Nimefanyiziwa na rafiki!!!!

Nimefanyiziwa na rafiki!!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Posts
6,157
Reaction score
4,454
Tumezaliwa kijiji kimoja, nimekuwa naye kijijini na nimesoma naye shule ya msingi, tuliachana tukiwa tunakwenda Secondary mpaka tunamaliza vyuo vikuu ambavyo tumesoma vyuo tofauti, tulikuwa tukionana pale kijijini mara chache sana wakati wa likizo mpaka tulipomaliza chuo.

Baada ya kumaliza chuo tulionana Dar katika mihangaiko ya kutafuta kazi, tulibahatika kupata kazi katika Taasisi mbili tofauti, yeye alipangiwa mkoani mimi nilipata nafasi hapa hapa Dar, ni zaidi ya miaka sita hatukuwahi kuonana face to face zaidi ya kuwasiliana kwa simu na kuchart kwenye mitandao.

Mwaka 2012 alihamishiwa kikazi hapa makao makuu ya Taasisi yao, kutokana na ukweli kwamba hapa mjini mambo ni mengi hivyo imekuwa ngumu sana kuonana mara kwa mara kwa masaa ya kutosha kiasi kwamba tunaweza tukastukiana kama kuna mabadiriko makubwa ya tabia baina yetu, tumekuwa tukionana mara chache sana tena sehemu za Starehe.

Mwezi July2012 alinishirikisha deal moja zuri sana lilikuwa la maslahi ya kutosha lakini, ilitakiwa nichangie kama Million15 ndani ya wiki moja, kutokana na hali yangu kifedha nilipigana sana ndani ya wiki hiyo ikaniwia ngumu kuikamata M15 hivyo nikalikosa lile deal nilisikitika sana.

Mwezi April 2013 miezi saba iliyopita ilikuwa ni jioni siku ya jumapili alinipigia simu kwamba yupo Mlimani City kuna transaction ya 2,500,000 anataka kuifanya amefanikiwa kutoa 800,000 lakini kadi imezama itabidi aifuate kesho yake asubuhi, akaniambia anahitaji hard Cash 1,700,000 za haraka haraka kama itawezekana vinginevyo atapata hasara kubwa, kiukweli ishu aliyoniambia ilikuwa ni lazima niamini, isitoshe ni mshkaji.

Kutokana na ukweli kwamba huwa ananisifia kwamba mimi ni 'ALWATANI' hapa mjini nililazimika kupambana ili ipatikane hiyo 1,700,000 nisimuangushe jioni hiyo hiyo japo mimi nilikuwa na 900,000 kwenye Akaunti yangu nikaongezea na 700,000 kutoka kwa mshkaji wangu aliye na duka pale Mwenge, then nikamkabizia.

Kesho yake asubuhi ya saa4 alinipigia simu kwamba wamepatwa na msiba wamefiwa na mfanyakazi mwenzao Ofisini yeye kateuliwa kuwa mmoja wa watu waliotakiwa kwenda Kilimanjaro kupeleka Maiti/Msiba, hivyo akadai akipata time atachomoka mara moja aende Benki arekebishe ule mzigo, siku hiyo hakufanya hivyo sikutaka kumsumbua sana nikasubiri arudi ila nikajitahidi kumalizana na mshikaji wangu wa dukani kwa kuhamishia deni kwa mtu mwingine, aliporudi toka Kilimanjaro akanishirikisha tatizo lingine, amekuwa akifanya hivyo kila ninapompigia huku akiniomba nimvumilie.

Siku zimekwenda miezi inakatika mpaka sasa nikimpigia simpati nahisi kani-Block, nikimpigia kwa simu nyingine anapokea lakini akistukia ni mimi ananikatia simu, hiki kitu kimekuwa kinanikera sana hakuna kitu kinachokera kama kukatiwa simu na mtu ambaye wewe unadhania ni rafiki yako.

Wadau nishaurini nimfanyeje huyu jamaa, ikumbukwe kwamba sina ushahidi kwamba kanidhulumu na kanisababishia usumbufu.
 
duh kikulacho kiko nguoni kwako jaribu kuendelea kumvumilia tu kama alivyokuambia ila taa ya hatari inakaribia kuwaka
 
Pole yako watu kama hao ndo wanafanya hata watu wengine wakiwa na shida washindwe kusaidiwa

manake na wewe nae ukajifanya ALWATAN haswa kwa kuitafuta hiyo pesa kumkopesha rafiki.....

Ofisin kwao hukujui....we nenda mvae face to face uone ye anaongea nini kama kwenye sim anakuzingua
 
kama unaweza lilipa lile deni , achana nae, kama bado make sure you get your money back,
 

Wadau nishaurini nimfanyeje huyu jamaa, ikumbukwe kwamba sina ushahidi kwamba kanidhulumu na kanisababishia usumbufu.

Mkuu kwanza pole, watu dizaini hiyo wanakera kweli yani!

Jiatahidi kutafuta evidence including transactions na maelezo ya mshkaji wako mwenye duka....Ukipata ushahidi wenye mashiko basi Alhamndulilah.

Kisha kwa sababu ni rafiki na jirani na kwa mbali kama ndugu. Mtafute mtu wa karibu yenu na kwa pamoja mumfuate mshikaji umweleze mwanzo mwisho usumbufu aliokusababishia. Kisha umpe deadline la kulipa kulingana na mtakavyoelewana.

Akishindwa fikisha kesi kwa wazazi/ndugu zenu huko kijijini. Ikishindikana nenda polisi na ushahidi wako kama akiweza kutiwa nguvuni basi tunamshukuru Mungu!
 
kaka si unajua ofisini kwakwe!! mtimbie hukohuko mkuu, hakika hatakubali kuibeba hyo aibu mbele ya staff wake/wenzake.....atafanyatu mambo akupe fedha yako.
 
Una uhakika bado yuko kwenye hiyo kazi mpaka sasa? manake hapa pananukia harufu ya utapeli!! huyu jamaa ni tapeli mzoefu.
 
Dah nashukuru Mungu hakukupiga ile deal ya kwanza maana. Muache tu usiharibu urafiki, inawezekana kakwama kweli. Fanya kama hiyo hela umeipoteza hivi
 
Back
Top Bottom