Nimechoka kusubiri ajira za walimu

Nimechoka kusubiri ajira za walimu

Shule kibao za private na bado unalia lia!!!
Hiyo private itakayonipa job la miezi miwili ipo wapii aisee niwatafute!.......

Maana si rahisi kuipata,...wote wanahitaji mkataba wa zaid ya hapo nishajaribu shule nyingi sana na hakuna hata mmoja alokubali kwa muda mfupi namna hii!.....

Na kama hakuna atayekubali kuajir mwalimu kwa miezi miwili basi ingekua vizur ukatengua kauli yako!.....

Unafikir kuna MTU anapenda kulialia!?....
 
UFAFANUZI.
1/Kama wewe ni mwalimu ujue una bahati kubwa sana ya kuja kuajiriwa na serikali. Wahitimu wa fani nyingine hawana hiyo bahati.

2/Ni jambo la kweli na uhakika kuwa serikali itaajiri walimu, Tatizo ni Lini wataajiri, wangapi wataajiriwa, wapi utapangiwa na utalipwa nini?

3/Upo uwezekano wa baadhi ya walimu wanaweza wasiajiriwe na serikali kama sio mwaka huu basi miaka michache ijayo. Kwanini? Serikali kwa sasa inaona watumishi wa umma ni wengi, ufanisi ni mdogo sana, gharama za kuwalipa ni kubwa sana. Kifupi kabisa serikali inaona wingi wa watumishi wa umma ni MZIGO na JIPU.

4/Mpaka sasa Serikali imeshasema kuwa haitawaajiri wahitimu wote wa Udaktari wa Binadamu. Kati ya madaktari zaidi ya 1000 waliohitimu Mafunzo ya Vitendo hivi karibuni, ni 400 tu ndio watakao bahatika kuajiriwa na serikali mwaka huu. Kwanini? Serikali haina pesa za kuwalipa wote.
Sasa jiulize suala la kuajiri walimu Elfu 40 kwa mkupuo mmoja kama linawezekana kirahisi rahisi mwaka huu?

5/Serikali imekuwa na vipaumbele vingi sana, na inataka vyote vitimizwe kwa wakati mmoja na hapo hapo mtizamo wa Rais kwa sasa ni kupunguza matumizi ya serikali na hapo hapo kukusanya mapato zaidi ili kujenga miundombinu na kununulia vifaa, na sio kuzifanyia matumizi ya kuwalipa watu Posho, mishahara mikubwa nk.
Katika hali hiyo, tegemea kabisa suala la kuajiri walimu litakuwa sio kipaumbele chake.

NI VYEMA UKIJIANDAA PIA KUISOMA NAMBA!!

kweli kabisa mkuu inabidi tuangalie upande wa pili wa kujiongeza ktk maisha
 
jambo usilolijua ni kama usiku wa giza msitulaumu sana ila tambua viongozi wa kiserikali wametusababishia psychological effect kwenye malengo yetu .mfano mimi niliuza kuku wangu 37 mwezi may mwanzoni nikiamin ajira zitatoka may na kuripoti juni.inaumiza sana unaposikia wameairisha
 
jambo usilolijua ni kama usiku wa giza msitulaumu sana ila tambua viongozi wa kiserikali wametusababishia psychological effect kwenye malengo yetu .mfano mimi niliuza kuku wangu 37 mwezi may mwanzoni nikiamin ajira zitatoka may na kuripoti juni.inaumiza sana unaposikia wameairisha
Mpaka mwezi wa nane. ....
 
Waalimu wananafasi ya kuajiriwa kwa sababu kila leo nchi bado inauhitaji kikubwa ni kuwa wavumilivu
Na ambao ni kama mimi tunaotarajia kusomea ualimu twendeni tukasome ili hatimae tuje tulikomboa taifa na vizazi vijavyo kutokana na ujinga
NINAJIVUNIA KWENDA KUSOMEA UALIMU KWA AJILI YA TAIFA LANGU
 
Na hata zikitoka hutokaa uendelee manake utapangiwa kijijini utakosa plan b na utabaki kusubiri mshahara kwa mwisho wa mwezi. Hii ni baada ya kugundua umeshindwa kujishughulisha na kitu chochote na kusubiri ajira ambayo kimsingi itakufanya masikini miaka nenda rudi
fudisha twisheni ww acha ujinga. nuu turubali weka pembe nne au omba shule uwe unafundisha huko madent
 
Jamani nimeshindwa kuelewa hesabu ya miezi miwili je ni mwezi wa sita na wasaba au wasaba na wanane maana ule waraka umeshindwa kuweka wazi ninamashaka na kauli za kisiasa zinazoendelea
 
Dah..... Inaumiza sana, bora watuambie cku rasmi ili mateso haya yapungue
 
Back
Top Bottom