Nimeamua kwenda Arusha kutafuta maisha

Nimeamua kwenda Arusha kutafuta maisha

Mungu akutangulie mkuu! A-Town utatoka faster kama ni mtu wa kazi! Napapenda sana A-Town!
 
Hapa Dar hakuna kusaidiana, ni mkono kwa mkono! Kama huna pesa mtoe sadaka hata mkeo agegedwe upewe mchongo! MSINGI KIUNO! Ni laana tupu hapa!
 
Nenda mwaya Mungu hatakucha dar jiji la wenyewe wakujuana ukitoka familia duni dar lazima utachina .
 
If YoU dOnT makE iT iN dAresSalAaM YouWoNt makE it In RcHugAaa. NendaMkoA mWinGine ila Sio cHuGaaa AriFuuuu

Mkuu Keyboard Yako Bado Ipo Matengenezoni au? Nimesoma Post Yako Na Sasa Natafuta Dawa Ya Kuondoa Kizunguzungu.
 
PM me! Karibu Sana! If what you say you mean you will surely succeed! But you need strategy!

Baada ya kukosa kazi ya kuniingizia kipato kwa hapa Dsm… na baada ya kupewa ahadi ya kusaidiwa namna ya kujikwamua kimaisha kuwa isiyotimilika…
Nimeamua kulikimbia Jiji la Dsm na kwenda Arusha.
Huko simjui mtu,sina ndugu wala mjomba. Naenda kupambana na hali yake. Labda kuishi Dar mda mrefu naona hakuna fursa kwangu tena! Lakini pia kuna labda kazi ambazo kwa hapa Dar zinaonekana siyo ila kwa Arusha na nje ya Dar zinaweza kuonekana ndiyo za maana! Vyote hivyo naviona akilini mwangu…
Kama nimepotea,potelea mbali! Ila namwomba Mungu anitangulie katika hili. Maisha ni magumu saana!
Wakazi wa Arusha,na viunga vyake,tengeru,moshono,kia,na Mererani nawaomba mnipokee aisee!! Nimekuja arusha kutafuta maisha. Ni hayo tu!
 
nenda mtwara utapata tu ikishindikana anza na kufundisha bila shaka utatoka tu.arusha ni kama dsm kuna competition kubwa sana

I real support you broda...namshauri jamaa aende Mtwara kama ana kaelimu au fani flani atatokelezea tu...hata kama ataamua aanze na restaurant au kuchoma chips...avizievizie pande za bandarini, dangote au makampuni mengine ya kigeni,fursa kibaaaaoooo!
 
Aisee njoo Tanga babaangu, huku maisha poaaaaaa
 
karibu chuga kaka unaweza toka cuz dar ni kutafuta pesa ya baba mwenye nyumba tu labda wale wenye kazi nzur
 
Chaliii wangu....ukija chugaa acha mambo yako ya kidasilamaa chalinze,huku ni ngumu nyeusi.kuna harakati kibao,mishe kibao,sio lazima kuajiriwa...kama kiniaje[kimombo]kinapanda unaweza kuwa fly catcher na mkwanja ukapata mwingi tu haiitaji lesheni.kuna potaa kupanda ma maunteniii kili nguvu zako tu na pesa unapata,achana na mererani maana sahii mawee hakuna utafukuzia moto kibao upati hata gonga kwa sasa.kama unaujuzi unaweza kujimix na machali wakakufundisha kushona cultural za viatu,kofia,masendo na kuuza kwa matashaa mkwanja njenje....judi zako ndo mafanikio yako,epuka makundi ya wavuta poda,wacheza kamari,wapenda bata maana huku mi bisuuu njenje.ukizingua cha mbavu
 
Duuhh!! Mkuu ameongea point, ila kiswahili chako kimeniacha hoi…

Mererani nishatoka muda huko… mawe hamna hata kidogo, kila siku ni moto tu ila ni empty…
 
Kumbe maisha yanalimwa Arusha...nitakuja na mimi kuyachukua nirudi nayo mjini!
 
Sikiliza kijana inaonekana wewe ni mvivu na unachagua shughuli au ulilelewa kimayai.Ulishindwa kupata elfu kumi na tano na kuanza kuzunguusha hata karanga za kuchemsha? Au hata kwnda kwenye masoko kuangalia watu wanajifunzaje biashara kwa mfano mitumba na kuanza hata kuuza kwa mali kauli? Kama unapenda starehe, na kupenda kulakula hilo ni tatizo kwa asiye na chochote.Pia jifunze kuishi Kihindi mnaweza hata kukaa chumba cha geto watu wawili,kila unapouza kidogo unaweka hela mpsa au tigopesa.Pia uskidharau kilimo au ufugaji baadaye.Na pia usipende kutegemea network au kubebwa.Tumia ubongo wako na nguvu zako!
 
Duuhh!! Mkuu ameongea point, ila kiswahili chako kimeniacha hoi…

Mererani nishatoka muda huko… mawe hamna hata kidogo, kila siku ni moto tu ila ni empty…

mkuu hii kiswaili arifuu ningeli ya chugaa...yani iko damuni eroo,hapa kuandika je ukiniskia stkupoteza hutanisoma chaliwangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom