Nimefanikiwa kuacha uzinzi 2020

Nimefanikiwa kuacha uzinzi 2020

Wakuu nilitegemea faraja kutoka kwenu.
Niliamini mini nimewashirikisha jambo jema.

Tayari nimeshajieleza hapo juu kwamba sio kitu rahisi, Mungu lazima usimuache hata dk.

Kwa kifupi tu, mi nina kujinafasi ambako ukiamua kukatumia vibaya kanatosha kujipatia warembo kadiri ya hamu zako bila hata ya kutumia fedha.

Huwezi kuacha uzinzi bila nafsi yako kuanza kuchukia uzinzi.

Nafsi ikishachukia itaanza kukuhoji pale utakapo jaribu kuisaliti.

Vishawishi haviachi kukujia ila nikupambana na kumwomba Mungu akuepushie
Mtego wa uzinzi kuushinda inahitaji nguvu ya ziada..mapenzi hayana kiapo..na huu ugonjwa nao dah..hata hivyo kila la kheri ndugu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila shetani mjanja sana..yaani zile nyakati ndio umedhamiria kuacha uzinzi ndio anakutengenezea mazingira ya kukutana na watoto wakali..halafu mbaya zaidi beki hazikabi...dah sijui wana ulimbo gani..mwenyezi Mungu atunusuru aisee...🤔
 
Wewe umejaribu na umeshinda, ni mshindi
Acha kusikiliza hawa wakatisha tamaa na wanaokuletea vitisho vya rasharasha.
Yes uzinzi ni una nguvu ila will power ina nguvu kuliko uzinzi ukiamua kucontrol mwili wako unaweza tu, kifupi UMEWEZA hata kama ni siku umeweza, hakika utaweza.Heko zako.
 
Huyo pepo hatakiwi kutangaziwa vita, ni kama pombe. Ukisema naacha vile ambavyo vilishindikana ndo vinafunguka, ukute miss flani ulitamani maisha yako yote ndo anakukubalia. Haifai kabisa, bora ungenyamaza tu upambane kimyakimyA
 
Vizuri umeoa lasivyo ungeangukia chapuboys,

Ila Safi sana mkuu, jitahidi meli yako isizame mawimbi pamoja na upepo vimeshamiri.
 
Habari wana bodi.

Namshukuru Mungu kwa kunifikisha mwaka 2020. Namshukuru pia kwa wana JF wenzangu mlioteuliwa kutunukiwa afya kwa mara nyingine.

Nirejee kwenye mada.

Hakuna gereza gumu kutoka kama gereza la uzinzi. Bila nguvu ya ziada yaani nguvu ya ki Mungu huwezi kugundua hasara maana akili inafungwa.

Wengi wetu hasa wanaume ndio mabingwa wa uzinzi kwa kuchepuka. Bahati mbaya asilimia kubwa sie wanaume ni wachepukaji ila machoni mwa wake zetu hawafahamu am a wanafahamu sehemu ndogo tu juu ya yale tuyatendayo nyuma ya pazia.

Kifupi, wanaume niwepesi sana kuingia uzinzi kuliko inavyo zaniwa. Ni rahisi sana mwanaume kuzini na mwanamke wa hali ya ajabuajabu hata kumwaibisha mkewe.

Kifupi, nimedhamiria kwa roho moja kuachana na ushetani wa uzinziili kuwa mume na baba bora mwaka 2020.

Nimeamua kurudi kwa Mungu kwa dhamira ya dhati japo bado nakumbana na changamoto kubwa sana kiasi kwamba kama sio nguvu ya kiroho niliyoshikamama nayo kwa sasa.

Kwa kweli ni ngumu ila ukianza kujitafakari, kumtafakari mke,watoto akili inaanza kurudi kichwani.

Kabla ya hapo haingekuwa rahisi mimi kukaa siku 3 bila kupata mwanamke mpya bila kujali ni baamedi, changudoa, malaya wa mtaani, wafanyakazi wenzangu, wateja wangu nk.

Namshukuru Mungu aliniepusha na ukimwi katika hali ambayo sio rahisi kuelezea na kueleweka.

Baada ya kukaa chini na kujitafakari nilianza kujiona mwenye hatia.
Nilianza kuchukua hatua mwezi November, kukataa uzinzi. Mpaka sasa ni mwezi wa pili mfululizo Mungu kaniwezesha kuushinda uzinzi.

Nimeamua kujifungamanisha na ibada pamoja na kusoma vitabu vitakatifu, kukata mahusiano na wanawake niliokuwa na mahusiano nao, kuondoa marafiki wabaya lakini pia kufikiri kabla ya kutenda.

Nimeweka malengo nimalize mwaka huu bila uzinzi kutamkwa kwangu.

Eee Mungu nisaidie nitimize haya.

Bado muda kutangaza mafanikio, tuna siku 4 tu tulizomaliza mwaka huu bado siku 300 mbele. Subiri kwanza yawezekana ukafanya majanga mbeleni
 
Back
Top Bottom