Nimeangusha pesa ya rambirambi 300,000/= cash mchana huu

Rudisha pesa za watu acha janja janja!

Wakuu, mchana huu mida ya saa saba nimeangusha Wallet ikiwa na pesa kiasi cha 300,000/= cash. Daaah, roho imeniuma sana aisee na haya maisha yalivyo magumu siku hizi.

Alafu ni mchango wa rambirambi ya msiba wa ndugu yetu aliyefariki kule Bagamoyo, watu 6 wamechangia ambapo kila mmoja alitoa 50,000/= na mimi nikiwa ni mmoja wao. Nikijiondoa mimi hapo ninabaki na deni la 250,000/=

Huu si ndio mwanzo wa kuonekana tapeli aisee? Wakuu, naombeni msaada wenu wa mawazo nifanyaje ili nirejeshe hizi pesa za watu?
 
Mkuu, mimi niliwahi kukataa ku-renew mkataba wa kazi wa mshahara wa 1.2m mwaka 2014 kwa sababu ya figisu katika kampuni ya wachina kisha nikarudi home kwenda kula ugali wa mama.
Ukarudisha mpira kwa golikipa??
Umetisha...
Sasa vitabu vya kijerumani huuzi tena??

Everyday is Saturday................................ :cool:
 
Back
Top Bottom