Nimebakiza mafanikio katika mapenzi

scope17

Member
Mar 7, 2017
35
47
Habari wakuu,

Mimi ni kijana kimri, nimebahatika kupata mafanikio ya kimaisha katika umri huu, ninafanya biashara ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Nje ya mafanikio ya kifedha nina ndoto ya kupata mwenzi atakaye kuwa taa katika mafanikio yangu, mwenye mapenzi ya dhati na sio mapenzi ya pesa zangu.

Nimewahi kuwa na wapenzi zaidi ya wawili, wote niliachana nao baada ya kugundua kuwa hawakuwa na mimi kwa kunipenda mimi bali pesa.

Namtafuta atakayenipenda kweli niendeshe naye maisha asizidi 25 years.

Asanteni!
 
Kama hutaki apende hela zako basi muache hata mapenzi ayapende ya wengine mkuu
 
Umefanikiwaje kibiashara ndani na nje ya nchi ukashindwa jamvo hilo la kumpata mwenza unaeweza kuonana nae na kujua mapema tu kwamba anakupenda au la! Huku kwenye mtandao ndio umeona kimbilio? Wamejaa sana watafuta fursa huku. Chukua tahadhari.

Ila nna mashaka na ufanikiwaji wa biashara yako kwa mwendo huu.
 
ngoja kwanza nikuchane halafu nikupe baraka..

wanaume wengi wenye pesa mna kasumba kuwa mnapendewa pesa sasa mkuu baada ya kukupenda wewe unategemea upendo wangu kwako nisiufaidi... pesa unazo unataka utumie na nani kama si mpenzi wako?

acha uchoyo tumia pesa ikuzoeee
all the best
 
nadhani mtoa mada amewalenga wale ma Gold-diggers

wapo nae kumchuna tu, yaani wamemgeuza ATM. the moment akifilisika na wao mapenzi yameishia hapo.

kwa wale wataompenda yy kama yy basi ni haki yao kula asali.
 
Sasa mtoa mada mwenye anajivunia kuwa na pesa hlf anataka mwanamke asiye na pesa si ujinga huo..we ungesema vigezo vyako vingine hlf kwenye kugezo cha kazi ungesema mfanyabiashara...ngoja waje Pm wapenda pesa maana ndo uliowaita
 
Acha ubahili mkono wa kutoa ndo wa kupokea. Kama hutaki kutoa baki na pesa zako na genye zako. Hivi kumpa pesa mtu umpendae kuna shida gani?

Kwaiyo mkuu hiyo pesa unatengeneza ya nn? Wanaume wa aina yako ni rahisi kutoa kwa wadada poa ila gf hata mia hatoi.

Kila la kheri bania pesa zako benki tuone kama zitakuzalia mtoto.

Nb usinielewe vibaya kwa kukwambia ukweli.
 
ngoja kwanza nikuchane halafu nikupe baraka..

wanaume wengi wenye pesa mna kasumba kuwa mnapendewa pesa sasa mkuu baada ya kukupenda wewe unategemea upendo wangu kwako nisiufaidi... pesa unazo unataka utumie na nani kama si mpenzi wako?

acha uchoyo tumia pesa ikuzoeee
all the best
Kwanza nilijua lazima uonekane kwenye huu uzi, pili nilipokuona nikajua utakoment nini kabla ya kusoma komenti yako, tatu pia na mimi nikawa tayari nimepata cha kukoment hapohapo..!

Hivi unasema kwa upendo wako ina maana yeye atakuwa hakupendi au wewe unafikiri hisia zake zimeporwa na pesa aliyo nayo?? Pesa ni ziada katika mapenzi MONEY IS NOT EVERYTHING eboo..!
 
money is everything my dear
 
Kila la heri wapo ambao wanapenda kwa mapenzi ya kweli ila wanazidi kupungua kila kukicha. Ukimuonyesha wewe ngawira zimekupitia kushoto hatakuonyesha mapenzi ya kweli lakini ngoja ajue kama unazo, lakini si wote wako hivi ni baadhi tu ila kama nilivyosema idadi yao inaongezeka THANKS to mitandao.

Habari wakuu,

Mimi ni kijana kimri, nimebahatika kupata mafanikio ya kimaisha katika umri huu, ninafanya biashara ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Nje ya mafanikio ya kifedha nina ndoto ya kupata mwenzi atakaye kuwa taa katika mafanikio yangu, mwenye mapenzi ya dhati na sio mapenzi ya pesa zangu.

Nimewahi kuwa na wapenzi zaidi ya wawili, wote niliachana nao baada ya kugundua kuwa hawakuwa na mimi kwa kunipenda mimi bali pesa.

Namtafuta atakayenipenda kweli niendeshe naye maisha asizidi 25 years.

Asanteni!
 
Labda nikusaidie usichojua,,we umefanikiwa kuweka mikondo ya kupata pesa ila hujafanikiwa maisha,,,unaweza kua na hela nyingiiii lakin usiwe na mafanikio,na moja ya mafanikio ni kua na vingi visivyonunuliwa kwa pesa,,hapo ndio umefeli,,na umefeli moja kwa moja mpka kuja kuomba ushauri jf umefeli sana... Jitahidi zaid ufanikiwe maisha sio uwe unapata pesa tu
 
Back
Top Bottom