Nimeamua sasa KUJIAJIRI tu YATOSHA!

Nimeamua sasa KUJIAJIRI tu YATOSHA!

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
380
Reaction score
534
Nilimaliza elimu yangu ya juu na kutunukiwa shahada ya KWANZA mwaka 2012. Tangu wakati huo nimekuwa nikifanya application NYINGI, mpaka sasa nimefikisha 289 application letters. Nimeitwa kufanya interview mara 12 kati ya hizo nimehudhuria 9 ambapo sijabahatika hata moja. Na Age yangu nayo inanikimbiza vibaya. Kwa kweli jamani NAOMBA USHAURI, nishaurini. Mimi ni mtoto wa mkulima na nilikuwa mkulima na mfugaji mzuri sana. kupitia shughuli hizi niliweza kujenga nyumba, kutunza mke na watoto na hata kujisomesha japo baadaye SERIKALI ilinisapoti kupitia bodi ya Mikopo. Baada ya kumaliza masomo nilijikuta nimemaliza mtaji wote wa kuendeleza shughuli zangu na sasa nimekuwa mtumwa wa kutafuta ajira ambazo hazipo, na kama zipo zinatolewa kwa rushwa, upendeleo, kujuana na vigezo vigumu. JE mawazo yangu ni sahihi? Na Hawa bodi ya Mkopo HSELB wanayo haki yakufuatilia huko shambani?
 
Wewe jiajili tu hao HELSEB hawatokupata labda ukitaka kusafiri nje ya nchi au kuajiriwa hapo ndo watakupata
 
Unachelewa kaka, mwanaume huwa hasuisui! Wewe unasema mpaka shamba unalo halafu unalialia ajira? nenda kalime, hiyo elimu itakuwa imekufungua vya kutosha ukikakamaa ni miaka miwili tu utaajiri na wenzako. Maisha ni medani, elimu ni moja tu kati ya siraha, karibu ulimwenguniw enzio tunajikwaa tunainuka tunasonga..:boxing:
 
Hayo ndo maamuz ya msing kwa sasa, ni wazo zuri endlea nalo. Wenzako toka 2010 juhud na maisha yanaendlea.
 
Elimu ya kibongo majanga , jamaa kajenga nyumba, katunza familia ,kajisomesha kwa kazi ya shamba, kamaliza shule na mtaji umekwisha dah.
 
Back
Top Bottom