Wahusika mtandao wa Tigo acheni wizi

Snipes

JF-Expert Member
Jul 2, 2013
9,109
16,681
Jana nimenunua vocha ya 1000 nikajiunga kifurushi cha MBs nikapewa na dk 5 ikiwa ni sehemu ya kifurushi. leo asubuhi nimetaka kujiunga kifurushi cha dk tupu ili niongee na watu wangu wameniambia sina salio la kutosha
nilivyoangalia salio nimekuta sh 216 kutoka ile sh 500 niliyobakisha jana
niliangalia salio la MBs nilikuta MBs za kutosha+zile dk 5

TATIZO LIKAJA HAPA SASA
nimewapigia huduma kwa wateja kutaka kujua hiyo sh 500 niliitumia vipi na katika huduma gani na malipo yakoje ya hyo huduma niliyotumia
walisema sijajiunga na huduma yeyote ya malipo ya baada(makato ya huduma)
nikahoji tena pesa imetumikaje kwa mara ya kwanza TIGO customer care wamenikatia simu.

Pia hii si mara ya kwanza kunifanyia kama hivi kuchukua pesa zangu kama hivi hawa Tigo. sh 500 ni pesa ndogo sana ikiwa mkononi ila ni nyingi sana ikiwa kwenye simu TIGO acheni wizi
 
Data hiyo boss. Always zima data usiku au unapoweka vocha. Usipozima data inakula tu. Hivi lini mtaelewa hili jamani.
kwahiyo wanaacha kula mb wanakula salio la kawaida
halafu mimi natumia data ninapohiitaji nikimaliza nazima
 
Ndo maana mi nimeacha kabisa kutumia internet ya Tigo, wezi sana. Kama unaweza hamia Airtel kwa matumizi ya internet. Huwa nanunua 1gb kwa 1000 , siku mbili natumia bila wasiwasi kwa matumizi madogo madogo.
 
Kuna sheria yoyote inayowalazimu kutumia huo mtandao? Mara kwa mara mnaleta thread za malalamiko humu jamvini.
 
Sio ww peke yako kaka kuhusu huu msiba wa kuibiwa vocha. Mm ck hiz nimeacha kabisa kuweka vocha halafu ikae tu kwny cm nikiweka hapo hapo najiunga yote ukiacha tu kidogo imekula kwako tgo wanaboa Sana. Na unakuta mtu hujajiunga na huduma yoyote ile ya kijinga kijinga naamaanisha coller tune
 
Wanatuchukulia Mabwegee Ukiweka Jero na ikikaa Nusu Saa Tuu 150 Haipo !
Wakifanya Hvi Kwa watu 1000 Washatufanya Zaidi Ya Mitaji [HASHTAG]#ShenzZaoo[/HASHTAG]
 
Tigo ni wa**ge sana wameniibia sana na nikiwapigia wanasema hauko kwenye huduma yoyote sasa yaan kila ukitia vocha baada ya muda kidogo 200 haipo wanatufanya mafala nshaachana nao
 
Hiyo imetokea mara nyingi hata kwangu na ww sio wa kwanza kulalamika na ukipiga cm majibu yao hayaeleweki
 
Data hiyo boss. Always zima data usiku au unapoweka vocha. Usipozima data inakula tu. Hivi lini mtaelewa hili jamani.

Hiyo siyo issue ya data mkuu kwasababu hata kwenye simu yangu ya nokia tochi wanakata pesa sana pasipo na sababu.
 
Data hiyo boss. Always zima data usiku au unapoweka vocha. Usipozima data inakula tu. Hivi lini mtaelewa hili jamani.
Msome mleta mada vizuri mkuu, anasema MB zipo, sasa iweje salio lake likatwe ziachwe MB?
 
Haya makampuni ya simu ni wezi hakuna mfano.
Yaani we weka salio kwenye simu kisha usiwashe data wala kufanya chochote..ukilikuta kamili baada ya masaa kadhaa katambikie.wanatabia ya kuwaunga wateja huduma za ajabu ajabu bila kijua au ridhaa yako..
Niliwapigia siku moja nikawaeleza ilo tatizo wakanieleza nimejiunga na huduma ya tigo hadithi...nikamjibu kuwa na adabu kijana yaani mi nijiunge na hadithi..haya basi tuseme kuna mtu alijiunga bila mimi kufahamu mbona sijawahi sikia au ona hizo hadithi zenu..akakosa majibu..
Yaani mitandao ya simu haswa TIGO ni wezi balaaa
..niko mbioni hamia halotel
 
Makampuni yote tu wezi mm nna voda na tigo lkn naona heri tigo kuliko voda
 
HiI mitandao ya simu mkuu nadhani ina mfumo wa wizi ambao uko sanctioned na management zao,vingenevyo wanavyopigiwa kelele management za makampuni hayo zingekuwa zimeshaingilia kati.Tigo na Voda ndio waliokubuhu kwenye mchezo huo.Airtel kidoogo afadhali.Yaani mimi inaniuma sana. Yaani jamaa wanachukua hela yako bila woga.TCRA nao kimyaa.

Back
Top Bottom