Habari wana bodi.
Namshukuru Mungu kwa kunifikisha mwaka 2020. Namshukuru pia kwa wana JF wenzangu mlioteuliwa kutunukiwa afya kwa mara nyingine.
Nirejee kwenye mada.
Hakuna gereza gumu kutoka kama gereza la uzinzi. Bila nguvu ya ziada yaani nguvu ya ki Mungu huwezi kugundua hasara maana akili inafungwa.
Wengi wetu hasa wanaume ndio mabingwa wa uzinzi kwa kuchepuka. Bahati mbaya asilimia kubwa sie wanaume ni wachepukaji ila machoni mwa wake zetu hawafahamu am a wanafahamu sehemu ndogo tu juu ya yale tuyatendayo nyuma ya pazia.
Kifupi, wanaume niwepesi sana kuingia uzinzi kuliko inavyo zaniwa. Ni rahisi sana mwanaume kuzini na mwanamke wa hali ya ajabuajabu hata kumwaibisha mkewe.
Kifupi, nimedhamiria kwa roho moja kuachana na ushetani wa uzinziili kuwa mume na baba bora mwaka 2020.
Nimeamua kurudi kwa Mungu kwa dhamira ya dhati japo bado nakumbana na changamoto kubwa sana kiasi kwamba kama sio nguvu ya kiroho niliyoshikamama nayo kwa sasa.
Kwa kweli ni ngumu ila ukianza kujitafakari, kumtafakari mke,watoto akili inaanza kurudi kichwani.
Kabla ya hapo haingekuwa rahisi mimi kukaa siku 3 bila kupata mwanamke mpya bila kujali ni baamedi, changudoa, malaya wa mtaani, wafanyakazi wenzangu, wateja wangu nk.
Namshukuru Mungu aliniepusha na ukimwi katika hali ambayo sio rahisi kuelezea na kueleweka.
Baada ya kukaa chini na kujitafakari nilianza kujiona mwenye hatia.
Nilianza kuchukua hatua mwezi November, kukataa uzinzi. Mpaka sasa ni mwezi wa pili mfululizo Mungu kaniwezesha kuushinda uzinzi.
Nimeamua kujifungamanisha na ibada pamoja na kusoma vitabu vitakatifu, kukata mahusiano na wanawake niliokuwa na mahusiano nao, kuondoa marafiki wabaya lakini pia kufikiri kabla ya kutenda.
Nimeweka malengo nimalize mwaka huu bila uzinzi kutamkwa kwangu.
Eee Mungu nisaidie nitimize haya.