Ndugu zangu
Mimi mmoja kati ya wale vijana ambao niliapa kutooa single mother na pia ni muumini wa kataa ndoa ila sasa kama mnavojua usilolijua ni sawa na usiku wa giza katika pilikapilika nikakutana na huyu mdada mmoja tukaanzisha mahusiano kama kawaida ila siku zinavyozidi kwenda naona naona kabisa ana vigezo vyote vya kuitwa mke.
Huyu binti ni mzuri wa sura mpka shepu ana fanya kazi zake mwenyewe sio ombaomba kama hao wenu na ananionesha mapenzi ya dhati kabisa na kuniheshimu ila shida ni kuwa tayari ana mtoto, kizuri pia kwa first day namtongoza hakunificha aliniambia kabisa ana mtoto ila baba ake walishaachana wakati mtoto ana miezi 3,huyu dogo asaivi ana 6 yupo kwa bibi ake na huyo baba ake yupo kenya.
Kwa mapenzi anayonipa nafikiria kubadili mtazamo wangu wa kutooa single maza mi naoa huyu huyu maana hawa wengine shida tupu.
Nb;Huyu dada sio mtanzania ni mkenya wa mombasa.