Nimeamua kumuacha mke wangu……………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeamua kumuacha mke wangu……………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jan 17, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni takriban miezi miwili sasa mgogoro huu umekuwa ukifukuta chini kwa chini na sasa imefikia mahali humu ndani hapakaliki wala hapaliki, ilimradi tafrani kila kitu vululu vululu. Nimelinyamazia jambo hili lakini sasa nimeamua kumuacha mke wangu mama Ngina ili roho yangu ipate kutulia.

  Ni miaka mitatu sasa imepita mke wangu hajaenda kuwaona wazazi wake huko kijijini, na hiyo ilitokana na majukumu ya kibiashara anayoiendesha, nakumbuka mwanzoni mwa mwezi wa sita tulikubaliana itakapofika mwezi wa kumi mwaka jana aende kuwaona wazazi wake lakini ilibidi tuiahirishe safari hiyo kutokana na mimi kupata ajali na kulazwa hospitalini. Lakini tangu nipone na kurejea kazini mwenzangu kanibadilikia anataka kwenda kuwaona wazazi wake kwa sababu amewa-miss sana.

  Nilikuwa nimepanga aende mwishoni mwa mwaka huu kwa sababu alilazimika kufunga biashara kwa takriban miezi miwili akiniuguza, na tangu afungue hajakaa hata miezi miwili na sasa anataka kufunga tena asafiri. Swala hilo limekuwa likizua manung’uniko na sasa imekuwa nongwa kila nikirudi nyumbani jioni hakuna maelewano na anachotaka ni kusafiri ili akawaone wazazi wake.

  Sasa nimeona bora yeshe, nimruhusu aende kuwaona wazazi wake akae huko kwa mwezi mmoja mpaka hamu yake iishe ndipo arejee, lakini kakataa anataka akakae wiki moja tu ndipo arudi kwani hayupo tayari kuniacha peke yangu kwa muda wote huo ikizingatiwa bado sijapona vizuri na ninahitaji ukaribu wake. Nimeona isiwe tabu tumeafikiana na sasa anajiandaa kwa safari wiki ijayo Mwenye enzi Mungu akipenda atasafiri, na mimi nitabaki nyumbani na wanangu Ngina, Ngano na Ngadu. Muombeeni mama yenu, wifi yenu au shemeji yenu safari njema……………………….LOL
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mtambuzi nimeipenda sana heading, lakini muda huu nafuatilia kuagwa kwa mpendwa wetu, nitacomment jioni!
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kichwa cha habari kama gazeti la udaku vile. . . Lolz

  Nwy mtakie safari njema, awarudie na zawadi toka kijijini.
   
 4. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  Ni vizuri ulivyoamua kumuacha mke wako aende kuwaona wazazi na kurudi baada ya wiki moja hakuna sijaona sababu ya msingi hapo ya kumzuia kwenda kuwaona wazazi, hizo biashara zipo tu na zitaendelea kuwepo kutafuta pesa hakuna mwisho. Labda kama unalako jambo zaidi ya ulioandika. NAMTAKIA SAFARI NJEMA, AENDE NA KURUDI SALAMA BAADA YA WIKI MOJA.
   
 5. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  lol..................yan io headin mtambuz duh! nilikuwa nawasubiri kina canta na king waje wakushambulie hapa mmh.
  nami namtakia mama ngina safari njema.
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kumbeee....umemtarifu bibi wa nyumba ndogo kama utawala ni wake sasa :)
   
 7. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Heshima yako baba,
  Dah hiyo heading imenistua nikampigia mama kabla sijasoma akawa hapokei na uzi ukawa umeshafunguka lol!
  Sijui ingekuwaje kwa nilichokuwa nimepanga kumuuliza,
  Poa tunamtakia mama safari njema,na mungu ampeleke salama na amrudishe salama.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ngina,NGANO
  NGADU,hahahahah
  i lyk the namez
   
 9. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,388
  Likes Received: 726
  Trophy Points: 280
  imeaandikwa mwanamume atawaacha wazazi wake naye ataambatana na mkewe watakuwa mwili mmoja.....
  sasa hapa kuna vitu vya kuvikubali kwanza (hii kwa uelewa wangu) inamaana mwanamke yeye haachi wazazi wake hivyo lazima aende maandiko hayajamfunga lakini la pili ni kwamba sielewe vizuri mkiwaacha wazazi ukiambatana na mkeo inamaana unaenda kwao hivyo nenda naye ka vipi kwa sababu maandiko hayakutoa mnaaenda wapi
  lakin katka hali ya kawaida ni vizuri akaenda likizo ni siku nyingi akirudi atakuwa na akili mpya na mawazo mapya kuliko ukin'gangania akae hapo (japo kwa shida na raha) vumilia m2 wangu
   
 10. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Babu turudishie chenji zetu bana..!!!!lol!!
   
 11. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Duuu isipokuwa makini huwezi kuelewa kinachoongelewa hapa maana kichwa cha hbr ni kizito ...okay twamtakia safari njema.
   
 12. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Huyu mdingi wetu sometimes mtata sana1
  Mie mwenyewe niliposoma heading nikajua labda yule dada glady aliyemchungulia siku zile kesha muweka dingi yetu mtu kati lol!
   
 13. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  baba ngina,uandishi wako umejaa suspense. Safiri salama mama ngano
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Umefanya uamuzi sahihi, Hongera kwa kuvua gamba.
   
 15. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kichwa cha habari kiliniudhi sana kabla sijaisoma hii habari. Maana sipendi mtu anayezungumzia kuacha mke. Lakini baada ya kuisoma habari nimekuelewa. Mungu ampe shemeji ulinzi wake wakati woote wa safari. Ameni
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Unajua hiyo safari sikuipenda kwa sababu sipendi mke wangu akae mbali na mimi hata kwa siku moja, na ndio sababu sikutafakari hata kichwa cha habari kiweje................ hata hivyo nimeona umeelewa
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Sijajivua gamba bana, usipotoshe habari
   
 18. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Anko umefanya la mana sana kumuachia aende kuwaona wazee,siunajua sie wanawake lazima ukamuone Baa na Maa ndio roho itulie....
  ulimpa mwezi ulikua ume nuna au?
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huu uandishi ni kipaji cha Mnyaazimungu kanijaalia, na ndio maana mkinisoma huwa mnaburudika.............
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa natishia Nyau, akikaa mwezi si nitazimia..............He! mwezi bila naniliu!
   
Loading...