Habari zenu wana jamvi,
Leo nimeamua kuvunja ukimya, nasema ukweli jamani ndugu zangu YESU ni mtamu, acheni nilewe huyu YESU mie. Yeye ni jana leo na hata mileleeee mwanzo na mwisho.
Hakuna kama yeye chini ya jua na kwingine kokote. Ni huyu Yesu aliyenipa elimu baada ya kufeli kwa mara ya kwanza form 4 na kukata tamaa kabisa, ni huyu Yesu, alinionesha njia hadi leo nina CV ya ukweli.
Ni yeye huyu aliyenipa kazi kwa muda mfupi tu baada ya kuhitimu masomo bila ujanja wowote ila kwa MAOMBI tu, ni yeye huyu aliyesimama na mimi pale kazini kupingana nao wale wote walionionyesha chuki na kunitengenezea mazingira ya mimi kufukuzwa kutokana na wivu wa elimu,.
Ni huyu YESU aliyempigania baba yangu kwa miaka 17 sasa akipita katik ajaribu lile.Ni huyu aliyenipa uzima hadi sasa naishi. Any way natamani na wewe umjue huyu MWANAUME ambaye;-
1. Sio msaliti
2. Mwaminifu 100%
3. Rafiki wa kweli nyakati zote
4. Mtimiza ahadi
5. Aliyeyashika maisha yako mkononi mwake
6. nk;
Jamani ndugu zangu tumwamini Yesu, dunia imeshatuchoka na hivyo inataka kututema tu, sasa sijui itakutema wapi, ni wakati wetu vijana tuamke na KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WETU. AMEEN.
GOD BE WITH YOU
Horse nina maombi maalumu ya binafsi ndani ya mwezi huu, naanza tarehe moja I will mention you evrday
aisee....anafaidii....:confused2::confused2:Ya namtolea vyote mkuu, nimejiachia kwake
sifa gani mkuu?, unataka maandiko? Ebu toa mfano sifa gani? Maana hapo nilitoa maelezo unataka maandiko gani?
Excellent answer! God bless you.Maswali mazuri sana, nimependa - ila natamani ningekuwa nakuelezea ana kwa ana ingefaa sana maana kuna vitu vingine ni vyema kuvielezea live. Ok nitajaribu kuweka kwa ufupi ili usichoke sana. -
Kwanza kwa haya maswali napata kuhisi kwamba wewe ni mchanga sana ktk masuala ya imani au labda ni muislamu tu, ila si ishu sana.
1. Tambua kwamba niliokoka tangu form 1 na nimekua mtumishi wa Bwana tangu hapo kupitia CASFETA, hivyo nilipomaliza form 4 mara ya kwanza nilifeli na wengine wengi walifaulu. Je hapo Yesu alinisahau? - jibu ni hapana ila alitaka ajitukuze kupitia mimi, nililia nikamwambia Yesu nimekutumikia kipindi chote cha masomo, y this? nilikata tamaa sana, nikarudia mitihani huku YESU nikimuomba kwa hali ya juu aniwezeshe> - MAOMBI
2. Yesu sio mbaguzi na wala si kwamba hao unaowafahamu Yesu amewaacha NO, - Isaya 43:26 inasema "Unikumbushe na tuhojiane eleza mambo yako upate kupewa haki yako" - MAOMBI, wapendwa wengi hawaombi, hawafungi, wakiambiwa njoo kuna mkesha tumuombe Mungu mtu haji, lakini ktk harusi hadi sa 9 usiku anaenda.- MAOMBI MAOMBI MAOMBI hili ndio tatizo, na hapa ndipo shetani ametushika sana, TUNAPASWA KUAMUA KUKAA KTK MAOMBI, - SIJISIFU, NILIAMUA KWA DHATI KUOMBA MUNGU, na ndio maana ameonekana,
Naamka usiku saa 9 hadi kumi naomba, usingizi ninao lakini nasema hapana YESU amesema nijaribuni muone - nikadhamilia kumjaribu, Nafunga peke yangu, nyumbani wanaleta kuku na vitu vingine vizuri, nafsi inashawishika kufungulia lakini nasema hapana hadi nimalize maombi jioni.
Kuomba ni mzigo mzito, wengi wanomba wakiwa wamekaa chini matokeo yake ni kusinzia tu, Niliamua kuomba kwa kusimama hadi leo nina uwezo wa kusimama hadi masaa 4 naomba tu huku natembea, na maneno hayajirudii, - MAOMBI MAOMBI, na KUJITAHIDI KUIKIMBIA DHAMBI + MAOMBI TUTASHINDA.
3. Hata ikitokea nimefukuzwa kazi sasa hivi, YESU bado ni wangu tu, hiyo ni sehemu ya majaribu ya kupimwa imani yangu, sitaaacha kamwe.
Nb: Ningekuwa na wewe ana kwa ana ingependeza sana
Ila angalia, mvumilivu ndio hula mbivu. Waweza chelewesha muujiza wako kama Abraham alivyochelewesha kwa kuzini na mjakazi kwanza.Thanks indeed! Mithali 18:22 Apataye mke apata kitu chema ;naye ajipatia kibali kwa Bwana. Kwa hiyo mtumishi please! moyo wangu sio mgumu kihivyo avatar yangu isikutishe!
Wanasema unavyoomba Mungu anafanya vitu 2
1. Kushughulikia ombi lako, lkn pia
2. Kushughulika na wewe.
So kwenye shida ni kushughulika na wewe, maana kutokana na kufuata njia zetu mara nyingi tunachelewesha kujibiwa maombi yetu.
Maana ni lazima ahakikishe kuwa tukipata hicho tunachokiomba
1. Hatutajidhuru nacho
2. Hatutamsahau yeye na kukitukuza hicho
3. Hatutajikweza na kudharau wengine
4. Kwamba kitakuwa kwa ustawi wa wengi
JF bana raha sana, kila kitu kimo...........
Leo naona mmeamua kututwanga mneno, ila safi sana!
Ila angalia, mvumilivu ndio hula mbivu. Waweza chelewesha muujiza wako kama Abraham alivyochelewesha kwa kuzini na mjakazi kwanza.
Leave all to God and as sure as his WORD atatenda
Hapa sijui niseme Amen ama niseme shindwa!
Hahahah naona na wewe umeamua kuwa mpole maana malumbano na kutwangwa verses vingekutoa knock out
Umeona eeh!!! we mjanja umenisoma vizuri kumbeee!!!
Hahahah,sema Amen to the word of God halafu mwambie shindwa huyo shetani anayekuja na logic argument za "utauziwaje mbuzi kwenye gunia bwana, kulaneni ili mjue what you are getting into".
Kama vile Yesu alivyomwambia 'Petro' "ondoka kwangu Shetani..." pale Petro aliposema over his dead body kwamba Yesu angesulubiwa na kufa msalabani
Ila biblia bana ina makavu si mchezo embu cheki hapa
[h=1]Yohana 8:44[/h]''Ninyi ni watoto wa baba yenu shetani; kwa hiyo mnapenda kufanya maovu kama yeye. Tangu mwanzo yeye alikuwa muuaji na hana uhusiano wo wote na mambo ya kweli; kwa maana hana asili ya kusema lililo kweli. Shetani anapodanga nya anadhihirisha asili yake kwa kuwa yeye ni mwongo na ni baba wa uongo''