Nimechoka wizi wa TIGO

Nimechoka wizi wa TIGO

Acheni kupiga kelele kwa maneno ya mitaani.
Nenda ofisi ya Tigo iliyo jirani nawe;ili kupata majibu ya tatizo lako.
 
Acheni kupiga kelele kwa maneno ya mitaani.
Nenda ofisi ya Tigo iliyo jirani nawe;ili kupata majibu ya tatizo lako.

Huku kijijini hakuna ofisi ya Tigo ni mpaka mjini, ukipiga namba 100 hawapokei! ni tofauti na voda hupokea haraka!
 
dah md tigo wamenichosha
yaan hadi naandika hapa wamenichosha kweli
wajanja sana me nimezoea nanunua muda wa maongezi tigo prsa fasta fasta then najiunga na vifurushi vyao nafata process zote afu sasa nikijisahau kuangalia sms kama wamekuunga unakuja kushtukia baadae salio limeisha afu kumbe hawakukuunga. Au sometimes unaharaka unajiunga fasta umpigie mtu then wanakusms umejiunga but ukipiga unaambiwa salio halitoshi baada ya dk 5 hivi ndo system inakubali.


Yaani natamani kuhama
sema bahati yao tu ni kuwa chip yangu imekatwa then hapo hadi nikakate ya airtell ninayoitumia kwenye simu ya tochi then iliyokatwa ni renew basi hilo tu ndo linafanya nachelewa kufanya maamuzi.

Lakini siku yao ipo tu
 
Tigo wamezidi walikua wananikata kila mwezi 750 eti ya tigobima nkawapigia waniambie ni lini nimejiunga na hizo tigobima zao dada akajiumauma hana majibu,nkawa nanunua vifurushi moja kwa moja tigo pesa nkawa naweka cha wiki 3500 mb 200 sjui yaani eti siku moja mb kwisha nkaamua kuzima data baadhi ya application ambazo sio muhimu bado tatizo likaendelea nkaona isiwe shida nkawapigia hakuna clarifications za msingi nw nimewachokaaa nahama anytime natumia katigo pesa kangu kakiisha tu nawahama kabsa kwanza net slowwwwww inaboa ukiwa na mambo ya msingi unafanya usiitegemee kabsa utajuta bureeee....!!!!
 
wamekula 2000 yangu nikiwapigia wanasema hakuna taarifa zozote juu ya matumizi ya pesa yangu,wamenipiga chenga hadi nikakata tamaa,natamani wauone uzi huu,ukijiunga kifurushi ya 3500 siku mbili wanakwambia dakika zimekwisha wakati hata hujawapigia watu wengi,nimeamua kujiunga tu na kifurushi cha internet cha buku kwa wiki na si zaidi ya hiyo.
 
True mkuu kama data iko on lazima aliwe tu afu analalamika oooh tigo wezi

Nina uhakika na ninachokizungumza kaka siwez toka uko niache kaz zangu kuwasingizia....kwann isiwe voda????
Nimeweka vocha siku ya kwanza simu ikiwa dataoff wakakata yote....jana nimeweka buku sijapiga wala kutuma sms na dataoff yangu wakafyeka yoooote.....
 
chukuia hatua hamia TTCL, ukimlipa tigo unamlipa pia ttcl, ye ananunua TTCL kisha anakuuzia wewe, fanya kweli acha kulalama .
Kwa kwel mtandao wa tigo umeniudhiiii kiasi cha kufikiria kuvunja vunja line yao...
Wamekua wapuuzi sana...kila nikiweka salio wanakata....nikiweka jero wanakata.....inabak kama 200 ivi muda ule ule nikiuliza salio mara mbili wanaikata mpaka na io mia mbili...nikiweka tena vocha wanakata....sijakopa wala sijajiunga na huduma zao za kulipia.wiki nzima hii kila nkiweka vocha wanakata.
Napiga customer care toka jiz hawapokei simu......nimewachoka!!
Pia hata internet yao ipo very slow........am so tired kwakwel kesho nakopy majina kwenye laini nyingine nawahama....nimechoka....nasema tigo nimechoka na wizi wenu
 
Itakuwe mmeunganishwa automatically na kifurushi cha tigoliwa. Hawa tigo na wale voda wote uaminifu wao ni mdogo. Kwa mfano voda ukitaka kujiunga na kifurushi ikagoma labda kwa sababu zao, kisha ukajaribu tena ikagoma.pindi system yao ikikubali unaunganishwa na kifurushi hicho hicho mara zote ulizojaribu na utakatwa fedha mara zote!.
 
Tigo ni mashetwani kabisa nilisha tafuna line sasa nadunda na airtel. Ukiweka salio bila sababu eti umeunganishwa na bima, caller tune na facebook notification nitoeni hawataki dawa ni kuachana nao tu.
 
Tigo hawafai unajiunga na kifurushi kabla muda kuisha wanakula salio lote nashindwa kuelewa inakuaje

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom