Nimeamua niache kazi nikajiajiri

Tuchki

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
1,740
1,441
Habari zenu wanajamvi,

Mwenzenu nimeamua niache kazi niliyoajiriwa nikajiajiri mwenyewe kutokana na sababu kubwa moja ya kutopenda kutumwa yani nikitumwa nachukia pia wafanyakazi wenzangu wananikera muda mwingi halafu mshahara ni mdogo sana.

Naomba mnijuze changamoto za kujiajiri, pia nina mtaji wa laki tano sasa ni biashara gani naweza kuanza nayo.
Asanteni
 
habari zenu wanajamvi.Mwenzenu nimeamua niache kazi niliyoajiriwa nikajiajiri mwenyewe kutokana na sababu kubwa moja ya kutopenda kutumwa yani nikitumwa nachukia pia wafanyakazi wenzangu wananikera muda mwingi halafu mshahara ni mdogo sana naomba mnijuze changamoto za kujiajiri, pia nina mtaji wa laki tano sasa ni biashara gani naweza kuanza nayo
asanteni
Nakupongeza sana. Umetoka kwenye utumwa. Mwanzoni utapata misukosuko na changamoto mbalimbali lakini ndo kusimama huko. Mtangulize Mungu utafanikiwa. Kuna siku utaajiri pia.
 
habari zenu wanajamvi.Mwenzenu nimeamua niache kazi niliyoajiriwa nikajiajiri mwenyewe kutokana na sababu kubwa moja ya kutopenda kutumwa yani nikitumwa nachukia pia wafanyakazi wenzangu wananikera muda mwingi halafu mshahara ni mdogo sana naomba mnijuze changamoto za kujiajiri, pia nina mtaji wa laki tano sasa ni biashara gani naweza kuanza nayo
asanteni
kama upo serious njoo inbox
 
Unatoka kwenye utumwa unaingia kwenye kujituma mwenyewe.....ili uyaone mafanikio unatakiwa ujitume kuliko hata ulivyokuwa ukitumwa mwanzo..........

Mimi huwa namheshimu mtu anayeuza karanga zake barabarani kuliko hata mkurugenzi wa ofisini.....
 
Umewaza kujiengua zama za kubana matumizi.... Pesa mtaani hakuna biashara zinatukatisha tamaa...... Anyway biashara haikosi changamoto..... Ujuzi wako na kujituma kwako ndio njia ya mafanikio yako..... Biashara hutegemea uhitaji/demand ya eneo husika..... Wahitaji ndio watakushawishi uwauzie nini .....Kila la kheri ktk maamuzi yako kuyaendea mafanikio yako.
 
Back
Top Bottom