Nimeamua niache kazi nikajiajiri

Acha kujitafutia shida. Huki sio kipindi kizuri cha kujiajiri. Utakuja kupata magonjwa ya moyo bure. Sasa kama elimu yako mbuzi kwa nini usitumwe tumwe? Kama hupendi kutumwa kaongeze elimu...
Acha kudharau binadamu wenzio!kauli zako tu zinaakisi ujinga ulionao,nani kakudanganya kuwa watu wenye credencials ndio wanaofanikiwa?matajiri wakubwa wa nchi yako hakuna hata mmoja mwenye PHD.
 
Acha kudharau binadamu wenzio!kauli zako tu zinaakisi ujinga ulionao,nani kakudanganya kuwa watu wenye credencials ndio wanaofanikiwa?matajiri wakubwa wa nchi yako hakuna hata mmoja mwenye PHD.
We kunguni! Unapata wapi ujasiri wa kunitusi? Watoto kama nyie ambao hamjui kuwa kuna wakubwa wenu ndio mnaoshia kuwa mzigo kwa taifa. Ni kwa sababu ya watu kama wewe ndio maana taifa hili haliendelei.
 
Umasikini mkubwa kuliko wote ni umaskini wa akili na fikra........

Mwanadamu anaanza kufa akili ndio unafuata mwili.....

Kichwa ni maktaba na hekalu la fikra mbali mbali........

Mtu mwenye kuitumia akili yake vyema....anakuwa na mawazo mazuri na yenye tija......

Mtu wa hivyo.....hata ukimpa shilingi elfu kumi....baada ya muda anaweza kuifanya kuwa laki moja........

Lakini mtu asiye na fikra na mawazo yakinifu hata ukimpa bilioni moja....bado kwake haitatosha.......

Think big
Take control of your destiny
Barikiwa.
 
Habari zenu wanajamvi,

Mwenzenu nimeamua niache kazi niliyoajiriwa nikajiajiri mwenyewe kutokana na sababu kubwa moja ya kutopenda kutumwa yani nikitumwa nachukia pia wafanyakazi wenzangu wananikera muda mwingi halafu mshahara ni mdogo sana.

Naomba mnijuze changamoto za kujiajiri, pia nina mtaji wa laki tano sasa ni biashara gani naweza kuanza nayo.
Asanteni
Kujiajiri its not as simple as your thinking, lazima uwe umeanzisha kiji-project ambacho utahakikisha kina-run parallel na kazi yako ya kuajiriwa uliyonayo, sasa ukiona ka-project kanaleta walau 80% ya basic needs zako na unahisi kanahitaji sasa usimamizi wako ili kaweze kufikia 100% hapo sasa unaweza ku-shift.

Vinginevyo watu mliozoea mishahara hamna Technics za huku mtaani kwetu - utaadhirika - jipange kwanza.

Kwa Laki tano ulizonazo kazi zinaweza kukufaa kuanzisha project kati ya hizi zifuatazo:
1. kuuza vocha
2. kufungua genge la mboga-mboga
3. Mama nitilie
4. Juice ya miwa kwenye busy street
 
Tengeneza kipato cha Ziada Kwa kupata kitabu maalumu kitakacho kufanya ujue kutengeneza bidhaa mbali mbali muhimu za viwamdani nyumbani kwako na uweze kujiajiri. Kitabu hicho utakipata Kwa bei ya TSh.5,000 tu! Katika email au whatsup yako. Ni Pigie au whatsup 0762208190 AU 0718978295. Utachagua unacho taka kujiajiri kitaalam kupitia kitabu hicho.
 
Uamuzi mzuri mkuu cha msingi fuatilia ni biashara gani unaweza kumudu kuifanya na fuatilia eneo zuri kwa biashara. Katika yote usikate tamaa na tambua kuwa hasara ni sehemu ya biashara
 
Back
Top Bottom