nilivyowajuza awali, msafara umeondoka kuelekea Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (anakofanyia kazi baba mzazi wa marehemu), nako wametoa heshima zao za mwisho, kisha ukaelekea Ihanda, Mbozi kwa ajili ya maziko. Msafara umetoka Iringa majira ya saa mbili usiku, hii ni kwa mujibu wa babake marehemu. Mimi, sikusafiri na maiti, bali nimebaki Morogoro kwa ajili ya kuweka mambo sawa wakati huu ambako wenye mji hawapo.
 
Poleni sana mkuu! Mungu ameruhusu yatendeke, tumwombe ampuzishe marehemu pema peponi. Amen
 
Pole sana mjamvi mwenzetu, fikisha pole zote hizi za JF pale msibani, endelea kujiliwaza na JF wakati huu wa msiba hasa chitchat na jokes. Tafadhali sana usiingie kwenye jukwaa la siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…