ALWATAN KIZIGO
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 539
- 642
Habari wana bodi,
Mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa waumini wa kufunga ndoa duniani.Nilikua nikimuona mtu anaoa nilikua namsikitikia sana na kumuona kapotea maboya.Lakini baada ya kuishi maisha ya uboyfriend &girlfriend kwa muda mrefu tangu balehe nimeona sipati maendeleo yoyote zaidi ya kutumia pesa nyingi kwenye viwanja kutanua na wasichana mbali mbali niliokuwa nao.
Hii kitu imenirudisha sana nyuma kimaendeleo maana nilikua nikitola na beby tunaenda viwanja kutumia na huko kukata laki 3 kwa siku ilikua kawaida sana.Sasa kwa mwezi tukitoka mitoko mi 5 maana yake nilikua nachoma milion 1.5 kwenye starehe na gal wangu huku nina majukumu mengine kama kusomesha wadogo zangu nk.
Kitu nilichokuja kugundua kumbe ukioa mwanamke ukaweka ndani gharama kama hizo unazipunguza na unazielekeza kwenye maswala ya msingi wewe na mkeo kwa ajili ya maisha ya baadae na vizazi vyenu.
Mke hana ghrama haswa kama anafanya kazi maana mkitenga laki mbili mkienda soko la Tandale mnanunua chakula cha kutosha mwezi mzima tofauti na angekua hujamuoa mngeenda kuzichoma pale KFC kwenye kuku.
Nahitimisha kwa kusema kutunza girlfriend ni ghrama kuliko kutunza mke.
Asanteni