Nimechelewa dakika 5 kwenye interview

Nimechelewa dakika 5 kwenye interview

Mie nakuombea uipate hii kazi, fundisho katika siku za usoni kama huifahamu ofisi itakayofanyika interview basi ni vizuri ukaenda kuitafuta siku mbili/tatu kabla ya interview ili kuepuka kuchelewa. Kila la heri.

kweli nimepata funzo.sitafanya hii mistake tena..
 
Ha ha haa sometimes the shit happen!
Hata mimi nakumbuka niliitwa interview na recr agent saa nne asubuhi. Basi niliwah kuamka nikajiandaa na hali ya hewa ilikua shwari tu that day. nikakalkuleti kutoka hapa nilipo mpaka posta kny intavyuu ni mwendo wa nusu saa tu plus nusu saa ya kusubiri na kujiweka fit room temp jumla lisaa limoja. basi ivofika mbili na nusu nikajongea kituoni. hatua mbili tu halahaulaa! Mua sijui wapi ilipotokea! Kama ujuavyotena siku ya intavyuu mtu unapojikip smart. Nkasema ngoja nijibanze ikate, Mwee lisaa lizima mvua haiachi. Nikacheki na bodaboda, Kumbe zilishakatazwa mjini! Daaah nikajitosa kwenye daladala foleni gani! Yani nilikua kama chizi. Mpaka nafika intavyuu rum saa tano badala ya nne. Nikadiskwalifai palepale thoo nilijitetea sanaa.
Iliniuma!

ee bana ee..hii yako noma hata afadhali mimi.najua how it feels.thank mkubwa for consoling me...
 
Ni ustaarabu kupiga simu kama dk 10 kabla kusema 'im running a bit late, but i will be there in say 15 minutes?'

inakera sana, watu wamekaa wangeweza kusoma emails ama walau kwenda kunywa chai ama toilet halafu hautokei. Unakuwa umewapotezea muda watu wengi.

kingasti i should have thought of that.I always observe time.but this particular day was just screwed up..
 
Usijali kuwa optimistic na utaupata. Anza kumwambia Mungu hata kama waliona kikwazo but kila mmoja wa panel aone ni wewe tu. Amini umeshapata. Let us cross our fingers.
 
Ukikosa usije ukajipa moyo kwamba ni kwa sababu ya kuchelewa..
 
Teh me yalinikuta nilienda wrong place ingawa ni kampuni moja,.. uzuri HR wa pale ilibidi ampigie hr husika aliyeenda kuinterview kuwa kuna watu wawili wamekuja ofisi yao nyingine, tukaelekezwa mahali husika good thing nilikuta zamu yangu bado maana HR alisema walisahau kuniambia muda siku wamenipigia simu hali iliyopelekea nikaenda sehemu tofauti, yule mwenzangu kwenye simu aliambiwa asubuhi akakuta zamu ake imepitaa though walimruhusu ila hawakumpa kazi.
 
pole sana ila usikate tamaa, ila nitakulaumu sana kama simu unayotumia ni smartphone au simu yoyote ambayo ina google map alafu ukapoteza muda mwingi kuzunguka au kuuliza watu wakati ramani unatembea nayo... ulimwengu wa sasa hata si wakuulizauliza hasa kwa sehemu zinazofahamika wakati location zipo kwa simu.
 
Kumbe ndio wewe niliokuelekeza siku ile!
Teh me yalinikuta nilienda wrong place ingawa ni kampuni moja,.. uzuri HR wa pale ilibidi ampigie hr husika aliyeenda kuinterview kuwa kuna watu wawili wamekuja ofisi yao nyingine, tukaelekezwa mahali husika good thing nilikuta zamu yangu bado maana HR alisema walisahau kuniambia muda siku wamenipigia simu hali iliyopelekea nikaenda sehemu tofauti, yule mwenzangu kwenye simu aliambiwa asubuhi akakuta zamu ake imepitaa though walimruhusu ila hawakumpa kazi.
 
Duh mkuu nakumbuka na mimi ilinikuta kuna shirika la wazungu flani waliniita kwenye usaili nikaamka mapema sana na nilitakiwa saa 3:00 asbh ile nataka kutoka mvua kubwa ikaanza nikapiga simu za madereva tax wote holaaaaa nikasogea kituo cha daladala nikapoteza muda mpaka napata bajaji ni saa 2:50 nafika eneo la tukio nimechelewa dakika 25 na jina langu limeitwa nikaomba nafasi kwa upole sana nikapewa,amini leo hii nafanya kazi na hao jamaa na kwenye usaili tulikua 43 nikapenya mwenyewe naamini utafanikiwa mkuu kama ulitulia kwenye kujibu maswali yao.
 
Mkuu ni kweli unachosema Muumba ndy kila kitu,ninakumbuka mm sikumaliza maswali ya interview ya practical na

nilimsumbua sana yule jamaa aliyekuwa anasimamia kwa kumuuliza maswali na tatizo lilikuwa mm sikuwa makini sana

vitu vinagoma halafu najifanya mtaalam namwambia setting zenu mmekosea mbona mambo yanagoma jamaa akija

anakuta kumbe nimekosea herufi moja hadi akaniambia kwa ukali "Hii mara ya mwisho ukinisumbua nakutoa" na

practical alikuwa anasahihisha yeye palepale lakini mwisho wa siku nikapata kazi,ningemaliza yale maswali ningetamba

ni ujanja wangu maana maswali yote yalikuwa yanatembea.

apo ndo uelewe kua kupata kazi sio ujanja wako..ni Mumba wetu ndio anaetoa rizki...Weka ahadi na Muumba wako ukipata kazi hii mshahara wa mwanzo baada kutoa mahitaji yako ya lazima utawapa watoto mayatima...au utafuta mtu masikini mtaani ili aanzishe japo mradi wa kuuza vitumbua...au maandazi...au kumnunulia mlemavu baiskeli ya maringi matatu....pia usimsahau kumfurahisha mama yako na baba yako mshahara wa mwanzo...kama wan uwezo wanunulie japo nguo mpya...kama ni masikini watengenezee chumba wanacholala.....
 
kama wamekupenda wanakuchukua no worries pray hard ila sasa next time, unatafura ofice zilipo kabla ya siku ya intaview, yaan hy siku ya intavyuu ni kuelekea tu mkuu..ila sio ishu, ka wamekuoenda utapata...
 
USIPANIKI kijana,
nakushauri kazi ya kutafuta mahali ofisi iliko ni siku moja au mbili kabla ya siku ya usaili.Siku ya usaili unatakiwa kufika pale dk5 kabla ili uwe na muda wa kuvuta pumzi
 
pole sana ila usikate tamaa, ila nitakulaumu sana kama simu unayotumia ni smartphone au simu yoyote ambayo ina google map alafu ukapoteza muda mwingi kuzunguka au kuuliza watu wakati ramani unatembea nayo... ulimwengu wa sasa hata si wakuulizauliza hasa kwa sehemu zinazofahamika wakati location zipo kwa simu.
Na mimi jinsi nisivyo muongeaji, huwa nawauliza google tu, ila sasa kuisoma hiyo ramani ni suala jingine kabisaa!
 
Mambo za kazi hizi! Majanki wananyanyasika sana!
 
Na mimi jinsi nisivyo muongeaji, huwa nawauliza google tu, ila sasa kuisoma hiyo ramani ni suala jingine kabisaa!

Sio issue sana kama sehemu inajulikana kwenye ramani ukishapata njia unaweka my location mshale unakuonyesha unakoelekea ukitembea nao una move.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom