Ukweli pamoja na kwamba mtoa mada kadanganya, mii namuona huyo aliyedanganywa na akadanganyika ndo boya kabisa. Hizo ndo heza za ESCROW, ni halali uzile alafu jitoe kwenye hilo group. Haiji akilini hela ulizosotea kwa jasho lako unaona picha tuu unatuma hela hata hujaongea naye. Hizo hela za dezo.
Mimi kuna kipindi nilikuwa na room mate wangu tunasoma chuo fulani. Siku moja kaja room anajisifia kuwa kuna mtandao fulani kwenye internet jamaa kapata demu, basi akanieleza kila kitu. Kesho yake nikajisajili kwa jina la kike, nikaweka details zangu. Jamaa kaja ananiomba friendship nikamruhusu, nikamwambia mi nasoma chuo mwaka wa kwanza,. Akaniomba nijieleze shape yangu urefu na vitu vingine basi nikamuwekea sifa nzuuuuuri kama alivyo Lulu Michael.
Acha bwana jamaa usiku karudi anafurahi kama vile drogba kafunga goli kwenye fainali ya Champions League, akanisimulia kapata demu mwingine mzuriiiii. Nami nikajiunga kumsifia. Nikaendelea kuchat naye kama wiki hivi. Basi anajisifia, akanipa details zote. Kiukweli nilikuja kumdharau sana. Siku moja nikatibuana naye nikampa live kuwa alikuwa anachat na mimi. Daaah from that day urafiki wetu ukaisha