Nimefiwa na Mama Mzazi

Pole sana mkuu,mungu akuongoze katika kipindi hiki kigumu
Msiba uko wapi?Kama nasi wa JF twaweza kushiriki kwa hali yoyote ile?
 
Pole sana Kamanda wetu!

Ni kweli sote tu wapitaji ila hakika ni mbaya kutangulia.
Najua una wakati mgumu ktk siku kama hii,lakini nina IMANI kwa kuwa tuna MUNGU mwenye uwezo atakujaza nguvu na utarudi ktk hali ya Imani Kamanda wetu!

Piga moyo konde ktk kipindi hii kigumu!
MUNGU MWENYE UWEZO MLAZE MAMA YETU KTK MALAZI YA AMANI YA MILELE NA SIKU MOTA TUTASHANGILIA NAYE PASIPO KUKOMA!

MAMA YETU LALA KWA AMANI YA BWANA!
Amen!
 
Pole mkuu 4 this sad moment u r having! Mungu amlaze pema ua beloved mom!
 
Pole sana Mkuu, Mama apumzishwe mahali pema nawe upate faraja kwa maombi na sala zetu
 
Ni Allah ndie atupae uhai na kuundosha pale siku zetu za kuishi hapa duniani zinapotimia.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Allah alikuze kaburi la mama etu mpendwa,
alijaze nuru, heri na baraka tele astahilizo kiumbe mwenye amali bora duniani
Mola amsamehe na kumfutia madhambi yake yote,
makubwa kwa madogo na abaki kama siku aliyoiona dunia kwa mara ya kwanza.
Utulivu na amani pamoja na Baraka za Allah ziwe juu yake.
Halikadhalika, Allah akujaze wewe pamoja na familia yako yote
Imani, ujasiri na ustahimilivu katika kipindi hiki kigume kwenu.
Pole sana Ustaadh wangu.
 
Pole sana Kiongozi mwenyeezi mungu aipumzishe roho ya marehemu kwa amani na wafiwa awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wenu alowaleta hapa duniani....
 
Maalim Ustaadh Xpaster, pole kwa msiba huo mkubwa. Mungu Mwenye enzi awatie nguvu ktk kipindi hiki kigumu.
 

INNAA LILLAHI WAINNAA ILAYHI RAJIUUN . Mmungu amuweke katika darja la wajawake wema ndani ya pepo yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…