Nimeamua kugive up lakini naumia....

Huyu ni GF wakati Wa kuoa ukifika kumbuka kutafuta mke!


QUOTE=First Born;4374770]Yalikuwa mapenzi ya dhati toka moyoni Mwangu na nilitamani kila mtu ajue nilizimika kwa Mtoto Sophy! Sikutaka nimuudhi kwa namna yoyote ile!
Nilipomkosea sikujivuta.. Nilimwangukia na kumuomba msamaha! Sikujali kuwa yeye ni just form four leaver ambae hata kwenye mtihani hakufanya vizuri, ckujali elimu yangu pamoja na uanaume wangu! Sikuwahi kwenda kwake mikono mitupu, Mara juice ghali, Mara chipsi, Mara nguo, kuku, voucher na vitu kibao ili ajue kuwa nilimpenda ingawa yeye hakuwahi kininunulia hata pipi!
Akikosea hakuwa mrahisi Wa kuniomba msamaha hadi nimwambie afanye hivyo kwa lazima! Sikuogopa hata kumpa mamaangu aongee nae kwenye simu!
Dahhhh! Hakujali,
Nilimwambia mwenendo Wa mahusiano yangu ya awali lakini nikimuuliza alidai sikuwa chanzo cha wao kuachanaso hainihusu!!!

Kwa kweli nilichoka, hakunipa nafasi ya kushika simu yake hadi aikague kwanza na wakati mwingine akipigiwa anaongea akimaliza anafuta call received! Alinipangia siku za kumtembelea na masaa hasa ya usiku, hakutaka nionekane na mtu yeyote majira ya mchana, nikifika kwake kuanzia mida ya saa Mbili usiku na kuondoka saa kumi na moja ya asubuhi! Kwangu hakuwahi kuja kwangu pamoja na kumsisitiza Kisa eti yuko busy na kazi( stationary)
Tukipishana Mawazo anapanda hadi anafikia maamuzi makubwa kabisa ya kununja mahusiano! Akinimbia kitu hataki nimuulize mwingine ili nijue ukweli hata ka ni rafiki yake, atadai eti kwa kuwa simuamini niachane nae ili niende kwa ninaowaamini! Nilichka nikakubaliana na maamuzi yake ya kuvunja mahusiano lakini bado no maamuzi yanaoutesa moyo wangu!! Nashindwa kabisa kumsahau coz nilimpenda sana pamoja na maasibu aliyonofanyia!
Duhhh! Nifanyeje? Ukishawahi kukutwa na Hali Kama hii? Ulifanyeje ukashinda?

Nishauri!
FB
Tukipishana Mawazo kidogo tu alipanda hadi anataka tuvunje mahusiano![/QUOTE]
 
Nadhani sio kwamba unampenda kiivo,sema huna ujanja wa kutafuta mwingine na huamini kama utampata!
 
Sio lazima kila unapopenda na wewe upendwe! Piga moyo konde move on with your life!
 
apendaye ni wewe angalia kero zazidi upendo au upendo wazidi kero hapo utajipanga
 
ACHANA NAE.............FULL STOP..........jipe muda utamsahau tuu,, tushukuru Mungu alitupa kusahau.....Pole
 
Achana na utoto. Hakuna mtu hapo. Ukimng'ang'ania atakupasua kichwa zaidi. kutokana na maelezo yako, huyo mtu inaonekana amekaa kibiashara zaidi na siyo wakumuwekea malengo. Kama utataka kurudi kwake, jifunze kujiridhisha kimapenzi pasipo kujiwekea commitments.
 
Mkuu FB!
Kwanza vp za masiku?

Samahani kama itakuwa ni offense ila nikiangalia hayo mahusiano yenu kwa jinsi ulivyoeleza, ni kwamba we ulichukua role ya binti na kwa bahati mbaya yeye akachukua role ya kiume.

Hebu rudi kwenye nafasi yako kama mwanaume, then take control ya mahusiano.

Kwasasa mpotezee tu wakati unajipanga, next time mkionana tena akigundua umebadilika hatokuacha hadi we utashangaa.
 
kama ni kweli hayo uyasemayo basi jitahidi uwezavyo kumsahau kwani kusoma hujui picha pia?
atakuumiza kichwa na atakupotezea muda kwa kifupi ni kuwa yuko na mtu anampenda sana kupita hata hivyo vijuice na chipsi unazo mpa na anavyoonekana anakutafutia sababu ya kijinga akubwage shukuru kwa kulifahamu mapema
songa mbele sahau yaliyo pita kwani hujui mbeleni MUNGU amekuandalia nn
 
ukipenda ucpopendwa ndio mambo yanakuwaga hivyo,,,,,just try to forget abt her!! anza maisha mapya.
 
Ebwana jG ushauri wako nomeusoma lakini sio kwamba huyu demu Niko nae, nimeshampiga chini Ila ndo nimebaki na maumivu moyoni! Naona Kama kuna window Fulani mkuu!
Mkuu FB!
Kwanza vp za masiku?

Samahani kama itakuwa ni offense ila nikiangalia hayo mahusiano yenu kwa jinsi ulivyoeleza, ni kwamba we ulichukua role ya binti na kwa bahati mbaya yeye akachukua role ya kiume.

Hebu rudi kwenye nafasi yako kama mwanaume, then take control ya mahusiano.

Kwasasa mpotezee tu wakati unajipanga, next time mkionana tena akigundua umebadilika hatokuacha hadi we utashangaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom